MAKOLE
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 618
- 280
Poleni na hongereni kwa kazi wana jf. Naomba kwa mtu anayefahamu hatua za kuanzisha NGO, Ushauri wa usajili na masuala mengine ya ki uzoefu wa namna ya kuendesha NGO anieleze kupitia jf. Tafadhalini naombeni msaada wenu waungwana. NGO yenyewe inahusika sana na mojawapo kati ya mambo yafuatayo; Msaada wa kisheria kwa wanawake, miradi ya utunzaji mazingira, misaada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na waishio katika mazingira maalum, elimu kwa waathirika wa HIV/AIDS.