Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Siyo swali gumu na wala siyo swali la mtego hata kidogo Jibu lake ni rahisi kweli kwani halihitaji uwe msomi wa elimu ya anga za mbali au uliyebobea katika sayansi ya Fizikia ya Nyota kuweza kutoa jibu lake. Ni swali ambalo kila mwana CCM anatakiwa awe na jibu lake na kila Mtanzania kuamua vile vile kulijibu.
Mwishoni mwa juma Rais Kikwete alizindua utaratibu wa kuchangia Chama cha Mapinduzi ili kiweze kushiriki vizuri uchaguzi mkuu na kushinda ili iweze kuongoza taifa letu kwa miaka mingine mitano. Katika uzinduzi huo lengo lao ni kuweza kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 40 ili kuweza kutimiza malengo mbalimbali ambayo yatafanikisha lengo hilo la kufanya vizuri kwenye Uchaguzi. Fedha hizi zikishakusanywa zitatumika:
- Kununua magari 60 kwa ajili ya kampeni
- Kununua pikipiki 170
- Baskeli 23,000
- Kukodi helikopta na ndege
- Matumizi mbalimbali ya makabrasha ya kampeni na uchaguzi
Ili kuweza kuchangia kwa njia ya simu mwana CCM au Mtanzania anayekiunga mkono Chama cha Mapinduzi anatakiwa atume neno CCM kwenda Namba 15377 ambapo atakuwa amechangia Shs 300, akituma neno CCM kwenda 15388 atakuwa amechangia Shs 500 na akituma neno CCM kwenda 15399 atakuwa amechangia Shs. 1000. Ni wazi kuwa CCM itatumia mbinu nyingine mbalimbali kuweza kufikia lengo hilo. Sasa tunajua ni kiasi gani kinahitajika, kitatumika vipi, na namna gani kuweza kuchangia. Baada ya kuyajua hayo hatuna budi kujiuliza kama tuchangie au tusichangie.
Kabla ya kuchangia jiulize!
Kwa vile najua watu wengi ambao ni mashabiki wa CCM watakuwa tayari kuchangia kwa sababu Rais kasema na kwa sababu wanataka chama chao kiendelee kutawala na wapo wengine ambao hawataki kusaidia upinzani ukomae na hivyo wako tayari kuunga mkono CCM basi nimeona ni vyema kujitolea kuwasaidia watu hawa ambao wana fedha na vitu mbalimbali ambavyo wako tayari kuviweka kwenye miguu ya CCM kujiuliza maswali kadhaa ambayo wakijibu ndiyo kwa yote mawili inawapasa watoe michango yao.