Kubana matumizi Serikalini vs shilingi kutoimarika

clasi

JF-Expert Member
May 5, 2013
378
683
Awamu ya 5 imejipambanua kwa kubana matumizi na kuzuia safari za nje ya nchi kwa watumishi wa serikali (umma) kwa mawazo yangu nilifikiri kuwa Tsh. itaimarika dhidi ya USD kutokana na serikali kutumia pesa mingi kwenye safari hizo za watumishi wa umma nje ya nchi (ununuzi wa tikiti za ndege, Per Diem (foreign)). Kwa mshangao bado Tsh. ni dhaifu (nyanya) mbele ya mbabe USD wachumi naomba msaada kwa hili.
 

Attachments

  • dolashilingi.jpg
    dolashilingi.jpg
    30.1 KB · Views: 127
Eti Taasisi ya ROHO? duuh wabongo siwawezi kwa kweli. Mkulu apunguze kazi maana wakubwa wanahamisha pesa kwenda nje tukifanya masikhara tutayumba. Akiweza ku-control MANUNUZI YA UMMA kazi nyingi za ujenzi, fenicha wakapewa SUMA JKT, Magereza, tukanunua magari ya Mtumba (Second hand pale BE FORWARD) lazima uchumi utulie.
 
Nashangaa pamoja na viongozi hawasafiri ila bado dollar iko juuu au importation zimeongezeka
 
serikali inabana matumizi hadi kwa kupunguza wafanyakazi wa umma na mashirika binafsi kama ilivyofanya kwa clearing agencies..
ambayo nayo yamelazimika kutimua,
ili mtaani kuwepo na kundi kubwa la vibaka na majangili..
abiria chunga mzigo wako..
 
Mambo haya yanahitaji uangalifu na utalaamu mkubwa sana wa KIUCHUMI, wanasayansi wabaki maabara wakichanganya kemikali tu na kuibuka na milipuko. Sasa tukikalia sijui #TUMBUA TUMBUA# watu badala ya kufanya kazi wanaishia kuruka ruka kama POPCORN kwenye kikaango.
 
kubana matumizi hakuhusian direct na kuimarisha shilingi, shilingi itaimarika significantly endapo tutafanya export nyingi na tujipunguza consumption ya imported goods
hiyo ya serikali kukadhibiti safari za nje inasaidia kupunguza demand ya dollar ila kwa kiasi kidogo sana kiasi kwamba huwezi ukaona impact
 
Wahindi wamekimbiza mitaji yao na hawaagizi tena wala kusafirisha korosho nje. Wamebaki wachina na uingizaji wa yeboyebo kwa ku-export chupa za maji. Jumlisha na EU na Marekani kwenye MCC kujitoa kuwapa kichele. Mbona Kafulila aliwaambia mkamkebehi? Tutaisoma namba wote kwa Tanzania ya viwanda tuliyoahidiwa kwenye kampeni. Natamani tuwe Zimbabwe the 2nd
 
Nafikili mpaka hapo badae kwasababu now kuna mipango ya kupunguza mabenki yaliyo zagaa hovyo ili kuimarisha shilingi yetu
 
Ungetoa yakwimu kwamba baada ya kubana matumizi ni kiasi gani cha pesa kimehifadhiwa ili tuone kama hicho kiasi kilichobanwa ni significant kuweza kuathiri uchumi mzima na pesa yetu. Hata na hivo kubana matumizi kuna mchango mdogo sana kuweza kupandisha thamani ya pesa ya nchi. Na inawezekana isiwe njia ambayo inatumika na nchi nyingi duniani.

Unapoongelea suala la kubana matumizi husianisha na nakisi ya bajeti ambayo inaathiri deni la taifa. Mfano naweza kukuambia kwamba kwa hatua hizi za magufuli tutegemee kwa haraka haraka ukuaji mdogo sana wa deni la taifa ambapo in the long run hatutakuwa na liability kubwa hivo kuondoa pressure ya kushuka thamani kwa shilingi yetu dhidi ya fedha za kigeni.

So napingana na wewe kuhusu kuwa na matokeo ya haraka haraka ya kubana matumizi na kupanda kwa thamani ya shilingi yetu kwa mda huu mfupi ila at the same time naungana na wewe kwamba in the long run shilingi ina uwezekano wa kuimarika kwa hatua ambazo ataendelea kuzichukua magufuli.
 
kubana matumizi hakuhusian direct na kuimarisha shilingi, shilingi itaimarika significantly endapo tutafanya export nyingi na tujipunguza consumption ya imported goods
hiyo ya serikali kukadhibiti safari za nje inasaidia kupunguza demand ya dollar ila kwa kiasi kidogo sana kiasi kwamba huwezi ukaona impact

Kwa kifupi ili shillingi yetu iimalike tunahitaji kuwa na fedha ya kigeni ya kutosha nchini [ FOREX]; sasa hiyo forex inaweza kuongezeka kwa kuuza bidhaa nyingi nchi za nje; kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa kutumia fedha ya kigeni kama vile kuthibiti safari za watumishi wa umma; kuwahamasisha wananchi watumie bidhaa za ndani ya nchi. Pamoja na yote hayo kuna umuhimu wa kuweka sera ambazo zitavutia watu wa nje waweze kuleta fedha zao nchini mwetu. Kuna ushindani mkubwa sana wa kuvutia watu wa nje kuleta fedha zao nchini kwetu hasa wakati huu ambapo marekani wameongeza interest rate !!!
 
Kwa kifupi ili shillingi yetu iimalike tunahitaji kuwa na fedha ya kigeni ya kutosha nchini [ FOREX]; sasa hiyo forex inaweza kuongezeka kwa kuuza bidhaa nyingi nchi za nje; kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa kutumia fedha ya kigeni kama vile kuthibiti safari za watumishi wa umma; kuwahamasisha wananchi watumie bidhaa za ndani ya nchi. Pamoja na yote hayo kuna umuhimu wa kuweka sera ambazo zitavutia watu wa nje waweze kuleta fedha zao nchini mwetu. Kuna ushindani mkubwa sana wa kuvutia watu wa nje kuleta fedha zao nchini kwetu hasa wakati huu ambapo marekani wameongeza interest rate !!!

Utawavutia vp wawekezaji kutoka nje wakati hata wajumbe wenyewe unawakaribisha kama wanafunzi mstarini, wawekezaji wengi kwa sasa wanafunga ofisi zao, na wanahamia nchi zingine wanazoona zinasera nzuri za uwekezaji.JK alizunguuka dunia nzima kuitanga tz ingawa analaumiwa kua safari zake nyingi ni za anasa. Bado tunahitaji Msaada kutoka ng'ambo, tz ilikua haijulkani baadhi ya nchi nyingi huko, hadi uwaambie nimetokea kwenye nchi yenye mlima Kilimanjaro. leo wakisema HATUTAKI BIDHAA ZENU,NA BIDHAA ZETU HATUWAPI. Baada ya mwezi tu tutaanza kuilamu serkali,na kama mnakumbuka wakate EAC inaanziasha wenzetu walitupa ofa kwa bidhaa zetu, tukiweza kupeleka kwa wanatupunguzia kodi kuliko wao kuleta kwetu. Hakika kwa jinsi wanavyobana hali utakua ngumu sana kwa mwananchi wa kawaida, lakini labda wana malengo mazuri, maana unaweza kubana kwa wananchi huduma za kijamii zikawa nzuri, unaweza kubana kwa wanaoishi mijini ukaachia wa vijijini (million 50,50) ili wasio na kazi mijini waludi vijijin wakalime.PIA KWA UBANAJI HUU INGUKUA KWA NCHI ZA KIJAMAA NI SAWA LAKINI KWA NCHI ZA KIBEPARI TUJIANDAE KWA MAUMIVU TU.
 
Vjana wengi toka Tanzania wapo USA, UK, The Netherlands, Kenya, Botswana, Namibia, Swaziland na Afrika Kusini huko ni watu wenye kazi nzuri na wanaingiza pesa nyingi sana hawa waundiwe WIZARA yao MAALUMU mfano; WIZARA YA DIASPORA na waziri mwana-diaspora ndo aongoze. Ili kuwavutia hao matajiri diaspora huko ughaibuni kurudisha pesa nyumbani.
 
Kama nilivyosema hapo awali ili kuimalisha shilingi yetu kuna hili la kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kwa bidhaa ambazo tunazizalisha humu nchini; hili linaweza kusaidiwa na elimu kwa wananchi hasa wale wa kipato cha kati lakini pia kwa sera za makusudi za serikali kuvilinda viwanda vinavyozalisha bidhaa kama hizo kutoka bidhaa kutoka nchi za nje.

Serikali imeonesha nia ya kuvifufua viwanda kama njia ya kuongeza ajira kwa wananchi lakini pia kuondoa utegemezi wa bidhaa toka nje ambazo zinahitaji fedha za kigeni kuzileta; hivyo basi kuna kila sababu ya kuvilinda viwanda hivi kwa sera mathubuti inayoeleweka. Hakuna sababu ya kuruhusu saruji kutoka Pakistani wakati saruji hiyo hiyo inazalishwa hapa nchini ambamo viwanda vinatoa ajira na kuipatia serikali mapato kwa kulipa kodi!! Selective protectionsm is practised all over the world hivyo serikali isiogope kutekeleza sera hizo kwa maslahi ya nchi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom