Kudai nauli kwenye daladala kwa kugongesha sarafu ni utamaduni ama ni kwa sheria ipi?

Malyenge

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,658
3,646
Wakuu napenda kuwasalimia kwa unyenyekevu mkubwa. Yawezekana nikawaboa na mada yangu hii lakini kwa kuwa JF ni jukwaa la busara, elimu, weledi nk., natumai nitapata majibu mazuri ya kuniwezesha kuelewa mambo haya hapa chini:
Nimeleta mada hii tuijadili kwa pamoja. Kuna huu utaratibu wa kudai nauli ndani ya vyombo vya usafiri hasa mabasi yanayofanya safari zake mijini na vitongoji vya pembeni katika Tanzania yetu. Karibu kila kona ya nchi yetu utaratibu huo hutumika, na ulianza miaka mingi sana tangu mimi nakua miaka ya 1970 nimeukuta utaratibu huu. Ni huu utaratibu wa KUGONGESHA SARAFU ikiwa ni ishara ya kudai nauli kwa abiria husika.
Kwa upande wangu nimekuwa nikiuliza je ni utamaduni ama ni sheria ipi inayoelekeza namna (hiyo) ya kudai (kuashiria nauli inatakiwa) kwa kugongesha sarafu? Na kama ni sheria haki za abiria ni zipi pindi akigongeshewa sarafu? Na lugha (sahihi) ya mawasiliano wakati wa abiria kuombwa nauli ni kugongesha sarafu tu ama na mazungumzo yanaruhusiwa?
Kama utaratibu huo ni wa kawaida katika jamii (zote) je, siku nauli ikifikia kiwango cha kulipwa kwa noti tu au sehemu wanazotumia noti (bank notes) kwa maana nauli yake imefikia kiwango cha kulipwa kwa noti na si sarafu, makondakta watadai vipi nauli? Au watakuwa wanatembea na sarafu ambazo si sehemu ya pesa za kurudisha chenji ili zitumike kugongeshea?
Nawasilisha...
 
Mi nadhani kufanya hivyo kondakta ndo anajisikia yupo kazini, lakini kwangu mimi naona ni kero tu, sidhani kama ni sheria, broo.
 
Back
Top Bottom