Kubenea wa MwanaHalisi yupo London kwa matibabu

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Kuna tetesi Kwamba Saed Kubenea wa mwanahalisi yupo London kwa matibabu na hali yake ni ya wasiwasi.

Inasemekana amelazwa katika hospital moja inayojulikana kama ni The Royal London Hospital huko London.

Mwenye taarifa zaidi atupe tujue maendeleo ya Mpiganaji wetu
 
Get well soon Kubenea. Hope sio Poloniumn, tunakuhitaji kuendele* mapambano ya ukombozi wa nchi toka kwa mafisadi
 
kuumwa ni kawaida sasa hmtaki aumwe? Yeye siku mbili tu hizi wakati mahospitali watu wapo hoi mwezi mzima
 
Sina habari Mkuu. Kesho nitaulizia kwa jamaa zake kujua kama kweli kaenda London ama la.
 
Kesho nitaulizia kwa jamaa zake kujua kama kweli kaenda London ama la.

NI kweli kwamba Saed Kubenea yuko London kwa matibabu. Nimeongea na ndugu yake mmoja wa karibu na kunithibitisha kuwa ni kweli mpiganaji yupo London kwa matibabu ya macho. Anatibiwa kwenye hospitali maarufu ya Moorfields Eye iliyopo mjini London. Hali yake siyo mbaya sana, ingawa imeelezwa kuwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji.

Amekuwa huko tangu 28 Februari 2012 na haijajulikana atarudini lini.

Tumuombee mungu mpiganaji arejee nyumbani.
 
Kimbunga na wengine,

Nimeongea na Kubenea dakika tano zilizopita. Facts: Kubenea yuko London kwa matibabu ya kawaida ya macho.

Maggid,

Mkuu shukrani sana. Sasa hapo tunaweza kumuombea uponaji wa haraka.

Mkuu ni yaleyale macho yaliyompeleka India baada ya kumwagiwa Tindikali?
Namuombea apone haraka na kurejea nyumbani kuwatumikia walipa kodi.
 
Kimbunga,
Karibu, nachelea kujibu swali lako maana nitakuwa nimeingilia kazi ya daktari na hakika anayepaswa kujibu swali hilo ni mgonjwa mwenyewe. Mie nimeleta ujumbe tu.

Na mjumbe auawi!

Maggid
Iringa.
 
Kimbunga na wengine,

Nimeongea na Kubenea dakika tano zilizopita. Facts: Kubenea yuko London kwa matibabu ya kawaida ya macho.

Maggid,
ahsante ubarikiwe. Ndugu saidi kubenea wewe ni mtumishi wa Mungu juu ya ukombozi wa watanzania! kama Bwana Yesu alivyomponya kipofu bartholomayo nami kwa mamlaka niliyonayo katika jina la YESU POKEA UPONYAJI SASA! AAMEN!
 
Mkuu shukrani sana. Sasa hapo tunaweza kumuombea uponaji wa haraka.

Mkuu ni yaleyale macho yaliyompeleka India baada ya kumwagiwa Tindikali?
Namuombea apone haraka na kurejea nyumbani kuwatumikia walipa kodi.

Kimbunga umeniacha hoi, kwani kubenea ana macho mengine zaidi ya yale mkuu????
 
Lamsingi tumombea kwa mola apate nafuu haraka mapambano ya ukombozi wa watu wetu yaendelee.
 
Kimbunga,
Karibu, nachelea kujibu swali lako maana nitakuwa nimeingilia kazi ya daktari na hakika anayepaswa kujibu swali hilo ni mgonjwa mwenyewe. Mie nimeleta ujumbe tu.

Na mjumbe auawi!

Maggid
Iringa.

Maggid hapo kwenye red panapunguza credibility yako ya uandishi, hivi kweli na wewe unaamanisha hauawi kwa neno hilo? Du! Viswahili vya siku hizi bwana!
 
Get well soon Saed Kubenea! Hivi ile kesi ya unyama aliofanyiwa iliishia wapi?
 
Get well or Rest in Peace! Historia ya huyu ndugu imegubikwa na unafiki! Yuko radhi kumtumikia yeyote mwenye pesa na kumsaliti yeyote!
 
Kuna tetesi Kwamba Saed Kubenea wa mwanahalisi yupo London kwa matibabu na hali yake ni ya wasiwasi.

Inasemekana amelazwa katika hospital moja inayojulikana kama ni The Royal London Hospital huko London.

Mwenye taarifa zaidi atupe tujue maendeleo ya Mpiganaji wetu

Sasa wewe ndiye umeleta taarifa hizi then unataka mwenye taarifa alete.Mkuu ungeweka wazi chanzo chako cha taarifa hizi kwanza.
 
Back
Top Bottom