Kudadeki pati ya bongo movie...

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
SHEREHE ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Klabu ya Bongo Movie iliyofanyika usiku wa kuamkia Machi 17, mwaka huu ilitia fora na kila mgeni aliyepata mwaliko alifarijika kwa namna yake.
Kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe hiyo, mwenyekiti wa klabu hiyo, Jacob Steven ‘JB' alianza kutambulisha viongozi wenzake na baadaye kukabidhi kipaza sauti kwa mshereheshaji Steven Mengele ‘Steve Nyerere' kuongoza sherehe hiyo.
Baada ya kufanya hivyo, ukafuatia mpango mzima wa kukata keki, ambapo Steve Nyerere alimwalika jukwaani mtoto wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Ridhiwan Kikwete kuendesha zoezi hilo.

Kituko cha kwanza kilianza pale mwigizaji wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu' alipoambiwa ajitambulishe cheo chake na kushindwa kufanya hivyo.
"Mi' mwenzenu kusema ukweli cheo changu sikifahamu, nimepandishwa tu hapa juu," alisikika Lulu na kusababisha watu kuangua vicheko hadi pale Vincent Kigosi ‘Ray' na JB walipomsaidia kumtajia cheo chake cha mjumbe wa bodi ya Bongo Movie.

Jambo lingine ambalo lilikuwa la aina yake ni pale wageni waalikwa walipoondoka huku wakiwa wamesaza vinywaji na chakula.
"Hii sherehe ni kiboko, watu wamekula na kunywa hadi kusaza jinsi vyakula na vinywaji vilivyokuwa vingi," alisema mmoja wa waalikwa.

Mwigizaji asiyeishiwa vituko, Wema Sepetu aliendeleza upedeshee wake jukwaani baada ya kwenda kuwatuza Steve Nyerere, Single Mtambalike na JB walipokuwa wakiimba wimbo wa ‘Pesa Position' ulioimbwa na Lwambo Lwanzo Makiad.
Wema alimwaga fedha jukwaani kwa staili ya aina yake huku akiwaacha midomo wazi baadhi wa watu waliofika katika tukio hilo.

Vazi alilokuwa amevaa mwigizaji, Jacqueline Wolper liliwasisimua baadhi ya wanaume waliobahatika kuliona kwani upande wa mbele liliacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake na kufanya matiti yake kuzibwa na sidiria tu.
Tukio la mwisho katika pati hiyo lilikuwa ni lile la kutoa tuzo za heshima kwa wasanii na wadau mbalimbali waliofanikisha maendeleo ya Bongo Movie.
Waliopata tuzo hizo ni Ridhiwan Kikwete, Mbunge wa Mvomero, Amos Makala, Mama Rolaa na wafanyabiashara mbalimbali ambao tuzo zao zilipokelewa na wawakilishi wao.
Kwa upande wa wasanii, Wolper, Steve Nyerere, Mainda, Ray, JB, Richie na wengine walipata tuzo kwa mchango wao kwa kundi hilo.

1.jpg
Steve Nyerere akimpa maelekezo Wema Sepetu wakati akiingia ndani ya ukumbi.

wolperredcarpet.jpg
Wolper akikatiza kwenye 'Red Carpet'.

2.jpg
Keki ya pati hiyo.

wemanamashosti.jpg
Wema (katikati) akiwa katika pozi na mashosti wake.

5.jpg
Mwenyekiti wa Bongo Movie, JB akimlisha keki Ridhiwani.

07.jpg
Ray akijiandaa kufungua shampeini.

lulushampen.jpg
...Mambo ya shampeini hayo.

richieakinengua.jpg
...Richie akikata mauno.

maindaakinengua.jpg
...Mainda nae akionyesha ujuzi katika kunengua.

wemanazawadikamakawa.jpg
..Pedeshee Wema akimtunza Steve Nyerere.
 
Ma'actress' wa bongo movie wamejaaliwa 'vitambi' na 'manyama nyama'! mbona tofauti sana na Nollywood, Bollywood au Hollywood?!
 
Ma'actress' wa bongo movie wamejaaliwa 'vitambi' na 'manyama nyama'! mbona tofauti sana na Nollywood, Bollywood au Hollywood?!
Ni kweli mkuu bado tunaiga mambo ya wenzetu lakini tupo nyuma sana tunajitahidi lakini ni mbio za sakafuni tu hizo.
 
katika vitu nisivyovielewa ni kama hivi yaani hii nchi haki ya nani ina mambo ya hovyo kibao,alafu huyu wema mbona kakongoroka hivi ama kweli mashine noma.
 
Kumwita Wema Pedejee sio sahihi maana neno hilo hutumika kwa jinsia ya kiume pekee ila kwa jinsia ya kike ungemwita shebedee ndio sahihi..samahani kwa ufafanuzi..
 
Wabongo ni watu tusiopenda vyetu na huwa tunaponda kila kinachofanywa na wabongo wenzetu sijui ndo inataka kuwa utamaduni wetu!?
 
*************!!!!!!!!!!!!!!!?????????????????? Ujinga mtupu.
 
Ni kweli mkuu bado tunaiga mambo ya wenzetu lakini tupo nyuma sana tunajitahidi lakini ni mbio za sakafuni tu hizo.

Ni kweli mkuu siku zote huishia ukingoni lakini siku zote safari moja huanzisha nyingine na hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Ipo siku tutafika.
 
Wabongo ni watu tusiopenda vyetu na huwa tunaponda kila kinachofanywa na wabongo wenzetu sijui ndo inataka kuwa utamaduni wetu!?

Tunawaponda kwa sababu wanafanya kinyume na mila na tamaduni zetu.
 
katika vitu nisivyovielewa ni kama hivi yaani hii nchi haki ya nani ina mambo ya hovyo kibao,alafu huyu wema mbona kakongoroka hivi ama kweli mashine noma.

Too much is harmful. Unategemea asikongoroke wakati muda wote kazi kujipodoa. Uzuri wa Wema unatokana na kujipodoa. akiacha kujipodoa anakuwa kama jini.
 
Ma'actress' wa bongo movie wamejaaliwa 'vitambi' na 'manyama nyama'! mbona tofauti sana na Nollywood, Bollywood au Hollywood?!

Kwa sbabau wanajiachia sana na kupenda kula hovyo hovyo. Hawana muda wa kufanya mazoezi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom