Kuchakaa na ufaulu mbovu wa mara secondary school

masatujr1985

JF-Expert Member
Oct 27, 2011
1,980
780
Wadau,Naandika post hii kwa masikitiko makubwa kuhusu shule ya sekondari MARA iliyopo mkoani MARA (Musoma Mjini). Kama mmoja wa ex-students wa shule hii nimebahatika kuitembelea katika kipindi cha hivi karibuni na pia kufuatilia matokeo ya ufaulu wa shule kwa miaka ya hivi karibuni. Hakika, shule imachakaa sana hata maabara ambazo shule zingine wanalilia kutokuwa nazo pale zimeota nyasi hadi mlangoni na jengo lenyewe kuonesha kama halina utunzaji thabiti. Kiujumla hali hii na ufaulu duni wa shule hii ambayo ni nembo ya MKOA, haupendezi kwa wapenda maendeleo na elimu kwa ujumla.Nilichojiuliza ni: je, kuna ombwe la uongozi katika shule hii? (maana hata kwa mkuu wa shule kumechakaa nyasi hadi mlangoni-hii inatoa picha kuwa huenda basi ndiyo sababu hata shule inazeeka majengo na kuchakaa mazingira bila attention ya mkuu). Kwa post hii, naiomba JF isaidie kutoa maoni nini hasa kifanyike na kuushauri uongozi wa SHULE hii kurekebisha hali iliyopo sasa.(NEXT time ntatoa na picha kuthibitisha haya).
 
Back
Top Bottom