Kuchapwa kwa Maggid Mjengwa ni fundisho kwa waandishi KANJANJA?

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,269
675
[h=3]
images

kisa na mkasa cha mwaka champata Maggid Mjengwa[/h]Ndugu zangu,Hizi si habari njema. Juzi alhamisi kunako saa kumi na mbili na nusu asubuhi nilipatwa na balaa la barabarani.Ilikuwaje? Niliondoka Iringa Jumatano jioni kuelekea kijijini kwetu Nyeregete. Nilifika Madibira, Mbeya jioni ya saa kumi na mbili na nusu. Kwa vile giza lilikaribia, nikaamua kulala kijijini Mahango, nyumbani kwa ndugu yangu aitwaye Salim Raphael Mjengwa.

Alfajiri tukaondoka pamoja maana naye alitamani kufika kijijini Nyeregete kumsalimu baba yake mzazi. Tukiwa katikati ya pori eneo la Ikoga kuelekea mji wa Rujewa nikabaini gari iliyokuwa ikija nyuma yetu kwa mwendo wa kasi.Nikamwambia ndugu yangu Salim juu ya uwepo wa gari nyuma yetu. Akaniambia kuwa ni basi dogo la abiria. Kupitia sight mirror nikamwona dereva wa nyuma yangu akijaribu kunipita mahali pasipostahili na kwa mwendo wa kasi. Kwa vile barabara ilikuwa ni nyembamba sana , basi, akalazimika kukatisha jaribio la kunipita.Baada ya mwendo wa nusu kilomita hivi nikapaona mahali muafaka pa kuegesha gari yangu pembeni kumruhusu apite.


Nikawasha indiketa, nikaweka gari yangu pembeni.Dereva yule akapita na kusimamisha gari yake katikati ya barabara. Akatoka kunifuata. Nami nikaanza kujiandaa kufungua mlango na mkanda wangu ili nitoke tuongee.Kabla hata sijafungua mlango, yeye akauvuta mlango wangu na kunishambilia kwa ngumi usoni. Nikainamisha uso wangu kwenye usukani. Nikasikia pia ndugu yangu Salim akitamka; " Seme unafanya nini?" Salim alimfahamu kwa jina dereva huyo, anaitwa Seme. Mara, dereva mwenzangu akaacha kunishambulia na kunitukana.

Nikainua kichwa. Nikamwona akiondoka huku kundi la vijana waliokuwa abiria wake nao wakirudi kwenye gari lao. Walikuja kushiriki shambulizi dhidi yangu.Walikuwa na dhamira mbaya sana. Kama si uwepo wa ndugu yangu Salim ambaye wote walimtambua hadithi ingekuwa nyingine.Tulipofika Rujewa nikaripoti tukio hilo kituo cha Polisi Mbarali. Dereva mwenzangu naye akafika kituoni. Afande Mwamakula, ambaye ni mkuu wa kituo aliweka wazi kuwa alichofanya dereva yule ilikuwa ni jinai.Kwa vile nilihitajika kufika kijijini kumwona mgonjwa aliye taabani.

Na kwa vile nilihitajika kurudi Iringa kupokea ugeni kutoka Ubalozi wa Sweden. Na kwa vile dereva yule alikiri kosa lake na kuniomba radhi. Na kwa vile dereva yule aliweka wazi kuwa ni msomaji wa makala zangu, basi, nikaamua kutoendelea na shauri lile. Nilimsamehe kwa kumwambia; hupaswi kufanya tendo kama lile kwa mtu yeyote yule. Ule haukuwa uungwana.

Wenu,Maggid Mjengwa,Iringa.
 
sasa hapo fundisho wakiona mtu anataka ovatake wampishe au? Wajifunze kukwepa ngumi kaka hao waandish makanjanja wajifunze lip.?
 
nimeisoma hii kwenye blog yake. sijui jamaa walikuwa na lengo gani wallahi
 
hahahahaha.....aseeeee!! Pole sana bana, nikija irg nitakununulia mdudu hapo vibanda umiza vya ccm.......lakini ccm kwa uwekezaji wa vibanda vya mdudu ni noma.
 
Mi mara nyingi huwa against na huyu mtu, lakini kwa hili mleta maada umegeuka kuwa kama watangazaji wa klauz, Sasa kama barabara ilikuwa nyembamba alitakiwa afanyaje? Wat if angemruhusu afu Jamaa akasababisha ajali, ulitaka MjengwA achukue lawama? Acheni unazi usio na mantiki aseee..:(
 
Inakuaje kosa la jinai la shambulio kama hilo liishe juu juu namna hiyo? hata kama mshtakiwa aliomba radhi bado Majid Mjengwa alistahili kujua sababu za kushambuliwa kwake. Nadhani kuna kitu zaidi ya shambulio na msamaha
 
Title na habari vinaonyesha mleta mada umeileta kiunafiki na kimbea kutulazimisha tumuone Maggid mbaya na tumshambulie
May be i miss something here, hebu unganisha dot hilo la fundisho kwa waandishi kanjanja na matukio ya ugonvi wa barabarani
 
kweli sikupoteza muda kujifunza GUJURU!! Huyo dereva angenikoma! Ningempa Ushiro Mawashi moja tu Chali! Pambaf zake!!
 
kweli sikupoteza muda kujifunza GUJURU!! Huyo dereva angenikoma! Ningempa Ushiro Mawashi moja tu Chali! Pambaf zake!!

Hua napenda sana baadhi ya style za karate kama vile Age-uke, Uchi-uke, gedan-zuki
 
Sasa kama kamsamehe na hakupress charges nia ya kuandika ni nini?

Mwanahabari anatakiwa kutojifanya yeye kuwa habari unless it is absolutely necessary and there is a greater reason than one's own emotions and ego.

Angekuwa anaongelea elimu ya udereva na umuhimu wa madereva kudhibiti "road rage" ningemuelewa.

Angekuwa anasema kuna a grand political conspiracy against him kwa sababu kawaandika watu vibaya, na hili linaingilia uhuru wa waandishi wa habari, ningemuelewa.

Lakini sioni story. Naona kama vile anasema kamsamehe wakati bado hajamsamehe na ndiyo mana kamuumbua kwa jina.

Maggid, ukisamehe una move on. Ukirudia rudia palepale kwa kuandika andika kwenye mitandao story za mtu local hata hatumjui bila hata ya kum link na a greater narrative hujasamehe bado.

Unakuwa bado uko katika personal squabbles with the local village ignoramus ambaye anakuvamia kwa fist fight bila kujua kwamba unaweza kuwa na a fully loaded M16 pembeni ya kiti hapo. Ukamfyatua na ku claim self defense quite rightly.
 
Pole sana mjomba, hao ndo madereva wa daladala bwana. Ungemruhusu tu apite kwa juu kama alikuwa na haraka. Vipi kuhusu leseni, alikuwa nayo?
 
title haiendani kabisa na habari

But Maggid needs to change, mara nyingi anajiweka kama center of attraction, niliwahi kusema jamaa ni drama queen
 
Mimi namjua Mjengwa kupitia makala zake, lakini kichwa cha habari hakifanani na habari yenyewe au ndiyo ile style ya udaku ya kuuza gazeti kwa kichwa cha habari, au alimaanisha iwe fundisho kwa madereva kanjanja kwa maana Mjengwa ni dereva kanjanja sehemu ya kutoa site mwenzake apite yeye aliona hapatoshi, nina wasiwasi na hilo zoezi zima kuwa Mjengwa anaweza kuwa alifanya makosa fulani ambayo hayajawekwa wazi na mleta habari, vinginevyo ifafanuliwe tu.
 
Sasa kama kamsamehe na hakupress charges nia ya kuandika ni nini?

Mwanahabari anatakiwa kutojifanya yeye kuwa habari unless it is absolutely necessary and there is a greater reason than one's own emotions and ego.

Angekuwa anaongelea elimu ya udereva na umuhimu wa madereva kudhibiti "road rage" ningemuelewa.

Angekuwa anasema kuna a grand political conspiracy against him kwa sababu kawaandika watu vibaya, na hili linaingilia uhuru wa waandishi wa habari, ningemuelewa.

Lakini sioni story. Naona kama vile anasema kamsamehe wakati bado hajamsamehe na ndiyo mana kamuumbua kwa jina.

Maggid, ukisamehe una move one. Ukirudia rudia palepale kwa kuandika andika kwenye mitandao story za mtu local hata hatumjui bila hata ya kum link na a greater narrative hujasamehe bado.

Unakuwa bado uko katika personal squabbles with the local village ignoramus ambaye anakuvamia kwa fist fight bila kujua kwamba unaweza kuwa na a fully loaded M16 pembeni ya kiti hapo. Ukamfyatua na ku claim self defense quite rightly.

Nadhani anatafuta namna flani ya Promo, besides,tunapata story ya upande mmoja tu (wake) hatujapata side ya dereva to what a ctually happened. The way I see hapa Mjengwa is only trying to pull the truth to his side
 
Back
Top Bottom