Kubenea amlalamikia Manji

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205
KubeneaSaed.jpg



Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, Saed Kubenea(Picha, na Maktaba)




Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, Saed Kubenea, amewasilisha malalamiko kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akimuomba kuingilia kati mwenendo wa kesi iliyoamuliwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke dhidi yake, kwa kusikiliza upande mmoja tu wa mfanyabiashara, Yusufu Manji.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Manji dhidi ya Kubenea, Mhariri wa MwanaHALISI, Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers Limited na Printech Company Limited, Julai 18, mwaka huu.
Kubenea amewasilisha malalamiko hayo kwa niaba ya wadaiwa wenzake kupitia barua yake kumbukumbu namba. HHPL/ADM/1101 ya Julai 25, mwaka huu, yenye kichwa cha habari: “Malalamiko dhidi ya kesi ya madai Na. 43/2011”.
Anadai Manji aliiomba mahakama itoe amri kwa kusikiliza upande wake mmoja tu na mahakama ilifanya hivyo na kuamuru.
Amri hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Rose Kangwa, Julai 19, mwaka huu, inawataka kuwasilisha kwa Manji hati ya viapo vyao, nyaraka zote za asili na vivuli, walizonazo zinazohusu taarifa anayolalamikia katika gazeti la MwanaHALISI, toleo namba. 250 la Julai 13-19, mwaka huu na kueleza walikozipata.
Kubenea anadai pamoja na kuwasilisha hati ya madai ya msingi siku hiyo, Manji alifungua pia maombi ya zuio siku hiyo hiyo. Anasema si kawaida maombi ya zuio la dharura kusikilizwa kwa njia hiyo kama alivyofanya hakimu huyo.
Anadai hati ya madai na amri ya zuio ya mahakama, vilipelekwa ofisini kwake Dar es Salaam siku hiyo hiyo ya Julai 19, akiwa Dodoma kusaka habari za Bunge linaloendelea hivi sasa.
“Wakati huo, mimi binafsi, ofisi yangu na hata wadaiwa wengine hatukuwa na taarifa zozote za kuitwa shaurini. Tunatishika kwa hatua ya Hakimu wa Mahakama Temeke kupanga na kukubali kusikiliza maombi ya mdai haraka kiasi hicho bila kutaka tujulishwe, bila kutaka tuhudhurie na bila kutaka tusikilizwe,” anasema.
Anasema ofisi yake na za wadaiwa wenzake ziko Dar es Salaam na zinafikika na kwamba, urahisi wa kuzifikia umedhihirika kwa jinsi Manji alivyofaulu kufikisha kwao ‘mara moja’ amri ya mahakama.
Kwa kuzingatia hayo, anasema walinyimwa haki ya kusikilizwa na utaratibu uliotumika una sura ya kinyemela.
Anasema kwa hayo yanayotokana na matakwa ya Manji na yaliyokubaliwa na mahakama hiyo bila kuwapo kwake, wakili wake wala wadaiwa wenzake, ni wazi kuwa wananyang’anywa haki ya kujibu na kutishiwa bila kusikilizwa.
Pia wanaonyeshwa kana kwamba kumekuwa na kesi na sasa imeisha, hivyo wanapewa masharti na mahakama, wanashinikizwa kufichua vyanzo vya habari vya gazeti kwa maslahi binafsi, kabla kesi haijasikilizwa na mahakama kuamua iwapo kuna sababu ya kufanya hivyo “kwa maslahi ya umma.”
“Mimi binafsi na wadaiwa wenzangu, tuna imani na mahakama. Kwa msingi huo, ninakusihi uingilie kati mapema iwezekanavyo, mwenendo wa kesi husika, kwa kuitisha jalada la kesi yenyewe ili ulipitie na kulifanyia maamuzi,” anasema.





SOURCE: NIPASHE
 
ni huyu kubenea anayehariri gazeti la mwanahalisi linalo milikiwa na Anthony komu mkurugenzi wa fedha wa cdm
 
[B said:
woyowoyo[/B];2305310]ni huyu kubenea anayehariri gazeti la mwanahalisi linalo milikiwa na Anthony komu mkurugenzi wa fedha wa cdm

CUF nyie hamna gazeti lenu???
 
Ndugu wakati mwingine huwa na doubt sana uhuru na uwajibikaji wa mahakama katika kesi ambazo zinahusisha matajili,
 
kubenea sasa tajifunza kuandika kwa chuki!!!! aislalmike apambane kama mwanaume wa shoka. wengi wamemvumilia sasa analilia nini????? he knew what he was doing and got exactly what he was looking for!
 
Nguvu ya fedha. Wanasema wakoloni wote waliondoka, akabaki mmoja naitwa Fedha! Sasa tunayaona.
 
Mahakama na mahakimu wanatakiwa kukwepa tanzi la kapu la mijihela ili kulinda hadhi na heshma ya mahakama kama kimbilio pekee na mtetezi wa wanaoonewa.
 
ninavyomjua kubenea hawezi kureveal source zake hata wakilifungia gazeti,..hell..they did it before...mkwara tu huo wanajua jinsi mwanahalisi linavyokubalika kwa wananchi...
 
Ndugu wakati mwingine huwa na doubt sana uhuru na uwajibikaji wa mahakama katika kesi ambazo zinahusisha matajili,

Halafu tukijadili madudu yao tunaambiwa tunaingilia uhuru wa mahakama, uhuru gani? Nilishangaa sana mahakama ilipoukataa ushahidi wa nyaraka zinazomhusisha Manji na wizi wa Kagoda. Hata hivyo hata mamlaka inayowateua nayo haiko huru.
 
Halafu tukijadili madudu yao tunaambiwa tunaingilia uhuru wa mahakama, uhuru gani? Nilishangaa sana mahakama ilipoukataa ushahidi wa nyaraka zinazomhusisha Manji na wizi wa Kagoda. Hata hivyo hata mamlaka inayowateua nayo haiko huru.

UHURU wa Mahakama za Tanzania ni UTUMWA wa Mtanzania
 
Kwanza, huyu kilaza aache kupiga porojo kwamba MwanaHALISI gazeti la Anthony Komu. Wewe hufahamu historia, badala yake unasikiliza maneno ya ZITTO. Hili ni gazeti la KUBENEA ambaye anamiliki 90 ya hisa.

Pili, KUbenea nimeambiwa ana nyaraka za wizi ambao Manji, Mkapa, Dk. Dau, Bugoya, Gavana Balalli na Mama Anna Mkapa wamefanya. Kuogopa Manji kuumbuka ameamua kuitumia mahakama kumfunga mdomo Kubenea.

Tayari naambiwa Manji amefungua kesi nyingine mbili katika mahakama ya Kinondoni na Mrorogoro. Zote zinahusu maoni ya mtu jinsi klabu ya Yanga iliyokuwa inafadhiriwa na Manji ilivyoingia katika mgogoro miaka 2 iliyopita. Ni ujinga mtupu.

Ninachokijua Kubenea hatakubali. Ameapa kufa na Manji. Anajiaanda kutupa kombora.
 
There are currently 8 users browsing this thread. (1 members and 7 guests)
Ngoja nisepe Fasta... Wageni saba na mimi wa 8... Ubnadaam kaaazi bora nifadhili Mbuuuz nitamla Mchuzzzz...
 
kubenea haki haipotei hivi hivi kaza mwendo Mungu atakufungulia neema kwakila ufanyalo zidi kutuelimisha acahana na wachawi wa nchi hii ambao hawatutakii mema hata siku moja
 
Tunaamini unayoandika bwana Kubenea na pigania haki ukweli utajulikana juu ya hao wezi wa nchi yetu,Mungu atakuongoza
 
Back
Top Bottom