Kuchangia harusi kukomeshwe

kwakweli limekuwa jambo sugu na limewalemaza wengi watu wanapanga harusi ya 7mil 10 mil yy anatoa laki 2 tu imeshajangeka akilini kwamba arusi ni garama sana mpaka uwe na mamilioni mtu kalipa mahari,kanunua pete za arusi, nguo zenu zote za arusi kila kitu tayari lakini awezi kufungisha ndoa mpaka afikirie namna ya kuwalisha watu 300 au zaidi mwisho wanaishia kumimbishana nafikiri ipo aja sasa ata viongozi wa dini kuhamasisha wanandoa kama mtu amejipanga vizuri kwa vitu vya msingi wafungishwe ndoa waende om waandae kipati cha familia mbili na marafiki bila mchango wa mtu jamani hii ndio wazo langu na ukifika wakati wangu nitafanya na nitatangaza hapa na nitaomba wawakilishi from jf
 
Tuna harusi/send-off kama 4 za wanaJF hadi sasa tunapoongea(wametangaza nia)...Kwa kauli hizi mnataka kusema nini?Kwa asili, kusaidiana katika jamii za kiafrika katika matukio yoyote ya kijamii ni kawaida. Wala tusianze kulaumiana leo. Kwa asili ilikuwa mtu anapokuwa na harusi watu huleta viti, majamvi na huduma physical!...Kibaya ni sasa hivi kufikia hatua ya kupanga kiasi cha msaada ambao mtu anataka kusaidiwa!..Naandika hivi nikiwa na kadi 5 za harusi na vipaimara zenye limited-mchango!..Inaniumiza na kunifilisi, lakini sina jinsi ya kujikwamua!..Anyway, itachukua muda sana!
 
mkuu umeowa/olewa wewe?. I wish unge kuwa bado halafu ikifika uwe wakwanza kudhubutu

Sijaoa bado... wakati uiwadia(mola anipe uzima na afya njema), moja ya maamuzi yangu ni kutoomba wala kutosumbua watu na michango... anaetaka atoe akijisikia!! nimejifunza kwa kushiriki katika shughuli(maandalizi ya harusi) za wenzangu... zenye gharama ndogo na kubwa,. Ukweli utabaki palepale.... wakati wa kusitisha michango umefika!!!!!

Nakubali kukosolewa!!
 
Kweli kabisa. Hii michanog ya harusi kwa sasa imekuwa ni kero. Hebu fikiria kwa mwaka unachangia harusi jumla sh ngapi. Katika michango yako jumlisha zawadi na hela ya mafuta au nauli ya TAX ya kuhudhuria harusi maana huwa zinafanyika usiku.

Baada ya hapo fikiria iwapo una wazazi wako kule kijijini je, kwa mwaka unawasaidia kasi gani cha fedha? Au msikitini au kanisani unamtolea Mungu wako kiasi gani?

Kuchanga ni chaguo lako haujalazimishwa. Mimi sichangiagi, nilishaacha na wananijua
 
Kuchanga ni chaguo lako haujalazimishwa. Mimi sichangiagi, nilishaacha na wananijua

Mr Chupaku sawa kuchangia ni uamuzi wa mtu lakini ipo haja ya kuelimishana kwa wale wanao jiandaa kutengeneza kadi za mialiko ya vikao au kutafuta pesa ya vocha za simu ilikualika watu watumie pesa hizo kujiandalia harusi zao wenyewe bila kuwapa mizigo watu wengine.Utamaduni wa kusaidian ni mzuri lakini tutoe kipaumbele kwenye matatizo kama magonjwa au elimu.Mtu anayetaka fanya harusi ya kifahari ajiandae mwenyewe ilituweze kubali uwezo wake.
 
Naomba kana kuna mtu yeyote aliyefunga pingu za maisha na kufanya tafrija "reception" bila kuchangiwa atueleze inawezekanaje? Against all oDDS
 
kwa kuwa huyu jamaa hajaoa

ngoja mda wake ufike, labda aolewe yeye!!!!!!!

usiweke mada hapa ili ugongewe sanks
 
Tuna harusi/send-off kama 4 za wanaJF hadi sasa tunapoongea(wametangaza nia)...Kwa kauli hizi mnataka kusema nini?Kwa asili, kusaidiana katika jamii za kiafrika katika matukio yoyote ya kijamii ni kawaida. Wala tusianze kulaumiana leo. Kwa asili ilikuwa mtu anapokuwa na harusi watu huleta viti, majamvi na huduma physical!...Kibaya ni sasa hivi kufikia hatua ya kupanga kiasi cha msaada ambao mtu anataka kusaidiwa!..Naandika hivi nikiwa na kadi 5 za harusi na vipaimara zenye limited-mchango!..Inaniumiza na kunifilisi, lakini sina jinsi ya kujikwamua!..Anyway, itachukua muda sana!
Kwenye hiyo list ya watu kama 4 najiongeza na mimi kama 5. Kwa kweli itakavyokuwa ni hivyo hivyo tu. Nikiandaa chai na sambusa moja moja kwa watakaoniunga mkono nadhani itakuwa inatosha.
 
Unapoongelea harusi hasa ni pale watu wanapokuwa madhabahuni kukubali ama kukataa kwa upande wa wakristo na kupiga goti mbele ya walii na mashahidi kukubali. Haya yote yanayofuata ni mambo ya kufikirika na waste of resources. Michango sasa hivi imekuwa kama fashion na watu wanafikia hata kununiana makazini na mitaani kisa tu hukumchangia mchango wa harusi.

Umefika wakati sasa kusema "NO" kama nitakuwa na zawadi nitakupatia kwa mapenzi yangu. Binanfsi kuna ndugu yangu alikuwa anaoa na kilichofanyika ni wanafamilia kukaa chini na kuamua kuchangishana kwa wenye uwezo kwa ajili ya chakula kidogo na kualika marafiki kusheherekea nasi na kupiga picha za ukumbusho tu. Japo wengi walilaumu kuwa ooh! sisi wachoyo hatuwapelekea kadi za mchango tukawaambia kuwa harusi sisi ilifanyika kwenye nyumba ya ibada baada ya hapo ikawa imeisha so aliyekuwa kwenye nyumba ya ibada alijumuika nasi.
 
Yani mmenigusa. Nimekuwa naumiza kichwa siku zote nini nifanye ili kulazimisha watu waache huu uchangiaji wa kula na kunywa kwa masaa matatu shs laki moja za zaidi kwa kichwa kimoja. Nikienda Kempinski pia siwezi kutumia kiasi hicho cha pesa. Afadhali basi ingekuwa tunakula na kushiba, lakini hela nyingi inaenda kwa waendeshaji wa sherehe (mapambo, tarumbeta na upuuzi mwingine)..
Niliamua siku nyingi kuwa mimi binafsi nachagua pa kuchanga, na kiwango ninachotaka. Kama hawataki , basi wasinipe kadi. Nitaokoa muda wangu na hela ya mafuta ya gari kwenda huko kwenye madubwasha yao saa sita usiku. Disgusting!
Nikifunga ndoa nitaandaa sherehe kwa hela yangu, nitaallika ninaowataka, atakaenuna shauri yake. Nina ushauri kwa wana JF
- Tususie michango ya harusi kimya kimya
- Tutafute mbinu za kuua huu utamaduni (mwanasheria anaweza kushaiwishi wabunge watunge sheria, mwana saikolojia/harakati anaweza kutoa elimu, mwanamuziki anaweza kutunga wimbo/igizo nik ili kuelimisha watu nk) vyovyote intavyowezekana..
Mimi binafsi nasoma Masters sasa. Nilikuwa nadhani nifanye utafiti wangu kwenye hii sekta. Nilitaka kuonyesha mchango/uharibifu wa sherehe za harusi kwenye uchumi wa familia/taifa, kwa kuonyesha kiasi gani cha fedha, muda, nguvu vinatumika. Ingesaidia labda kufungua watu macho kuona wanachofanya. Ila nina wasiwasi kama naweza kupata ushirikiano wa kupata data (taarifa).
Kama kuna mtu ana wazo kunisaidia naomba msaada wa mawazo katika kutoa mchango wangu kupambana na hili.
Nitatembelea hapa mara kwa mara.
Asante kwa wazo la mbolea, hasa kwa vijana. Tuna mengi ya kufanya kuliko kununua bia mbili kwa shs elfu 50,000!
 
Ni vigumu sana kusema harusi zisichangiwe, hii inatokana na tabia ambayo tumejiwekea ya kutaka kufanya sherehe kubwa kubwa za harusi ambazo ni vigumu sana kwa mtu mmoja kuweza kufanya hivyo, ndio maana utamkuta mtu anatembeza bakuli la mchango (card za mchango) ili aweze kukamilisha malengo yake aliyo ta weka.....

Hivi juzi tu jamaa yangu wakaribu ali funga ndoa na harusi yake ili gharimu takribani tsh million 17, na kulikuwa hakuna pombe, kilicho ni shangaza kwenye harusi hii haikufana sana japo ili gharimu pesa nyingi sana, nimesema hivyo kwa kuwa kuna rafiki yangu alifanya harusi ya tsh million 4 tu huwezi hamini ilifana sana na watu walikuwa wengi kushinda hiyo iliyo gharimu million 17.

Nilicho jifunza hapa ni kwamba harusi unaweza kujipanga mwenyewe kwa kuigharamikia , kwa mfano hiyo ya million 4 ni pesa ndogo sana ambayo mtu unaweza kujipanga kwa mwaka mmoja na kipata na kufunga ndoa pasipo kuwasumbua watu.

Tatizo kubwa lipo kwetu wenyewe kwamba tuna taka vitu vya gharama kubwa na ambavyo hatuwezi kivi fanya wenyewe pasipo kutegemea michango ya watu.

Umefika mda sasa watanzania tu funguke macho na kufanya mambo ya maendeleo na kuachana na hizi hanasa na masaa 4/6 ambazo mwishoe ndoa ina vunjika ndani ya wiki moja huku ukiwaacha ndugu zako kwa kilala njaa kutokana na harusi yako.

Kwa wenzetu ulaya kwa jinsi nilivyoona huwa wanafanya harusi ya kawaida sana na ambayo hai gharimu pesa nyingi sana na muoaji na muolewaji ndio huwa wana gharamia kwa 90% gharama ya harusi yao,ambapo ni tofauti na huku bongo ambako utakuwa bwana harusi mara nyingine anachangiwa hadi kununua gauni la bibi harusi.
 
Umesema vema kabisa. Wazungu kwa hili la vipaumbele wanatuzidi. Sherehe zao za arusi ni za kawaida tu kama ulivyosema pamoja na kwamba wengi wao wangetaka wangeweza kufanya harusi kubwa kabisa. Lakini daima ni watu economical, wenye kupima na kuweka vipaumbele vya matumizi ya fedha.

Sisi watanzania tunasumbuliwa na ugonjwa wa pomposity, misifa, kutaka kujionesha kwamba arusi ya fulani ilikuwa kiboko bila kujali gharama kubwa inayotumika kwa shughuli hiyo. Mshindano ya kutaka kuonekana juu zaidi ndo yametukisha hapa. Watu wanajali zaidi arusi (sherehe) na si ndoa yanyewe (ibada). Shughuli nyingi zinazotumia mamilioni ya fedha ni kwa ajili ya sherehe; kitu ambacho si kiini cha ndoa (maagano ya ndoa). Watu badala ya kuhangaikia ufanisi wa ndoa itakayofungwa (maisha ya wanandoa watarajiwa) mbele ya Mungu ili idumu, iwe na mapendo na amani, wanahangaikia zaidi mavuvuzela /matarumbeta, mapambo, vinywaji ambavyo - japo ni vitu vizuri - si vya lazima kwa maisha ya wanandoa wapya.

Kumbe sasa jambo la maana jamii ielimishwe ijue vipaumbele katika maisha - vipaumbele kama familia lakini pia kama taifa. Hali ya watanzania wengi ni mbaya kiuchumi, tungeweza kuunganisha nguvu ya kuchangia maendeleo badala ya kuchangia arusi. Wenzetu kule Kenya walikuwa na tabia ya kufanya harambee kuchangia wanafunzi (sijui kama bado wanaendelea na hii) kwenda vyuo. Hapa kwetu tunachangia matarumbeta, mlo na vinywaji, nk. Tunahitaji kubadilika kwa hili. Tufanye sherehe lakini zenye kiasi bila mbwembwe za mamilioni mengi ya fedha.
 
Nasikitika kwanza kuwa pendekezo hili naliweka katika maneno ambayo hayajadailutiwa hata kidogo. Kwa maoni yangu, umefika wakati sasa wa kusema no kwa michango ya harusi, ama fedha au mda. Maoni yangu yanazingatia kuwa kwanza kuoana ni uamuzia na muhimu kwa wanaooana. Yapo mambo mengi yenye faida ambayo tunaweza kuchangiana kama vile ada za watoto mashuleni, kuhudumuia wagonjwa na kadhalika. Kama anadhani anataka kufanya harusi, basi aandae kwa fedha zake na awaalike watu waje wamuunge mkono kusheherekea, sio kuwakalisha watu kwa zaidi ya masaa 400 (e.g vikao 5 x masaa mawili kila kikao x wanakamati 20) eti wakiumiza vichwa na hela ili mtu aoe!
OUT: michango ya harusi+ubatizo+kipaimara+birthday+annivessary+ngoma+arobaini
IN: michango ya ada ya shule+yatima+wajane+walemavu+maradhi+kujenga hosp, shule,etc
 
Nasikitika kwanza kuwa pendekezo hili naliweka katika maneno ambayo hayajadailutiwa hata kidogo. Kwa maoni yangu, umefika wakati sasa wa kusema no kwa michango ya harusi, ama fedha au mda. Maoni yangu yanazingatia kuwa kwanza kuoana ni uamuzia na muhimu kwa wanaooana. Yapo mambo mengi yenye faida ambayo tunaweza kuchangiana kama vile ada za watoto mashuleni, kuhudumuia wagonjwa na kadhalika. Kama anadhani anataka kufanya harusi, basi aandae kwa fedha zake na awaalike watu waje wamuunge mkono kusheherekea, sio kuwakalisha watu kwa zaidi ya masaa 400 (e.g vikao 5 x masaa mawili kila kikao x wanakamati 20) eti wakiumiza vichwa na hela ili mtu aoe!
Wewe umeshaoa/olewa?
 
...Harusi ni ya wawili Wapendanao lakini wanaofaidika ni wenye kumbi, magari, salon, wakodisha suti na gowns za harusi, caterers na kadhalika na kadhalika!
I am now unto my third year of saying NO to this foolishness. Understandably, my decision has caused a huge rift between me and a large number of friends and relatives. I forgive them. Eventually they will come to their senses!
 
Nasikitika kwanza kuwa pendekezo hili naliweka katika maneno ambayo hayajadailutiwa hata kidogo. Kwa maoni yangu, umefika wakati sasa wa kusema no kwa michango ya harusi, ama fedha au mda. Maoni yangu yanazingatia kuwa kwanza kuoana ni uamuzia na muhimu kwa wanaooana. Yapo mambo mengi yenye faida ambayo tunaweza kuchangiana kama vile ada za watoto mashuleni, kuhudumuia wagonjwa na kadhalika. Kama anadhani anataka kufanya harusi, basi aandae kwa fedha zake na awaalike watu waje wamuunge mkono kusheherekea, sio kuwakalisha watu kwa zaidi ya masaa 400 (e.g vikao 5 x masaa mawili kila kikao x wanakamati 20) eti wakiumiza vichwa na hela ili mtu aoe!

Hivi kufunga ndoa hakuna faida kwa jamii inayokuzunguka? Wale watoto si ndio taifa la kesho. Tutakuchangiaje ada ya watoto wakati unawazaa bila mpangilio - eti kila mmoja atakuja na riziki yake. Pili tutakuchangiaje matibabu wakati unafanya ngono zembe, hautumii chandarua cha mbu, ukati kucha, unakula bila kunawa, unatupa taka ovyo - kwanza tayari nilikwisha changia yote haya kasoro la harusi kupitia TRA!

Kama alivyosema PJ, huu ni utaratibu wa siku nyingi sana, vijijini watu wakienda kwenye harusi wanaenda na unga, mchele, pombe na kadhalika; kwa mjini tunaviweka hivyo kwenye pesa, sasa kama wewe ni 'anti-social' hilo ni tatizo lako binafsi kwani kitu hiki ni 'social event'. Wewe hutaki kuchangia halafu unataka upewe mwaliko ili uokoe bajeti yako ya chakula siyo? Nasikia Kenya wahusika wanaanda ukumbi na chakula tu, mengine juu ya anayealikwa.

Ukiangalia kwa undani kiasi cha mchango unatoa mwenyewe na ni kwa ajili ya gharama zako mwenyewe katika wasaa wa kutoa pongezi kwa wanandoa. Na kwani wewe umelazimishwa? Sasa kama wewe ni anti-social subiri mambo mengine yakukute ndipo utakapo ona umuhimu wa kushiriki shughuli za kijamii. Ukipata msiba utakodi na watu wa kulia kama unazo lakini. Je, unasemaje kuhusu kuchangia misiba, lile daftari na ile sahani pale kwenye turubai?
 
Back
Top Bottom