Kuchelewa kutangaza baraza la mawaziri nin maana yake?

Ibara ya 51 (2) inasema Waziri Mkuu atateuliwa ndani ya siku 14.

Ibara ya 55 inaongelea kuhusu uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Mawaziri, lakini iko silent kuhusu muda ambao Raisi inabidi ateue hao waakulu.

Kuhusiana na Mawaziri wa zamani kama bado ni mawaziri Ibara ya 57 inaongelea tenure of office of Ministers and Deputy Ministers, A.57(2)(f) "immediately before the President elect assumes Office". So, the office of Ministers and Deputy Ministers among others things became vacant when the Chekibobu assumed that high position of the president of URT. Hivyo Masha na wenzie sio mawaziri kwa sasa.

Mkuu asante kwa maelezo yakinifu.
 
Kweli Barara la Mawaziri linachukua muda mrefu sana kutangaza,lakini sioni JK angeweza vipi kutangaza mapema. Ni lazima asubiri Wabunge waapishwe,ni lazima asubiri Waziri Mkuu athibitishwe. Lakini Rais anapochelewa kutangaza Cabinet,inaondoa utulivu katika Nchi.
Halafu kulikuwa na mawazo kwamba labda CHADEMA wangeweza kuwepo katika Cabinet. Hii ni kutoelewana kumetokea,nadhani kwa bahati mbaya kabisa. Kwa sababu,katika hitimisho la hotuba yake ya kufungua Bunge,Rais alisema ataunda Cabinet ambayo ''itawatendea haki watu wote bila kujali ni wa Chama gani cha siasa'',jambo ambalo limefanya watu wengine,mimi mmojawapo,tudhani kwamba Rais amesema ataunda Cabinet ambayo itajumuisha watu wote bila kujali wanatoka Chama gani.
Labda hiyo ndiyo iliyosababisha mpasuko CHADEMA. Kwa sababu kama CHADEMA wangetofautiana kuhusu walk out,basi,wengine wangetoka na wengine wangebaki ndani ya Bunge siku ile Rais alipoongea. Lakini kwa vile walitoka wote,inaonyesha wametofautiana baadaye,baada ya kusikia hotuba ya Rais.
Cabinet inapaswa kutangazwa upesi. Lakin fikiria Cabinet ya Iraq,ambayo haikuundwa mpaka baada ya miezi sita au tisa. Tena imeundwa baada ya walk out ya CHADEMA,ingawa hatuwezi kusema kwamba ulikuwepo uhusiano wowote kati ya Al Maliki kuunda Serikali,na ile walk out ya CHADEMA.
Ukifikiria utaona kwamba Rais asingeweza kuamua pale pale kuwaweka CHADEMA katika Cabinet. Kwa sababu hilo ni jambo ambalo lingehitaji majadiliano na wengine,labda kumuuliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Uamuzi inaelekea umeshafanyika,na labda hata sasa hivi tunavyojadiliana labda Rais anatangaza Cabinet Ikulu. Kwa hiyo tutasubiri kuona nani amechaguliwa kuwa Waziri. Yoyote atayechaguliwa sawa.Mimi sioni kwamba ni lazima wachaguliwe vijana,yoyote tu mradi awe mwadilifu. Kwa sababu ukisema wazee hawawezi kufanya kazi,itabidi useme Pope Benedict hawezi kuwa kiongozi.
Lakini mimi nadhani ingekuwa bora ,hata ikibidi kuchelewesha kutangaza Cabinet, kutazama uwezekano wa kuwaweka CHADEMA pamoja na vyama vingine katika Cabinet.
 
Kwa maelezo yako hususani sentensi ya mwisho inaelekea wewe ni muumini wa siasa za chama kimoja na huenda mpaka sasa ambapo ni miaka 18 toka kuruhusiwa siasa za vyama vingi bado huoni faida ya kuwepo vyama vingi
 
Mawaziri wa nini hata hivyo? Wengi wao huwa ni WAWEKEZAJI tu kwenye SIASA. Ingekuwa wanateuliwa nje ya BUNGE labda tungepata watu wa maana. KATIBA mpya ya wenzetu wa Kenya imewaondoa WABUNGE kwenye UWAZIRI.
 
Kumbe twaweza songa mbele bila ya kuwa na mawaziri. Sasa hebu angalieni sasa Mashangingi yote yapelekwe vijijini na Pesa hizo ziende kilimo kwanza. Bado kutakuwa na salio liende mashuleni kusaidia elimu. Wizarani makamishna watafanya kazi.
 
Wenzako wanasema katiba tuliyonayo bado ni nzuri saaan kwetu. Kwa sasa hawana mpango wa kuibadilisha!!!!
 
SHAUKU ya kujua majina ya wanaounda baraza jipya la mawaziri inazidi kuongezeka kiasi cha Ikulu kulazimika kuwataka wananchi kutokuwa na wasiwasi, huku kukiwa na taarifa kuwa Rais Jakaya Kikwete anatarajia kulitangaza leo.Tangu Rais Kikwete amteue Mizengo Pinda kuwa Waziri Mkuu, kumekuwa na shauku kubwa ya kujua wanaounda baraza hilo na kumekuwa hakuna taarifa ya siku ambayo mkuu huyo wa nchi ataweka bayana majina ya wasaidizi wake.

“Sioni s ababu ya wananchi kuwa na wasiwasi kuhusu Baraza la Mawaziri; kwani kuna jipya hapo,’’ alisema mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rais, Salvatory Rweyemamu alipoulizwa siku ya kutangazwa kwa baraza hilo. Badala yake, Salva aliwataka wananchi kutotumia muda mwingi kujadili baraza hilo kwa kuwa si mara ya kwanza kutangazwa.

“Shughuli ya kutangaza Baraza la Mawaziri ni ya rais na atatangaza atakapoamua,’’ alisema mwandishi huyo wa habari wa siku nyingi. “Nakuuliza hivi, pamoja na kutokuwepo kwa baraza la mawaziri umeshasikia Mtanzania amekufa kwa kukosa chakula. Acheni kuwatia hofu wananchi.

Rais atakapokuwa tayari atalitangaza kwa kuwa ndiye mwenye shughuli hiyo.’’ Hata hivyo, taarifa zilizolifiki Mwananchi jana zilieleza kwamba Rais Kikwete anatarajia kutangaza leo asubuhi baraza lake baada ya kazi ya ushauri wa kiufundi wa namna ya muundo wake, kukamilika jana.

Tetesi zilizolifikia gazeti hili pia zilieleza kwamba baraza hilo jipya limepunguzwa kutoka wizara 27 hadi kufikia 23. Baraza hilo pia linaelezewa kuwa na mawaziri kamili 23 wakati idadi ya manaibu inatarajia kupungua na kuwa kati ya 20 hadi 22.
Pia imeelezwa kuwa baraza hilo jipya, ambalo litakuwa la tatu kwa Rais Kikwete tangu alipoingia Ikulu mwaka 2005, litakuwa na manaibu waziri watano waliopandishwa kuwa mawaziri kamili. Vyanzo vyetu pia vimebainisha kuwa idadi ya mawaziri wanawake itaongezeka kulinganishwa na baraza lililopita na kwamba uteuzi umezingatia umri, uzoefu pamoja na uwiano wa mikoa.

Pamoja na kuwepo kwa sura mpya, idadi kubwa ya waliotajwa katika baraza hilo ni wanasiasa wakongwe ambao wengi wao walikuwamo katika baraza lililopita. Wabunge wanaotajwa kuingia kwenye baraza jipya ni Peter Serukamba (Kigoma Mjini), Anna Tibaijuka (Muleba Kusini), Samuel Sitta (Urambo Mashariki) ambaye alikuwa spika wa Bunge la Tisa, Dk Harrison Mwakyembe (Kyela) na Anne Kilango (Same Mashariki).

Wengine ni Januari Makamba (Bumbuli) ambaye alikuwa msaidizi wa Kikwete kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Salehe Pamba (Pangani), Steven Masele (Shinyanga Mjini), Gerson Lwenge (Njombe Magharibi) na Nyambari Nyangwine (Tarime).

Wengine ni Shamsi Vuai Nahodha (mbunge kuteuliwa) na alikuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Angela Mkwizu (Viti Maalum) na Amos Makala (Mvomelo) ambaye ni mweka hazina wa CCM, Said Bwanamdogo (Chalinze), Lazaro Nyarandu (Singinda Kaskazini) na Zakia Meghji (wa kuteuliwa na rais).

Akilihutubia Bunge Alhamisi iliyopita, Kikwete alidokeza kuunda serikali itakayokuwa na watu waadilifu, makini na wachapakazi hodari. Pia alisema ataunda serikali ya watu wachache ambao itakuwa na mwelekeo wa kuwa karibu na wananchi na kushirikiana nao kikamilifu katika kuleta maendeleo na kupambana na umasikini.
 
Hilo Baraza la Mawaziri linavyosubiriwa kwa hamu i dont expect any big changes same old shit
 
jamani walisha haribu tangu mwanzo,sasa wapo makini ktk kuleta baraza ambalo litakubaliwa na watu,huu ni mchakato wa maandalizi ya uchaguzi 2015,hivyo tuwape mda wajipange
ila leo jk anatangaza baraza la mawaziri lenye mawaziri 23 na manaibu waziri 5 wamepandishwa cheo kuwa mawaziri kamili
mapinduziiii daimaaaa
 
Hivi kuna watu wana shauku ya kujua baraza la mawaziri...
Si mpaka raisi aamue...!!!! Kwa ufupi hakuna jipya hapo!!!

Yale yale tu...
 
Kuna jipya wala tusijidanganye, jamaa atateua mafisadi mpaka mbaki midomo wazi. wale ambao hukutamani waingie watakuwemo.sasa hilo si ndo litakuwa jipya? Kumbuka hii ndo lala salama ya jamaa wa mitandao....fadhila lazima ziendelee.......CCM hawana haya wewe!
 
Makatibu wakuu wa wizara wapo (Civil servants wanaendelea na kazi kama kawaida kwenye wizara zenye wakurugenzi, makamishna katika idara zake). In fact, kwa katiba iliyopo, Rais anaweza kuendelea na kazi bila mawaziri ' indefinitely'. Msemaji mkuu wa serikali bungeni yupo, ambaye ni Waziri Mkuu (aliteuliwa ndani ya siku 14 kwa mujibu wa katiba!) Kuna jambo lolote wabunge watataka majibu, Waziri Mkuu atapeleka ombi la jibu kwa Katibu Mkuu wa wizara husika...jibu linaletwa.... mchezo unaendelea.....Siku ya bajeti...Katibu Mkuu Fedha, analeta bajeti, inasomwa na Waziri Mkuu.....Sianaweza hata kuongozewa hiyo 'portfolio'. Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha.

Rais, kwa mujibu wa katiba yetu ya sasa (hamna muda maalamu wa kutangaza 'Cabinet'), anauwezo wa kuteua mawaziri wachache na kusema wengine tutaendelea kufikiria kama tutahitaji msaada wowote katika utendaji wa wizara husika. Makatibu Wakuu wa Wizara wanaweza kuripoti moja kwa moja kwa Rais (Ndiye aliyewateua!) Vilevile anaweza kuchagua waziri mmoja atakae simamia wizara mbili, tatu, nne, n.k (kama Rais ataamua kuendelea na wizara zilezile kutoka cabinet iliyopita. Mambo ya kuunganisha wizara situnayajua. Katiba ya sasa haina 'instructions on fixed format of cabinet'!). Mfano Mhe. X anaweza kuteuliwa kuwa Waziri wa Maji, Mifugo, Kilimo, na Miundombinu - Katibu Mkuu mmoja na manaibu Katibu Wakuu kama watakvyohitajika 'to oversee day-to-day operations' za Mifugo, Kilimo, n.k.). Rais anaweza kuform a cabinet of 5 ministers!
 
Back
Top Bottom