Kuanzia leo natangaza rasmi kuacha kutazama taarifa za TBC1

Tangu siku ile ya hafla ya Prince Charles pale ikulu, nilianza kujihoji uhalali uhalali wa kodi yangu kuiendesha TBC1. Ila leo uzalendo basi tena hata kama ni hiyo kodi yangu waendelee kula tu.

Ina maana gani kutuonesha picha za barabarani za tukio la Mbeya badala ya kutuonesha wahanga wa tukio hilo. Wameshindwaje kwanda hospitali kuona majeruhi na maiti wa tukio hili. Wamewezaje kutuonesha makaburi ya wachina waliokufa miaka zaidi ya 40 iliyopita lakini wameshindwa kutuonesha ndugu zetu wa mbeya.

Kuna sababu gani ya mimi kuendelea kuitazama tv hii. Eti Ukweli na Uhakika! Upuzi mtupu. Wanasoma sms za watu wanaomsifia mzee tu na kilimo kwanza, ina maana haikuwepo hata moja ya kuwapa pole wahanga wa tukio. Uchakachuaji gani huu jamani?

Kuanzia leo naiacha rasmi TBC.

Nawatakieni kila la heri nyie mnaoendelea kuiamini.

Mkuu upo dunia ipi? Kule Misri, Tunisia na Libya uliona television za taifa zikitangaza revolutions? Grow up.
 
Mi huwa naangalia ze komedi tu!

Mimi nilianza kuisusia ze comed kwanza. Niliona wana edit sana sauti, wanakatakata maneno mpaka hata fleva ya kusikiliza inapotea kabisa.
Sikuona sababu ya kuedit kila siku badala ya kuwaambia waigizaji wawe wanatumia maneno wanayotaka wao. Wakuwa wanasubiri akina Seki wameishamaliza kurecord kipindi chao wakishapeleka tu studio wao ndio sasa wanaanza kukatakata maneno. Wanakera sana hawa jamaa.
 
Back
Top Bottom