Kuchelewa kutangaza baraza la mawaziri nin maana yake?

Urais wa Kikwete ni jina - there are people who driving him remotely. Naamini those guys hawajaamua atangaze. Hivyo omba waamue mapema ili JK atangaze mapema.
 
Wakuu hivi ndani ya katiba yetu kuna time limitation kuhusu kutangaza baraza la mawaziri? Say Raisi anaaamua kukaa miezi mitatu bila kulitangaza kuna namna yeyote anaweza kuwa anakiuka sheria.

Je leo hii November 23, 2010. Mawaziri wa zamani bado ni mawaziri? Mfano Masha ni waziri wa mambo ya ndani bado?
 
nchi bado haina serikali iliyokamilika
 
Ndo maana Mbowe na Chadema wanadai katiba. Katiba inampa Raisi siku kumi na 5 toka amteue waziri mkuu awe ameteua baraza la mawaziri. So the guy inakunywa kahawa kwanza hilo baraza baadaye
 
Wakuu hivi ndani ya katiba yetu kuna time limitation kuhusu kutangaza baraza la mawaziri? Say Raisi anaaamua kukaa miezi mitatu bila kulitangaza kuna namna yeyote anaweza kuwa anakiuka sheria.

Je leo hii November 23, 2010. Mawaziri wa zamani bado ni mawaziri? Mfano Masha ni waziri wa mambo ya ndani bado?

Nchi hii haina Rais, ila ina mtu anayeona fahari kuitwa Rais.
 
Haya ni kati ya mapungufu lukuki yaliyokuwepo katika katiba yetu lakini watu wamekuwa ving'ang'anizi katika kuibadili.
 
Kimsingi mimi Rais wangu ni Dr. W.P. Slaa, mtu ambaye ni mzalendo mwenye kujali wanyonge, mpenda haki, na anipenda hii nchi na watu wake kwa dhati.

Tumuunge mkono na wabunge wake 48 aliowapata, maana huyu JK hana mpango na mtanzania wa kawaida kwake issue ya msingi ni kutetea ufisadi.

umenena Stein, tupo pamoja.
 
Jana Raila Odinga katuambia waziwazi suala katiba ni shauri yetu watanzania lets wake up guys. Tunao fahamu tutoe elimu ya uraia kwa wenzetu ili likija wawe wamefumbuka. ebu ona upungufu kama huo.
 
Miongoni mwa mambo ambayo KATIBA MPYA italazimika kuzungumza wazi wazi ni pamoja na Time-Frame ya serikali kufanya mambo.

Baraza la mawaziri iwepo ndani ya kipindi gani kuundwa, na iwe na mawaziri wangapi, na utendaji wao utafanyiwa vipi tathmini na wananchi kwa uwazi kabisa. Bado FFU wanapangwa kila pembe ya nchi, jamani wizi ni mbaya sana tena inatesa.

Mataifa yanayotoa misaada inasubiri kwa hamu kuona baraza ndogo na inayoundwa na sura halisi ya demokrasia lakini kwa uchakachuaji huu, tusubiri mijeledi kwa sana.
 
Ibara ya 51 (2) inasema Waziri Mkuu atateuliwa ndani ya siku 14.

Ibara ya 55 inaongelea kuhusu uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Mawaziri, lakini iko silent kuhusu muda ambao Raisi inabidi ateue hao waakulu.

Kuhusiana na Mawaziri wa zamani kama bado ni mawaziri Ibara ya 57 inaongelea tenure of office of Ministers and Deputy Ministers, A.57(2)(f) "immediately before the President elect assumes Office". So, the office of Ministers and Deputy Ministers among others things became vacant when the Chekibobu assumed that high position of the president of URT. Hivyo Masha na wenzie sio mawaziri kwa sasa.
 
SHAUKU ya kujua majina ya wanaounda baraza jipya la mawaziri inazidi kuongezeka kiasi cha Ikulu kulazimika kuwataka wananchi kutokuwa na wasiwasi, huku kukiwa na taarifa kuwa Rais Jakaya Kikwete anatarajia kulitangaza leo.Tangu Rais Kikwete amteue Mizengo Pinda kuwa Waziri Mkuu, kumekuwa na shauku kubwa ya kujua wanaounda baraza hilo na kumekuwa hakuna taarifa ya siku ambayo mkuu huyo wa nchi ataweka bayana majina ya wasaidizi wake.

"Sioni s ababu ya wananchi kuwa na wasiwasi kuhusu Baraza la Mawaziri; kwani kuna jipya hapo,'' alisema mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rais, Salvatory Rweyemamu alipoulizwa siku ya kutangazwa kwa baraza hilo. Badala yake, Salva aliwataka wananchi kutotumia muda mwingi kujadili baraza hilo kwa kuwa si mara ya kwanza kutangazwa.

"Shughuli ya kutangaza Baraza la Mawaziri ni ya rais na atatangaza atakapoamua,'' alisema mwandishi huyo wa habari wa siku nyingi. "Nakuuliza hivi, pamoja na kutokuwepo kwa baraza la mawaziri umeshasikia Mtanzania amekufa kwa kukosa chakula. Acheni kuwatia hofu wananchi.

Rais atakapokuwa tayari atalitangaza kwa kuwa ndiye mwenye shughuli hiyo.'' Hata hivyo, taarifa zilizolifiki Mwananchi jana zilieleza kwamba Rais Kikwete anatarajia kutangaza leo asubuhi baraza lake baada ya kazi ya ushauri wa kiufundi wa namna ya muundo wake, kukamilika jana.

Tetesi zilizolifikia gazeti hili pia zilieleza kwamba baraza hilo jipya limepunguzwa kutoka wizara 27 hadi kufikia 23. Baraza hilo pia linaelezewa kuwa na mawaziri kamili 23 wakati idadi ya manaibu inatarajia kupungua na kuwa kati ya 20 hadi 22.
Pia imeelezwa kuwa baraza hilo jipya, ambalo litakuwa la tatu kwa Rais Kikwete tangu alipoingia Ikulu mwaka 2005, litakuwa na manaibu waziri watano waliopandishwa kuwa mawaziri kamili. Vyanzo vyetu pia vimebainisha kuwa idadi ya mawaziri wanawake itaongezeka kulinganishwa na baraza lililopita na kwamba uteuzi umezingatia umri, uzoefu pamoja na uwiano wa mikoa.

Pamoja na kuwepo kwa sura mpya, idadi kubwa ya waliotajwa katika baraza hilo ni wanasiasa wakongwe ambao wengi wao walikuwamo katika baraza lililopita. Wabunge wanaotajwa kuingia kwenye baraza jipya ni Peter Serukamba (Kigoma Mjini), Anna Tibaijuka (Muleba Kusini), Samuel Sitta (Urambo Mashariki) ambaye alikuwa spika wa Bunge la Tisa, Dk Harrison Mwakyembe (Kyela) na Anne Kilango (Same Mashariki).

Wengine ni Januari Makamba (Bumbuli) ambaye alikuwa msaidizi wa Kikwete kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Salehe Pamba (Pangani), Steven Masele (Shinyanga Mjini), Gerson Lwenge (Njombe Magharibi) na Nyambari Nyangwine (Tarime).

Wengine ni Shamsi Vuai Nahodha (mbunge kuteuliwa) na alikuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Angela Mkwizu (Viti Maalum) na Amos Makala (Mvomelo) ambaye ni mweka hazina wa CCM, Said Bwanamdogo (Chalinze), Lazaro Nyarandu (Singinda Kaskazini) na Zakia Meghji (wa kuteuliwa na rais).

Akilihutubia Bunge Alhamisi iliyopita, Kikwete alidokeza kuunda serikali itakayokuwa na watu waadilifu, makini na wachapakazi hodari. Pia alisema ataunda serikali ya watu wachache ambao itakuwa na mwelekeo wa kuwa karibu na wananchi na kushirikiana nao kikamilifu katika kuleta maendeleo na kupambana na umasikini.

Mwananchi
 
Siwezi kusoma Katiba iliyosainiwa na Andrew Chenge.

Ina maana katiba inayoongoza nchi yetu ilisainiwa na Chenge huyu huyu????
kweli JF inatufumbua macho.
ila inabidi mtu kuwa jasiri kusoma pumba zoooote, kisha kuchuja upate mchele huo kidogo.
asante kwa kunifumbua macho
 
Back
Top Bottom