Kubenea afanyiwa tena upasuaji wa macho India

Njele

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
275
121
ku%2B2.jpg

Mhariri Mtendaji wa magazeti ya MwanaHALISI na Mseto, Saed Kubenea akichukuliwa vipimo na mmoja wa wahudumu wa hospitali ya Apollo nchini India kabla ya kupelekwa kwenye chumba cha upasuaji . Kubenea yuko nchini India kwa matibabu ya macho yalitotokana na kumwagiwa tindikali. Tayari amefanya upasuaji huo jana.
 
ku%2B1.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Hali halisi publishers Ltd, Saed Kubenea akiwa katika wodi ya Hospitali ya Apollo, New Delhinchi INDIA mara baada ya kufanyiwa Upasuaji macho jana.Kubenea amekuwa akitibiwa katika Hospitali hiyo tokea mwaka 2008 alipomwagiwa tindikali katika ofisi yake jijini Dar es Salaam na hii ni operesheni yake ya tano.
 
What happen? Ametiliwa mara nyingine au ni kutokana na ile aliyomwagiwa hapo awali?
 
Tangu amwagiwe tindikali kwa sababu ambazo hadi leo hazijulikani kutokana na kujitokeza madai mbali mbali kuanzia ugoni hadi uanaharakai, Mwandishi Saidi Kubenea amekuwa akienda India kila mara kutibiwa kwa gharama za serikali. Je hii ni takrima, wajibu au kukwepa lawama? Je ni wangapi wanaumia kazini na serikali haiwapi upendeleo kama huu isitoshe kwa mtu ambaye si mtumishi wake? Kunani nyuma ya pazia jamani?
 
Yaani hawa CCM hawa! Pole ndugu yangu Kubenea Mungu atakupigania na utarudi kwenye hali ya awali
 
Hivi hawa viongozi wetu wa nchi kwa nini wasiwashawishi wamiliki wahospitali kama hii ya Apollo waje nchini wawekeze katika huduma hii tuepuke na gharama za kusafirisha watendaji wa serikali?
 
Tangu amwagiwe tindikali kwa sababu ambazo hadi leo hazijulikani kutokana na kujitokeza madai mbali mbali kuanzia ugoni hadi uanaharakai, Mwandishi Saidi Kubenea amekuwa akienda India kila mara kutibiwa kwa gharama za serikali. Je hii ni takrima, wajibu au kukwepa lawama? Je ni wangapi wanaumia kazini na serikali haiwapi upendeleo kama huu isitoshe kwa mtu ambaye si mtumishi wake? Kunani nyuma ya pazia jamani?
Una uhakika mkuu? Alipokuwa Appolo mara ya kwanza tunaambiwa alilipiwa mwanzoni then wakamtelekeza! Kama hata this tym amelipiwa hebu thibitisha walau kwa nukuu ya any reliable source!
 
Kubenea anasemwa sana now days! Nafikiri ni wakati Kubenea aanze kujibu hizi hoja maana zinaanza kuaminiwa!
 
Tunakuombea kheri mpiganaji Said Kubenea, Mungu ni mwaminifu atakurudisha salama. Ugua pole
 
Kumbe hospitali ni appolo peke yake au inamilikiwa na mtanzania manake kila mtu ni huko
 
Back
Top Bottom