Elections 2010 Kuchagua ccm ni sawa na kung'ang'ania kuendelea kutembea kwa miguu umbali mrefu.

miradibubu

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
312
84
Nimeamua kusema haya ili kuwatanabaisha wale wanaodai kwamba sisi tutachagua sisiem kwa sababu tumezaliwa katk sisiem.

Hii ni kushindwa kutafakari na wakati mwingine ni mwendelezo wa propaganda wa sisiem.
Ninawakumbusha kwamba hivi ingekuwaje wazee wetu wangeendelea kuukataa usafiri wa magari eti kwa sababu tu wamezoea kutembea kwa miguu.

Tungesitaajabu kwa muda mrefu sana. Rai yangu ni kwamba Dr. Slaa ni mbadala wa sisiem ambayo ni sawa na kutembea kwa miguu umbali mrefu.

Kuliko kuendelea kutembea kwa miguu ni bora hata ukanunua baiskeli-( Hashim wangwe, Mwitamwega, Mziray na n.k) au nunua pikipiki- Prof. Lipumba.

Lakini kama unataka kufika unakotaka kwenda hauna budi kununua gari jipya ambalo ni Dr. Slaa. Sitaki kumfananisha na ndege kutokana na ukweli wa changamoto zilizopo katika nchi yetu.
 
Back
Top Bottom