KUBENEA: Nipo tayari kufa lakini nitaendelea kutetea haki za watanzania mpaka mwisho

Simba mnyama

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
348
129
"Mimi sioni kama gazeti la Mwanahalisi linaandika habari za uchochezi kama zinavyo daiwa lakini hiyo ni njama ya mtu ambaye analengo la kutaka kuwafunga mdomo waandishi wa habari ili wasieleze mambo ya kweli jambo ambalo halikubaliki," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali halisi , inayochapisha Gazeti la Mwana Halisi, Saed Kubenea, na kuongeza kuwa siyo vyema kulifungia gazeti hilo kwani habari zinazoandikwa zinafuata maadili na taaluma ya uandishi wa habari.



"Nipo tayari kufa lakini nitaendelea kutetea haki za watanzania mpaka mwisho wangu,"

Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz
 
Hivi hii trend ya Watanzania wengi siku hizi kujiapizaapiza! mpaka kieleweke, niko tayari kufa, mpaka tone langu la mwisho la damu, mbele kwa mbele; je ni ishara za watanzania kukata tamaa au kushamiri kwa mfumo wa utawala kandamizi na wa kibabe?!

Is it amaggedon, epocalypse now or a prelude to East african spring a' la Arab spring?! God save our country.
 
hivi hii trend ya watanzania wengi sana siku hizi kujiapiza apiza! Mpaka kieleweke, niko tayari kufa, mpaka tone langu la mwisho la damu, mbele kwa mbele; je ni ishara za watanzania kukata tamaa au kushamiri kwa mfumo wa utawala kandamizi na wa kibabe?!



Is it amaggedon, epocalypse now or a prelude to east african spring ala arab spring?! God save our country.

kukata tamaaa...ndo ikijaa maji huyamwaga mwingine
 
Watu wamechoka na iko siku wote wataacha magari na kutembea njiani huku kila mmoja akinena kwa lugha hapo itakuwa too late na polisi watakuwa mkumbo huo huo na mahakama nk sijui itakuwaje
 
sio lazima ufe ndo watu wakujue kama umefanya makubw au la, democrasia inapopotea zipo njia nyingi za kudai, usikate tamaa kubenea kumbuka dunia watu wanapita. tanzania sio mali ya mtu mmoja ni bali ni mali ya MUNGU kwa watanzania wote
 
Tatizo mahakama imekuwa chaka la serikali vinginevyo tungekushauri uende mahakamani ukadai haki yako ya kufunguliwa gazeti lako.
 
sio lazima ufe ndo watu wakujue kama umefanya makubw au la, democrasia inapopotea zipo njia nyingi za kudai, usikate tamaa kubenea kumbuka dunia watu wanapita. tanzania sio mali ya mtu mmoja ni bali ni mali ya MUNGU kwa watanzania wote

unadhani ni njia gani mbadala iwapo kalamu na makubuliano ya mezani vimeshindwa. Mbona historia hipo wazi ya wapigania haki kuwa ni kupoteza uhai au kumwaga damu yao pale kalamu inapogoma.
My take. A guy he iz right, kwa aliyoyanena. Lord av mercy on him.
 
mkuu kati ya magazeti nayopenda kuyasoma ni pamoja na mwana halisi nahisi serikali inahofu kuwa wananchi wamefunguka na 2015 haturudi nyuma na sisi tukishika madaraka lazi mali zote walizogawana tuzirudishe kwa wananchi
 
Siwaelewi serikali,
hivi kati ya Kubenea na waliomtesa Dr. Ulimboka, nani mchonganishi...??? By the way, uchonganishi ni nini? Kusema ukweli kuhusu yaliyotokea au ...?? Kwani, kukaa kimya bila kuripoti kilichotokea nao si uchonganishi..??? Kuongea tofauti na hali halisi si uchonganishi??
 
Back
Top Bottom