Kuanzishwa kwa CDM TV na ku-update Website ya CDM

Ishina

Senior Member
Dec 27, 2011
169
57
CDM TV:
Kuanzishwa wa CDM TV ni jambo ambalo linapigiwa debe na wana-CDM wengi, jambo hili sio jipya na limeshazungumziwa sana hapa kwenye JF na wana-CDM na wote wenye mapenzi mema na CDM kwa muda mrefu saana. Hapa, mimi ni katika kuwakumbusha tu viongozi wangu wa CDM kuwa tupenda watufahamishe kuwa mpango wa kuazishwa kwa TV yetu ukoje?! Mpango wa kuazisha TV utaanza lini na utakamilika lini?! (kama limeshajibiwa hapa kipindi cha nyuma, basi naomba na mimi kama mwana-CDM niweze kujua).
​
Mimi kama mmoja wapo watu wanao-support M4C, na ili hii movement iweze kufanikiwa kikamilifu, na tuweze kuchukua nchi 2015, lazima sehemu kubwa ya Wa-TZ waweze kufikiwa na kuelimishwa, na njia mmojawapo na muafaka ni kupitia TV, Radio, na mitandao ya internet. Je wana-CDM tunategemea kufika kila pembe ya nchi kwa kutegemea tu mikutano ya majukwaani, pamoja na TBC, Clouds fm, ITV etc.??!!

Suala la Website ya CDM
Hapa napo kuna tatizo, inabidi watu wa Kitengo husika wawe wepesi ku-update website yetu. Kwa kipindi hiki cha kampeni huko Arumeru, kuna mambo mengi saana ya kuyatolea taarifa, naamini website ya CDM ingekuwa ni mmojawapo wa njia muhimu saana, za kutolea taarifa za kinachoendelea Arumeru na sehemu zingine ambazo CDM inashiriki kwenye uchaguzi, na mambo mengine kwa ujumla yanayohusu CDM.

Pia, hata matamko, ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayohusu CDM, ni vyema pia, yakawepo kwanza kwenye website ya chama, na baadae kwenye mitandao ya internet (e.g JF). Hivi karibuni imekuwa ni kama utaratibu CDM kutolea ufafanuzi wa mambo yanayohusu chama hapa JF (hata kama jambo hilo halija-originate hapa JF). Sipingi kutumia mitandao kama sehemu mojawapo kuwafikia wa-TZ wengi, lakini nashauri kuwa tuwe tunaweka na kwenye website yetu, then nakala tunaweza kupeleka kwenye vyombo vingine vya habari ikiwa ni pamoja mitandao ya internet. Kitengo cha habari cha CDM naomba mtoke usingizini na muwe mna-update website kwa taarifa mbalimbali zinazohusu chama chetu.

Ni hayo,

Pipooooo, Pawaaaaa

Ishina.
 
Suala la TV kwa cdm limeongelewa kirefu sana na members mbalimbali, hata viongozi wakuu wameshaona threads hizo, na kwa nyakati tofauti wamejibu wakionyesha taratibu na hatua za kufikia jambo hilo!
 
Suala la TV kwa cdm limeongelewa kirefu sana na members mbalimbali, hata viongozi wakuu wameshaona threads hizo, na kwa nyakati tofauti wamejibu wakionyesha taratibu na hatua za kufikia jambo hilo!

Nafahamu kuwa hili jambo limeongelewa saana hapa, lakini haina maana kuwa wengine ambao hatujui status ya jambo hilo hatustahili kuliongea . Ungefanya jambo la maana saana ungenipa status tu ya jambo lenyewe limefikia wap mpaka sasa. Hizo thread za nyuma mimi sijaziona (usiniambie nianze kuzitafuta).
 
Mwenye clues kuanzisha TV unitaji ela kiasi gani!
Maana hawa magamba na TV zao wanabana sana
 
Mwenye clues kuanzisha TV unitaji ela kiasi gani!
Maana hawa magamba na TV zao wanabana sana

Tuanzishe kamati maalumu ya kuanzisha TV ya Demokrasia na Maendeleo. Itakayokuwa huru, bila kujali itkadi. Iwe chachu ya maendeleo.
 
Tuanzishe kamati maalumu ya kuanzisha TV ya Demokrasia na Maendeleo. Itakayokuwa huru, bila kujali itkadi. Iwe chachu ya maendeleo.

Hili swala mimi naliongelea kila siku. Na nitaendela kusema.

CHADEMA kama wanamikakati ya kweli kuchukua nchi wanapaswa kuwa na TV yao...

Sio watu wote ambao wanaweza kuingia humu Jamii forum ili kujua habari za CHADEMA. Au kuingia kwenye website ya CHADEMA kusoma update.. Au kuhudhuria kampeni na mikutano ya CHADEMA... Asilimia ya kubwa ya wananchi mtawapata kwenye TV.

Nakumbuka 2010 dr. SLaa alipata umaarufu mara dufu. Kwenye ile coverage ya mdaharo.. Kuliko hata kampeni ambazo tulikua tunazisoma kwenye magazeti au kusikia kwenye ma_radio.

Mimi nawasihi, muachane na ule mpango wenu wa kujenga chuo. Ni bora hiyo hela muanzishe TV... Itawasaidia kutoa elimu kiurahisi. Kuliko kutumia nguvu nyingi katika maandamano au mikutano ya hadhara. Ambayo mwisho wa siku vyombo vya habari havitaki kurusha habari za mikutano yenu.
 
vyombo vya habari ndivyo vyenye kuweza kuleta mabadiliko mahali popote pale duniani ,hata wanajeshi wakipindua serikali cha kwanza wanakimbilia ktk tv na redio kwanini wasikimbilie mitaani na kuanza kutoa taarifa? hapo utaona umuhimu wa vyombo hivyo tv na redio kwani habari husambaa kwa haraka zaidi tofauti na magazeti
 
arumeru na kata nane kwanza,tv na website baadae
Ndugu yangu unajua umuhimu wa media kwenye siasa? Je wajua information is power? Kuwa na taarifa sahihi kwa wakati muafaka ni nguvu na ushindi wa hali ya juu sana, mf kama matusi ya Lusinde na wenzake yangesikika nchi nzima unajua impact yake kwa ccm ingewagharimu mpaka kipindi cha uchaguzi mkuu. Kwakifupi ni muhimu kwa cdm kuwa na vyombo vyao vya habari vyenye kuwafikia wananchi wengi kwa wakati mmoja.
 
mmmh
kazi kweli kweli! mmeshindwa kuchakachua zilizopo? naona kadiri siku zinavyoenda TV za bongo zinazidi kuwapa mkono wa kwaheri. Nakumbuka ITV ilikuwa inawapa coverage sana ila nahisi wameshituka. maneno hayaendani na matendo.
OK
ila ni wazo zuri mpate kuuza sura.
 
mna mawazo finyu ofisi yenyewe hamna makao makuu ni kibanda badala kwanza mfikirie kujenga ofisi mnafikiria Tv hovyo kabisa, inaonekana viongozi wenu wamekaa mkao wa kula, hapo hakuna TV wala Ofisi itakayojengwa.
 
Akili kama za Lusinde
 
Presha inawapanda,Presha inawashuka na bado mpaka uharo uwatoke nyie magambazi
 
Ndugu yangu unajua umuhimu wa media kwenye siasa? Je wajua information is power? Kuwa na taarifa sahihi kwa wakati muafaka ni nguvu na ushindi wa hali ya juu sana, mf kama matusi ya Lusinde na wenzake yangesikika nchi nzima unajua impact yake kwa ccm ingewagharimu mpaka kipindi cha uchaguzi mkuu. Kwakifupi ni muhimu kwa cdm kuwa na vyombo vyao vya habari vyenye kuwafikia wananchi wengi kwa wakati mmoja.

Umeongea point mkuu.
CHADEMA wangekuwa na TV, Lusinde angejiuzulu mwenyewe hata bila kulazimishwa...
 
mmmh
kazi kweli kweli! mmeshindwa kuchakachua zilizopo? naona kadiri siku zinavyoenda TV za bongo zinazidi kuwapa mkono wa kwaheri. Nakumbuka ITV ilikuwa inawapa coverage sana ila nahisi wameshituka. maneno hayaendani na matendo.
OK
ila ni wazo zuri mpate kuuza sura.
Wewe gamba mwenzako amejitokeza kuwa anaitwa William malecela baada ya kuteuliwa kugombea ubunge wa east Africa najua muda si mrefu hata wewe tutakujua baba yako ni nani kwenye huo usultan wenu
 
Back
Top Bottom