Kubenea na siasa za Kyela

Status
Not open for further replies.
Mkuu,

Moja ya watu wapole duniani ni mie. Ila ningelipewa MADARAKA basi usingeliamini kuwa ni huyu Sikonge unamfahamu.

Mie na homeboy Samuel Sitta hatufahamiani. Ila kama ningelimwambia jina la baba yangu mdogo wa Urambo basi KWA VYOVYOTE VILE ANAMFAHAMU. Kwa maana nyingine, jina la familia yetu Sitta alifahamu. Huyu bwana nimekuwa mpinzani wake mkubwa kwa UFISADI wake tangu awe CDA. Ila kama kuna siku alinifurahisha ni siku alimwambia Kikwete "AWE MKALI KIDOGO". Kwa hili brother Sitta ulizoa maksi nyingi sana kwangu.

Wakati mwingine kwa WAPUUZI kama Kubenea, ningelikuwa Rais basi si ACID tu ila ntafanya kibaya zaidi. Kama anaandika ukweli ambao kwa sababu moja au nyingine unaleta hali ya hewa mbaya kisiasa, ninaweza kumwita na kumwambia kwa nini tunaDANGANYA hivi. Ila kama anadanganya na kupotosha habari, basi lazima afahamu kuwa ACID ni cha mtoto.

Kwa upande fulani ni MPENZI wa siasa za KICHINA, hasa ukikumbuka maneno ya Kikwete mwenyewe kuwa 70% ya Watz ni MIFUATA UPEPO. Ina maana kuwa hawa watu inabidi kuwaongoza kama kondoo. Ukitegemea waende wenyewe basi utasubiri sana.

Rais Msanii na mwenye kuchekacheka muda wote hafai kwa nchi masikini. Hebu fikiri watu wanamwambia Rais aende Mtwara kufungua daraja la kwenda Msumbiji (Kubenea type) na akifika hapo anakuta daraja halijaungana. Anaishia kumtuma Mla panya Membe kwenda Msumbiji kwa kimtumbwi eti kwa sababu yeye hafahamu kuogelea. Hawa liomdanganya Rais wanatakiwa wamwagiwe kitu kibaya zaidi ya Acid. Ila kama wewe kiongozi unachekacheka, watakuwekea vidole machoni.

Kama kubenea kashaamua kuwa Mwanasiasa na anacheza Siasa kwenye uandishi wake, hamna tena huruma. Tutamlima kwa kila upuuzi wake na hatapata huruma tena. Kama alimess up na mke wa mtu zamani basi afahamu kuwa kama kama mwanasiasa sasa yeye ni CHAKULA YETU.

Mhh timu Mwakalinga wanachukua play book toka kwa mfadhili wao mkuu - Lowassa.

Hawa watu wakipewa nafasi tena, jehanamu itakuja kabla ya wakati wake. MUNGU azidi kumlinda mpiganaji Mwakyembe toka kwa mafisadi na watu wenye visasi kama hawa.
 
Mkulima Version yako ya kwanza umesema
Ogah,

Unasema Kubenea anadaiwa kusema uwongo? Ina maana wewe baada ya kusoma hapo juu na yote unayoyajua bado bado hujaona kwamba amesema uongo?

Kweli mswahili akipenda chongo huenda chengeza. Uzuri wa dunia hii, anayechafuliwa leo ni Mwakalinga na kesho utakuwa wewe au mtoto wako.

Tatizo la JF ni hilo miaka yote, hoja zinaangalia uso wa mhusika.

......hapendwi mtu hapa.......na hiyo sio tabia yangu......ukinisoma tangu mwanzo maoni yangu yalikuwa wazi......kumpongeza Mtanzania (but with exceptions).........kama kubenea akichemsha atapewa vipande vyake.....(of which Ndg Mtanzania alishaweka wazi kilichojiri)......kilichonishtua ni arrogance na immaturity shown.......na ninashtuka zaidi......ninavyoona hiyo hali inashabikiwa........

....anza hata sasa hivi kunichafua mimi "Ogah".....KAMWE sitakuja kukumwagia Tindikali.........au cha moto zaidi yake........

na version yako ya pili.......
Ogah,

Unasema Kubenea anadaiwa kusema uwongo? Ina maana wewe baada ya kusoma hapo juu na yote unayoyajua ya mwakalinga hapa JF bado hujaona kwamba amesema uongo?

Kweli mswahili akipenda chongo huita chengeza. Uzuri wa dunia hii, anayechafuliwa leo ni Mwakalinga na kesho utakuwa wewe au mtoto wako. Tatizo la JF ni hilo miaka yote, hoja zinaangalia uso wa mhusika.

Kama kungelikuwa na utawala wa sheria hao waandishi wangeachiwa kuchafua watu kila siku bila kuwajibishwa? Siku hizi usipojilinda mwenyewe na hawa waandishi njaa, hakuna atakayekulinda. Wanachukua pesa zao na kisha wanaandikiwa nini waandike.

.....ni kweli vijana wa dala dala barabarani ni wasumbufu sana/wajeuri/wanatukana matusi and things like that..........Marehemu Mh Ukiwaona Ditopile Mzuzuri........aliua hivi hivi......baada ya gari lake kugongwa......sasa hivi vitendo.......ni vya kuvishabikia jamani.......!!

..........Ni mara ngapi tumeona waandishi wakiomba radhi wazi wazi kwa makosa waliyofanya?..........ushabiki mwingine bana.........
 
mimi nilikutetea kiasi cha kufungiwa wiki moja hata pole hukunipa.

Wewe ulifungiwa kwa sababu ya kutoa lugha za matusi huku ukitishia watu kuwa utawapungia majini ya mafia whatever that means (kutumia muda mwingi madrassa kumeharibu kila kitu kichwani mwako).
 
Mheshimiwa Mwakyembe, imekuwaje mwaka huu umesusa hata Xmas Kyela?

Kutoonekana kwako kumesababisha gumzo kubwa huku. Kulikoni mheshimiwa?

Nimemwona Mwakipsile leo pale kwake akitanua na wapambe wake.

Mwakalinga vipi mbona tuliambiwa ungelikuwa Kyela wakati wa Xmas?

Hii ya Kubenea naona amefulia big time! kama anavyosema FMES.

- Mhhhhh! Mkuu wangu heshima mbele sana, Kubenea ni ndugu yangu sana sasa bado najaribu kumtafuta toka jana ili aje hapa aweke ukweli unapotakiwa, so far sijamuhukumu anybody, isipokuwa nimesema kwamba iwapo Kubenea atashindwa kujitokeza atakuwa amejiangusha sana, bado sijafikia hatua ya kuamini hivyo kwamba ameandika majungu asiyo na uhakika nayo!

- Mimi ni bin-adam huru na huwa sihitaji kusemewa na anybody kuhusu msimamo wangu on any ishus, huo uliousema hapo juu sio msimamo wangu on the conclusion ya hii article, ninashukuru sana kwamba jina langu linatajwa sana kwenye hii topic lakini please msimamo wangu nitausema mwenyewe!

- Kama ambavyo ninasubiri time itakapofika, niamue nani anafaa kutuwakilisha huko Kyela, kati ya wagombea watakaojitokeza bado tunasubiri wengine, otherwise tunaendelea kusubiri Mkulu Kubenea aje hapa, unajua mwisho wa mwaka huu na Kristmats, watu wako kwenye pilika pilika tuwape nafasi kwanza!

Respect.

FMEs!
 
FMES,

Labda umeshindwa kuelewa nilichoamaanisha. Maneno yako niliyoyatumia ni hayo ya big time! Sikuwa na maana kwamba unasema Kubenea amefulia big time.

Maneno ya Kubenea kafulia ni ya kwangu na ndio nikaongezea na msemo wako wa big time!

Kama ulielewa tofauti samahani sana, sikuwa na maana hiyo.

Nimesoma ujumbe wako wa leo na hujasema popote kwamba Kubenea kafulia, ningelikuwa nimesema hivyo ungelikuwa ni uzushi kwa upande wangu.

Nilitaka kulitumia hilo neno ambalo kwa kawaida hapa JF naona unapenda sana kulitumia la big time! kumbe nikaishia kulikoroga. Samahani kama kwa aina yoyote Kubenea ataona umemsema hovyo.
 
Nguvu kubwa na za kifedha na mikakati ya kisiasa, zinatumika kuhakikisha John Mwakipesile, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anaingia katika kinyang’anyiro cha Ubunge mwaka kesho katika Jimbo la Kyela.

Lengo ni kutaka kumtokomeza kisiasa Mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Dk. Harrison Mwamyembe, imefahamika.

Taarifa zinasema Mwakipesile anajengwa kisiasa na kiuchumi na mtandao mpana wa wanasiasa na wafanyabishara wakubwa nchini.

Miongoni mwa waliotajwa kumusimika Mwakipesile, aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo hilo ni mfanyabiashara na Mbunge wa Igunga Rostam Aziz, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Mbunge wa Bukoba Vijijini Naziri Karamagi na mfanyabaishara Shubash Patel.

Rostam, Lowasa na Karamagi ni baadhi ya majeruhi wakuu wa kashifa ya mkataba wa kufua umeme kati ya serikali na Kampuni ya Richmond Development Company (LLC) aliyoibuliwa na Kamati Teule na Bunge, chini ya Mwakyembe.

Ni kamati ya Mwakyembe iliyomzamisha kisiasa Lowassa na Karamagi, Februari 2008, huku ikimuacha Rostam katika majeraha makubwa ya kisiasa na kiuchumi.

Wengine wanotajwa kuwa nyuma ya Mwakipesile ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa w a Mbeya, Nawab Mullah na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba.

Baadhi ya vijana waliohojiwa mjini Kyela wamemtaja pia Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Cornel Apson Mwang’onda.

Matokeo haya ya uchugnuzi wa muda mrefu yamesaidia kubaini uteuzi wa mwakipesile kuwa Mkuu wa Mkoa ule ule aliopotezea ubunge 2005, kuwa kiini cha haraka zake nyingi Wilayani kyela, ambazo zimeibua malalamiko kutoka kwa Mbunguw a sasa. Dk. Mwakyembe kuwa anahujumiwa kisiasa.

Alipoulizwa juu ya juhudi hizi za kumg’oa Mwakyembe alisema kwa ufupi, “Nimekuwa nikifanya kazi za umma ulionituma. Sitishiki na yeyote anayetaka nafasi hii. Wananchi ndio waamuzi.”

Haraka za Mwakipesile kuingia kwenye kinyang;anyiro cha Ubungu mwakani zimechochea mwawazo hasi Mkoani Mbeya dhidi ya Rais Kikwete.

Kwa kumwacha Mwakipesile Mkoani Mbeya muda wote huu, kuna wanaomwona Kikwete kuwa ni “Mtu wa Visasi” na asiyepend akuzungukwa na wenye mawazo tofauti.

Rais Kikwete ameonyesha hampendi Mbunge wetu na sababu tunazijua. Mbunge wetu alimuunga mkono Profesa Mwandosya (Mark) kwenye kura za maoni za Urais mwaka 2005. Hivyo, alimteua Mwakipesile na kumbakiza Mbeya ili awakwamishe Mwakyembe na Mwandosya,” anasema mfanyabiashara katika somo kuu la Kyela, jailo Mwangego.

Madai ya Mwangego yaliungwa mkono na wafanyabaishara wengine katika soko hilo, hasa wanawake, ambao walipandisha sauti zao wakidai kuwa Rais kikwete “anamwonea” Mbunge wao na kukemea kwa kusema juhudu za kumwangusha kwa kura mwakani “zitashindwa”.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa mjini Kyela, wanawataja madiwani wanane kuwani mawakala wa mwakipesile, ambao kazi yao kubwa ni kuzunguka Wialya nzima wakigawa magazeti bure yanayochapishwa kwa lengo la kumchafua mwakyembe na kumnadi Mwakipesile na “Vijana” wake.

Vijana wanotajwa kuwa wanafaa kuchukua ubungu wa Kyela ni George Mwakalinga, Hunter mwakifuna na Elias Mwanjala. Hata hivyo, inadaiwa kuwa mwakipesile yuko nyuma ya vijana hao.

George mwakalinga ni mwanafunzi na mjasiriamali anayeishi Uingereza. Inadaiwa alifuatwa London na Mwakipesile na Mwang’onda kuombwa agombee ubungu Kyela. Mwakalinga alifika Kyela Agosti mwaka huu na kuendesha kampeni ya kujinadi kwa mwezi mzima.

“Alifanya karamu kubwa kijijii kwao katumba, Songwe, kwa kuchinja Ng’ombe , kutangazia wananchi kuwa anaingia vitani. Alitembelea kata zote na kutoa misaada ya mabati na sementi.

Taarifa kuwa aligawa fedha kuanzia shs. 10,000 hadi 100,000 kwa uongozi wa CCM wa Vijiji na Kata, hazikuweza kuthibitishwa ingawa Edson matai wa Kasumul, mpakani na Malawi anadai anajua hili kuwa ni kweli.

Kwa mujibu wa nduguzake wanaoendesha baishara kwenye jengo la Kyela Devcelopment Corporaiton (KDC) mjini Kyela, Mwakalinga alirejea London September mwaka huu na hadi leo hajarudi Kyela. Aliacha nyuma “Kamati ya kampeni” inayodiwa kuratibiwa na Mwakipesile.

.

- Anyways, ninaomba kwenda ndani zaidi na this article, ningependa sana kuona Kubenea, anakuja hapa na kutoa maelezo zaidi katika hizi sehemu nilizoziwekea alama nyekundu,

- Kwa mfano sio siri kwamba Mwakyembe, in one way or another alikuwa anatekeleza kazi ya Muungwana katika kumtwanga Lowassa, sasa iweje tena amtumie Mwakipesile kuwasumbua Mwandosya na Mwakyembe?

- Sasa ni vyema Kubenea akaja kutolea maelezo hizi habari zenye wekundu, in the meantime bado tunaendelea na juhudi za kumtafuta, maana alisema mwenyewe kwamba Mwanahalisi ni upanga kwa upanga, je ni theory for the truth au majungu?

Respect.

FMEs!
 
FMES,

Labda umeshindwa kuelewa nilichoamaanisha. Maneno yako niliyoyatumia ni hayo ya big time! Sikuwa na maana kwamba unasema Kubenea amefulia big time.

Maneno ya Kubenea kafulia ni ya kwangu na ndio nikaongezea na msemo wako wa big time!

Kama ulielewa tofauti samahani sana, sikuwa na maana hiyo.

Nimesoma ujumbe wako wa leo na hujasema popote kwamba Kubenea kafulia, ningelikuwa nimesema hivyo ungelikuwa ni uzushi kwa upande wangu.

Nilitaka kulitumia hilo neno ambalo kwa kawaida hapa JF naona unapenda sana kulitumia la big time! kumbe nikaishia kulikoroga.

- Ahsante mkuu, tuendelee kukata ishus na yamekwisha na huwa siangalii nyuma tena.

Respect.

FMEs!
 
FMES,

Kwenye hiyo habari Kubenea ana mengi tu ya kujibu. Inaelekea hata huyo Matai wanayesema alisema anajua kuwa ni kweli kwamba Mwakalinga alikuwa anatoa pesa mpaka laki moja anakataa, anasema hajawahi kuongea na mwandishi yeyote wa Mwanahalisi. Kwasasa hili tuliacha na ukweli utajulikana tu muda sio mrefu.

Hata hilo suala la kwamba Mwakipesile anashinda Kyela. Kwa taarifa nilizo nazo mimi na labda watu wa Kyela wanaweza wakathibitisha, familia ya Mwakipesile iko Kyela, hajahama kwenda nayo Mbeya. Mwakipesile anaondoka Jumatatu asubuhi kwenda Mbeya na anarudi Ijumaa usiku kurudi Kyela kwenye familia yake. Huko ni kushinda Kyela? Labda, lakini kwa maoni yangu sidhani kama huko ni kushinda Kyela. Kutoka Kyela mjini mpaka Mbeya mjini ni kama km 110. Huyu mtu angeweza hata kila siku kulala Kyela na kufanya kazi Mbeya.

Hilo la Dr. Hunter, huko nyuma jina lake liliwahi kutolewa kwa madai hayo hayo lakini CCM mkoa likarudishwa baada ya kuridhika na maelezo yake kwamba huo ndio umri wake na wao kufuatilia documents zilizokuwepo. Nafikiri kwa mwandishi wa habari angeweza kuchunguza zaidi na kuja na ushahidi kuonyesha huyo kijana kadanganya umri au la.

Mtafuteni aje atoe msimamo wake na kama amekosea awe tayari kuomba msamaha kwenye gazeti lake la wiki kesho.
 
Waooo,

Timu Mwakalinga kwa lugha za ajabu, utadhani wametumwa na Kingunge au yule mama mwenye matatizo ya akili (Sophia Simba)

Bwa ha ha ha

Eti huyu naye anajiona ana akili kuliko watanzania wenzake

Eti ananishauri kusoma ...

Bwa ha ha

Bwa ha ha ha,

Eti principal engineer wa Lucient .. so what? Lucient my foot. Yale yale ya kina Balali na Ndulu (wafanyakazi wa benki ya dunia).

Hii ndio strategy ya Mwakalinga? kurusha rusha hovyo kazi yake na kampuni yake aliyoifanyia kazi? the next thing itakuwa nini - kutaja jina la mke wake na kuanza kumsifia kuwa ni mrembo kuliko mama sophia simba?

Of course sio kwamba Mwakalinga alimpigia magoti Lowassa, alimramba vidole vya miguu pia. Pesa za richmonduli na dowans si mchezo (kwa wafanyakazi wa lucient inaonekana).

Mkuu Solomon David.
Ushauri wa bure
Nenda Darasan kaka.Unachekesha.
Ni Lucent na sio Lucient
 
- Anyways, ninaomba kwenda ndani zaidi na this article, ningependa sana kuona Kubenea, anakuja hapa na kutoa maelezo zaidi katika hizi sehemu nilizoziwekea alama nyekundu,

- Kwa mfano sio siri kwamba Mwakyembe, in one way or another alikuwa anatekeleza kazi ya Muungwana katika kumtwanga Lowassa, sasa iweje tena amtumie Mwakipesile kuwasumbua Mwandosya na Mwakyembe?

- Sasa ni vyema Kubenea akaja kutolea maelezo hizi habari zenye wekundu, in the meantime bado tunaendelea na juhudi za kumtafuta, maana alisema mwenyewe kwamba Mwanahalisi ni upanga kwa upanga, je ni theory for the truth au majungu?

Respect.

FMEs!
.

FMEs,
Ninakuunga mkonono kwa 100%.Kubenea ajitokeze na atuambie nini alichoandika.Huo ndiyo Uungwana.Kama aliteleza au hiyo habari imeandikwa na MWAKYEMBE mwenyewe aseme.Nimepata PM nyingi sana zinasema Kubenea ni mtu makani sana na Hiyo Taarifa imeandikwa na Mwakyembe mwenyewe.
 
Pole sana kanda2. Niliowataja ni wale ambao nafahamiana nao kwenye real life na niliongea nao nilipokuwa Tanzania na wakasaidia kufikisha ujumbe wangu JF.

Kuna wengi walinitetea na nawashukuru sana. Ila Kanda2 si ni wewe uliyesema nimeahidi kutoa laptops shule zote Kyela? Sijawahi kusema kitu kama hicho mahali popote au kwa mtu yeyote. Je ulitoa wapi maneno kama hayo? Kama sio wewe basi samahani sana. Kuna watu wengi tu waliamini mimi nimesema kitu kama hicho hasa kwa wale ambao hawanifahamu. Mimi siahidi jambo lolote na kama kuna kitu nataka kutoa basi natoa kwanza kabla ya ya kuwaambia wananchi. Kule vijijini ukiahidi kitu watu wanategemea utekeleze. Mimi sina uwezo wa kutoa laptops kila shule na kama ningesema hivyo ungelikuwa usanii tu ambao mimi mwenyewe naupinga hapa kila siku.

Kuna wakati nilitaka kuomba shirika fulani huku lisaidie vitabu kule Kyela. Wakanipatia forms zao ambazo ilikuwa ziwekwe sahahi na walimu wa shule husika (shule tano). Na kweli kule Kyela walimu wakasaini na kuzirudisha. Bahati mbaya huo msaada wa vitabu ukaunganishwa pamoja na maombi mengine na kukabidhiwa WAMA ambao nao wakavipeleka kule walikotaka wao. Kule Kyela ikawa kasheshe, pamoja na kuwaambia mwanzoni kwamba tunajaribu na chance ya kupata ni kama 10%, wao waliamini hivyo vitabu vimepatikana. Baada ya muda yakaanza maneno ya chini chini kwamba nimewatapeli. Ikabidi nitoe pesa yangu mfukoni na kuwanunulia vitabu hapo Dar. Hapo ndio maneno yakaisha ila nikawa nimejifunza kwamba huko nyumbani watu wanafikiri kila mtu ni mwizi na kwamba kila ukiomba kitu nje utapewa. Usiahidi kitu hata siku moja maana utawapa matumaini watu bure wakati huenda usifanikishe. Fanya kila kitu kimya kimya na kikiwa tayari ndio waambie.

Hata halmashauri ya wilaya walishawahi kusaini barua yetu fulani ya kuomba msaada fulani ambao kwa leo sitautaja. Baada ya muda wakaanza kusema kumbe nao akina Mwakalinga ni wasanii. Barua zote kutoka chombo cha serikali kilichokuwa kinashughulikia usajili wao walikuwa wanapewa copy lakini bado hawakuamini. Siku tumefanikisha, watu waliona aibu kama nini. Mkuu mmoja ndio akasema wazi kwamba hata yeye alishaanza kuamini na sisi ni wasanii lakini sasa tumemuumbua hata yeye na ni jambo zuri kwetu maana wale wote waliokuwa wanasambaza hayo maneno sasa ndio wanaona aibu kubwa.

Ku deal na watu wa wilayani ni ngumu sana, inatakiwa elimu kubwa ili waelewe na waunge mkono juhudi za kusaidiana nao kujiletea maendeleo yao. Hata michango wanayotoa inatakiwa kuwe na uwazi mkubwa mno ili kila mtu aone kila senti imeenda wapi, vinginevyo watalia ufisadi hata pale ambapo hakuna ufisadi.
MKUU kwa hiyo hukunishukuru kwa vile hunijui kwenye Real Life? kufungiwa kwangu hakukusumbua kichwa kwa vile mimi hunijui? kazi yangu hukuiona hapa?

Anyway nilisema kuhusu Laptop kwani tulikuwa kwenye kampeni kama unaingia kwenye siasa lazima ujue mbinu za siasa huwezi kuwa smart kwa siasa za Tanzania au Africa.Obama kuna mambo aliyasema lakini kiutendaji ni magumu.

suala la Laptop niliamini unaliweza kutokana na fani yako.kutoa Laptop kwa kila shule ya sekondari Kyela sio issue,kwani mimi ndio niliyesema baada ya kujiingiza kwenye timu yako.sasa ilikuwa uniulize hivi vitu tutapata wapi? na kama unataka hizo Laptop mimi naweza kukutafutia hadi 40 moja kila shule.nitafute kwenye PM kama una nia na vitu hivyo sawa.
 
Kanda2,

kampeni za namna hiyo hapana, hata kama ni Afrika.

Hatuendi kudanganya watu, tunaenda kufanya yale tunayoyaamini. Hata kama una uwezo wa kutoa laptops 40, bado ungetakiwa kujadiliana na mimi kwanza kabla ya kusema mimi nimetangaza kwamba nitatoa hizo laptops.

Sijui ya mungu, hata mimi naweza kutafuta hizo laptops lakini kwasasa sio priority na kuna mambo mengine ambayo ni muhimu zaidi.

kwa kusema mimi nimeahidi kutoa laptops bila mimi mwenyewe kusema hivyo, tayari watu wengi walishaamini mimi ni mwongo ninaposema siahidi kitu.

Ni bora umethibitisha mwenyewe kwamba mimi sikuahidi mahali popote kutoa laptops na hata sasa siahidi hilo.

Siku hizi kuna idea mpya ambayo ni bora inaitwa no pc. Ni bora hiyo kuliko hata laptops.

Pole sana kwa kufungiwa japo sijui ulifungiwa kwasababu zipi. Kuna wengi walinitetea na mbona hawakufungiwa?
 
Mhh timu Mwakalinga wanachukua play book toka kwa mfadhili wao mkuu - Lowassa.

Hawa watu wakipewa nafasi tena, jehanamu itakuja kabla ya wakati wake. MUNGU azidi kumlinda mpiganaji Mwakyembe toka kwa mafisadi na watu wenye visasi kama hawa.

Ungelikuwa na dada Mzuri ningelifahamu unataka niwe SHEMEJI yako.

Na kwa sababu nimeshaowa miaka mingi na sitaki kuwa Muislaam, basi nipishie mbali mwana wa Itimba aka Sikonge.

Kama ulikuwa unanitafuta basi utanipata. Na hivi nataka nifungiwe kwa miezi mitatu baada ya mwaka mpya (David Beckham style), nisije nikakuangukia kwa lugha za wabeba Lami na Zege.

Hao Maruhani wako wa kusema mie ni wa Lowassa, itabidi ushukuru Mungu kama utaishia kumwagiwa ACID. Ntamtafuta mkeo au girlfriend wako....... Ukishapata donge, tuone kama utakuwa unachekacheka hivi na kutuita kuwa tumekumegea mkeo kwa kutumia hela za mfadhili wetu Lowassa. Wanaume wengine bana, utafikiri wanavaa SHIMIZI.
 
Kanda2,

kampeni za namna hiyo hapana, hata kama ni Afrika.

Hatuendi kudanganya watu, tunaenda kufanya yale tunayoyaamini. Hata kama una uwezo wa kutoa laptops 40, bado ungetakiwa kujadiliana na mimi kwanza kabla ya kusema mimi nimetangaza kwamba nitatoa hizo laptops.

Sijui ya mungu, hata mimi naweza kutafuta hizo laptops lakini kwasasa sio priority na kuna mambo mengine ambayo ni muhimu zaidi.

kwa kusema mimi nimeahidi kutoa laptops bila mimi mwenyewe kusema hivyo, tayari watu wengi walishaamini mimi ni mwongo ninaposema siahidi kitu.

Ni bora umethibitisha mwenyewe kwamba mimi sikuahidi mahali popote kutoa laptops na hata sasa siahidi hilo.

Siku hizi kuna idea mpya ambayo ni bora inaitwa no pc. Ni bora hiyo kuliko hata laptops.

Pole sana kwa kufungiwa japo sijui ulifungiwa kwasababu zipi. Kuna wengi walinitetea na mbona hawakufungiwa?

wapi nilisema wewe umesema utatoa LAPTOP? niliyesema ni mimi.kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM 2005 HAKUNA kipengele cha chuo kikuu cha Dodoma ni JK aliamua kulisema yeye kama binafsi kwa vile ni jambo jema CCM ikalichukua na kulifanyia kazi.

sasa kama huhitaji Laptop mbona unalalamika kukosa vitabu vya BOOKAID INTERNATIONAL?hawa waliona WAMA wamejikita kwenye utaifa na wewe umekijikita kwenye Ukyela,wakaona uzito uko Wama.

Unasema wewe hutoi ahadi ila unatekeleza.utachaguliwa vipi bila kueleza kuwa nia yako ya kuwa mbunge ni kuwafanyia hili na lile wana Kyela?huwezi kukopi siasa za Ulaya ukapeleka Kyela.kama unasema huwezi kufanya siasa za Africa mbona unamjibu KUBENEA ambaye yuko kazini kisiasa kukuchafua wewe.ungenyamaza na kusema watu wa KYELA wakupime na utekelezaji wako.
 
Ogah,
Nafahamu umeolea Kyela/Mbeya kwa Wanyakyusa. Kama unafikiri mie ni wa huko basi umenowa. Ni hili tu litakuokowa kwa leo. Ngoja nirudie tena. Mie ninaitwa Sizya kimila au Mwanangwa (adopted mtoto wa Mtemi) wa Sikonge yaani Lugusha Family wa pale Sikonge kwenye kona ya barabara inayokwenda Kisanga Village ikiwa karibu na kanisa la RC la Sikonge. Kyela hata sijawahi kufika kwa hiyo usinifanishe na hao watani zangu. Mie ni NGOSHA wa kikwelikweli.

Mkuu Sikonge,

...heshima mbele, sijawahi na sitajaribu kutaka kujua wewe unatokea wapi...na wala sihitaji kujua....huo utambulisho wako.......kwani haipo katika sehemu ya utashi wangu.....kutafuta kujua/ku-speculate nani ni nani na anatokea wapi.............

Unachokisema wewe kinafaa kwenye nchi zilizoendelea. Huwezi kujifanya unatumia SHERIA kwenye nchi yenye asilimia 70 mifuata upepo. Ingelikuwa nchi za kawaida, watu kama Chenge, Lowassa, Mramba, Liyumba, Mkapa, na wengine wengi au wangelikuwa jela au wasingelikuwa wamefikia kwenye POST kubwa kiasi kile bila kuwa wamezuiliwa.

Kiongozi pekee atakayefanikiwa Tanzania/Africa ni yule atakuja na kuanza kutembeza UBABE wa hali ya juu huku akiwa na mapenzi makubwa kwa nchi yake. Watanzania ni wachapa kazi si kawaida. Watz wanaipenda sana nchi yao, wanasoma sana, wangelipenda sana kuona maisha yao yanabadilika. Ndiyo maana Kikwete alipowapa maneno wanayoyataka, walimchagua kwa kishindo wakijua atasafisha PUMBA zote za MKAPA. Walikuwa tayari hata kuletewa sheria za kijeshi ili muradi UCHUMI WETU uanze kukimbia kwenda mbele. Hata mie nilikuwa naamini kuwa "cha moto tutakiona ila tutasonga mbele". Nimechoka kushabikia wenzetu kwenye michezo, kuangalia Wakenya wakitufunga magoli, kuangalia ndege za wetu bila kuona Twiga akitua ............................

Ili haya yaje, inabidi KICHAA kama Putin aje ABADILI akili za tu. Kubadili akili za watu ni au utengeneze KIZAZI kipya (hamna muda) au kuleta sheria za China. Wewe unachagua lipi? Unategema watu wanaomwambia Rais aje afungue DARAJA wakati bado halijaisha, ni watu wa KUCHEKEA HAO? Mrisho Mpoto anaimba "Ukicheka na nyani mjomba, utavua MABUA". Dawa si KUCHEKA na nyani ili uvune mahindi. Nashindwa kuelewa hata Mpoto analielewa hilo na Ogah bado hujaliona. Anyway, usihofu kwani sina mpango wa kugombea kwenye SIASA kwa siku za karibuni na mwaka 2012 ni mwisho wa dunia.

...........fair enough!...............you are entitled to your own opinion.......
 
Mkuu Sikonge,

...heshima mbele, sijawahi na sitajaribu kutaka kujua wewe unatokea wapi...na wala sihitaji kujua....huo utambulisho wako.......kwani haipo katika sehemu ya utashi wangu.....kutafuta kujua/ku-speculate nani ni nani na anatokea wapi.............

...........fair enough!...............you are entitled to your own opinion.......

Kumbe unatishwa NYAU? Nilitaka kuwa na uhakika unavyojibu ujumbe wangu kiutaniutani, unafikiria pia mie ni wa Kyela? Ndiyo maana nikataka kuweka rekodi sawa. Kufahamu mtu anatoka wapi haina maana umemfahamu.

Tuke pamoja mkuu wangu. Wote lengo letu ni moja labda tu kila mtu ana maono ya njia tofauti za kutumia. Zangu kidogo ni Radical na wengine zenu ni soft. Ingawa kusema ukweli, ili mambo yaende inabidi zote zitumike yaani kama ni POLISI, basi kuwe na POLISI mbaya (mimi) na POLISI mzuri(wewe).

NB: Jumbe mbili za mwanzo kwako nazifuta. Ntafurahi ukifuta kuanzia ule wako wa kwanza kama kweli unaamini "i'm entitled to my own opinion".

*** Wee nyanda Samwel, nenda kalale :) Utapewa talaka bure. Kesho nakulima waya kwenye mtandao(Skype).
 
Pole sana kanda2. Niliowataja ni wale ambao nafahamiana nao kwenye real life na niliongea nao nilipokuwa Tanzania na wakasaidia kufikisha ujumbe wangu JF.

Kuna wengi walinitetea na nawashukuru sana. Ila Kanda2 si ni wewe uliyesema nimeahidi kutoa laptops shule zote Kyela? Sijawahi kusema kitu kama hicho mahali popote au kwa mtu yeyote. Je ulitoa wapi maneno kama hayo? Kama sio wewe basi samahani sana. Kuna watu wengi tu waliamini mimi nimesema kitu kama hicho hasa kwa wale ambao hawanifahamu. Mimi siahidi jambo lolote na kama kuna kitu nataka kutoa basi natoa kwanza kabla ya ya kuwaambia wananchi. Kule vijijini ukiahidi kitu watu wanategemea utekeleze. Mimi sina uwezo wa kutoa laptops kila shule na kama ningesema hivyo ungelikuwa usanii tu ambao mimi mwenyewe naupinga hapa kila siku.

Kuna wakati nilitaka kuomba shirika fulani huku lisaidie vitabu kule Kyela. Wakanipatia forms zao ambazo ilikuwa ziwekwe sahahi na walimu wa shule husika (shule tano). Na kweli kule Kyela walimu wakasaini na kuzirudisha. Bahati mbaya huo msaada wa vitabu ukaunganishwa pamoja na maombi mengine na kukabidhiwa WAMA ambao nao wakavipeleka kule walikotaka wao. Kule Kyela ikawa kasheshe, pamoja na kuwaambia mwanzoni kwamba tunajaribu na chance ya kupata ni kama 10%, wao waliamini hivyo vitabu vimepatikana. Baada ya muda yakaanza maneno ya chini chini kwamba nimewatapeli. Ikabidi nitoe pesa yangu mfukoni na kuwanunulia vitabu hapo Dar. Hapo ndio maneno yakaisha ila nikawa nimejifunza kwamba huko nyumbani watu wanafikiri kila mtu ni mwizi na kwamba kila ukiomba kitu nje utapewa. Usiahidi kitu hata siku moja maana utawapa matumaini watu bure wakati huenda usifanikishe. Fanya kila kitu kimya kimya na kikiwa tayari ndio waambie.

Hata halmashauri ya wilaya walishawahi kusaini barua yetu fulani ya kuomba msaada fulani ambao kwa leo sitautaja. Baada ya muda wakaanza kusema kumbe nao akina Mwakalinga ni wasanii. Barua zote kutoka chombo cha serikali kilichokuwa kinashughulikia usajili wao walikuwa wanapewa copy lakini bado hawakuamini. Siku tumefanikisha, watu waliona aibu kama nini. Mkuu mmoja ndio akasema wazi kwamba hata yeye alishaanza kuamini na sisi ni wasanii lakini sasa tumemuumbua hata yeye na ni jambo zuri kwetu maana wale wote waliokuwa wanasambaza hayo maneno sasa ndio wanaona aibu kubwa.

Ku deal na watu wa wilayani ni ngumu sana, inatakiwa elimu kubwa ili waelewe na waunge mkono juhudi za kusaidiana nao kujiletea maendeleo yao. Hata michango wanayotoa inatakiwa kuwe na uwazi mkubwa mno ili kila mtu aone kila senti imeenda wapi, vinginevyo watalia ufisadi hata pale ambapo hakuna ufisadi.
mkuu unajichanganya umesema hapo juu kuwa huna uwezo wa kupata Laptop halafu leo umetuma ujumbe mwingine ukisema unao uwezo wa kupata hizo Laptop lakini sio priority kwako.

kingine unaposema wewe huwa hutoa ahadi jee hutakuwa na Manifesto kwenye kampeni zako?

Sijawahi kuona siasa ambazo hazina AHADI iwe America,ulaya au Africa. Kama ajira OBAMA aliahidi kuzalisha ajira,na JK naye aliahidi hivyo hivyo. Ameanza kwa kufungua chuo kikuu cha DODOMA na miradi mingine. Mtu hupimwa kwa ahadi zake. Huwezi kufanya siasa za kufikirika.

Gordon Brown na David Cameroun wanatoa ahadi kila siku ambazo zingine hazitekelezeki ingawa wako ulaya ndio siasa. Kwa mtindo wako huo sidhani kama ubunge ni mahala pako lazima ubadilike.

Niambie mbunge gani mkweli kuanzia vyama vya upinzani hadi tawala? Wewe utakuwa malaika? Mfano utaenda kwa waziri wa miundombinu atakwambia kuwa barabara ya kyela itajengwa kwenye bajeti ya 2010/2011 wewe kama mbunge ukitoka hapo utaenda kuwaeleza wananchi wako kuwa barabara hiyo itajengwa muda ujao. Halafu wizara ghafla inabadilisha ratiba hiyo, hayo yanatokea sana.
 
Mwakalinga has taken out his veil and announced that he is our JF'S Mtanzania!! Mwakyembe inasemekana yeye anaingia humu JF kwa majina mengi tu lakini si la Mwakyembe; will he be courageous enough like his nemesis to announce his true identity hapa ukumbini? hiyo itatusaidia kujua kama ninani anaetoa hoja badala ya sasa ambapo wahusika ndio wanaoandika nasi tunadhani ni wapambe wao!! Mtu yeyote anaeandikaka kitu anachokiamini na si majungu hawezi kujificha kwa kutumia majina bandia; mbona sisi wengi tunatumia majina yetu humu janvini!!
Pole sana, yaani kwa kusema mie ni Mwakalinga basi kwako amekuwa Mwakalinga kweli?...Wewe kutapeliwa ni sekunde tu...!
 
FMES,

Kwenye hiyo habari Kubenea ana mengi tu ya kujibu. Inaelekea hata huyo Matai wanayesema alisema anajua kuwa ni kweli kwamba Mwakalinga alikuwa anatoa pesa mpaka laki moja anakataa, anasema hajawahi kuongea na mwandishi yeyote wa Mwanahalisi. Kwasasa hili tuliacha na ukweli utajulikana tu muda sio mrefu.

Hata hilo suala la kwamba Mwakipesile anashinda Kyela. Kwa taarifa nilizo nazo mimi na labda watu wa Kyela wanaweza wakathibitisha, familia ya Mwakipesile iko Kyela, hajahama kwenda nayo Mbeya. Mwakipesile anaondoka Jumatatu asubuhi kwenda Mbeya na anarudi Ijumaa usiku kurudi Kyela kwenye familia yake. Huko ni kushinda Kyela? Labda, lakini kwa maoni yangu sidhani kama huko ni kushinda Kyela. Kutoka Kyela mjini mpaka Mbeya mjini ni kama km 110. Huyu mtu angeweza hata kila siku kulala Kyela na kufanya kazi Mbeya.

Hilo la Dr. Hunter, huko nyuma jina lake liliwahi kutolewa kwa madai hayo hayo lakini CCM mkoa likarudishwa baada ya kuridhika na maelezo yake kwamba huo ndio umri wake na wao kufuatilia documents zilizokuwepo. Nafikiri kwa mwandishi wa habari angeweza kuchunguza zaidi na kuja na ushahidi kuonyesha huyo kijana kadanganya umri au la.

Mtafuteni aje atoe msimamo wake na kama amekosea awe tayari kuomba msamaha kwenye gazeti lake la wiki kesho.
Mhh...wewe ni Mwakalinga? Si ungesema mimi badala ya Mwakalinga? anyways, i might be wrong though...ila i wonder...!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom