Kuanzia leo natangaza rasmi kuacha kutazama taarifa za TBC1

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,691
633
Tangu siku ile ya hafla ya Prince Charles pale ikulu, nilianza kujihoji uhalali uhalali wa kodi yangu kuiendesha TBC1. Ila leo uzalendo basi tena hata kama ni hiyo kodi yangu waendelee kula tu.

Ina maana gani kutuonesha picha za barabarani za tukio la Mbeya badala ya kutuonesha wahanga wa tukio hilo. Wameshindwaje kwanda hospitali kuona majeruhi na maiti wa tukio hili. Wamewezaje kutuonesha makaburi ya wachina waliokufa miaka zaidi ya 40 iliyopita lakini wameshindwa kutuonesha ndugu zetu wa mbeya.

Kuna sababu gani ya mimi kuendelea kuitazama tv hii. Eti Ukweli na Uhakika! Upuzi mtupu. Wanasoma sms za watu wanaomsifia mzee tu na kilimo kwanza, ina maana haikuwepo hata moja ya kuwapa pole wahanga wa tukio. Uchakachuaji gani huu jamani?

Kuanzia leo naiacha rasmi TBC.

Nawatakieni kila la heri nyie mnaoendelea kuiamini.
 
mara ya mwisho niliiangalia wakati waziri mkuu anajiuzulu.wanafki sana hawa wanasifu tu serekali badala ya kueleza matatizo ya jamii
 
Mimi nimeishia tu kwenye habari za nyumbani, vipi wamekumbuka kuonesha sakata la UDSM japo kwenye habari za kimataifa?
 
Natamani kuungana nanyi kuisusia TBC1,lakini ndiyo pekee inayopatikana huku niliko!nifanyeje kuwaunga mkono?!
 
Hawa mahodari wa kutangaza vurugu za nchi jirani mfano kenya au Rwanda kwa style ya kushabikia ehhe mnaona! Wanasahau bila haki amani hutoweka popote Mwenyezi Mungu atuepushe.
 
nakuunga mkono kuna wazee nawaona wanaangalia cnn na bbc nilikuwa sijui kumbe tz media ni hovyo hovyo
 
Natamani kuungana nanyi kuisusia TBC1,lakini ndiyo pekee inayopatikana huku niliko!nifanyeje kuwaunga mkono?!

JF inakutosha kabisa, kila kitu kipo hapa mkuu. Wewe ungana nami tu.
 
Kama una interest na miaka 50 ya uhuru wewe angalia TBC1, vinginevvyo unapoteza muda hawana jipya kabisa.
 
mimi nitaendelea kuitazama TBC ukweli na uhakika...pole yako kama inakubore

Asante, nimaeishapoa kwenye JF.
Hata hivyo nimeamua kuisusia mwenyewe wala sijakushauri uiache. Ila kama unaona haikuhusu kwanini umejibu?
 
TBC real wanaudhi sana,wana kile kipindi chao asbh"jambo cjui' kuna wakati wanasoma magazeti,basi heading yoyote inayozungumzia negative serikali hata kama ni truth ama matukio yoyote negative kwa gvt wanayaruka kuna mtangazaji anaitwa Amina Mollel aliniudhi sana siku hiyo nimetune tbc
 
Tangu siku ile ya hafla ya Prince Charles pale ikulu, nilianza kujihoji uhalali uhalali wa kodi yangu kuiendesha TBC1. Ila leo uzalendo basi tena hata kama ni hiyo kodi yangu waendelee kula tu.

Ina maana gani kutuonesha picha za barabarani za tukio la Mbeya badala ya kutuonesha wahanga wa tukio hilo. Wameshindwaje kwanda hospitali kuona majeruhi na maiti wa tukio hili. Wamewezaje kutuonesha makaburi ya wachina waliokufa miaka zaidi ya 40 iliyopita lakini wameshindwa kutuonesha ndugu zetu wa mbeya.

Kuna sababu gani ya mimi kuendelea kuitazama tv hii. Eti Ukweli na Uhakika! Upuzi mtupu. Wanasoma sms za watu wanaomsifia mzee tu na kilimo kwanza, ina maana haikuwepo hata moja ya kuwapa pole wahanga wa tukio. Uchakachuaji gani huu jamani?

Kuanzia leo naiacha rasmi TBC.

Nawatakieni kila la heri nyie mnaoendelea kuiamini.

NDUGU YANGU MRIMI ULICHELEWA SANA! YAANI BADO ULIKUWA UNAITAZANA??????? ''POLE''' ILA HONGERA HUJECHELEWA UMEAMUA WAKATI MUAFAKA. NAKUMBUKA WAKATI WA UCHAGUZI WA IGUNDA ASUBUHI MOJA NILIFUNGUA TBC1, SI KWA KUWA NAIPENDA LAHASHA BALI ITV ILIKUWA HAIPATIKANI....Nilichokuta ni kipindi cha kusoma magazeti (Vichwa vya habari).
KITUKO CHENYEWE NI HIKI''''''' Magazeti mengi yalikuwa yanaongelea uchaguzi'' na kwa namna moja au nyingine Mvuto wa CHADEMA ulitawala magazeti mengi. Sasa cha Ajabu Yule Msomaji wa TBC1 Kila Akikuta Gazeti Lina kichwa cha habari kikubwa kinahusu Chadema, Mathalani kinasema '''' CHADEMA YAKUSANYA MAELFU''' Mtangazaji hakukisoma kabisa bali aliishia kusema ''' nachukua Gazeti fulani analitaja mambo ni yale yale siasa huko Igunga! halafu anaenda kutafuta Kakichwa kadogo kahabari kamejificha kamendandikwa Waziri mkuu aasa vyama kuvumiliana!!!! '''MAAJABU HAYA''' Haingii Akilini Kabisa!!!!!!!!! Mara Akafungua Gazeti Lingine ambalo kwa mtazamo wangu linashabikia Chama'' WATALA'' ...Kichwa hicho cha habari kilikuwa juu kabisa kama kile cha CDM lakini kwa kuwa Kilihusu chama WATALA Alikisoma Kwa mbwembwe ati!'''' CHAMA WATALA Kushinda kwa Kishindo....UNAFIKI HUU!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Hiyo ndo TBC! Ukweli na Uhakika....Kama Mtu haamini subiri uchaguzi wowote au maswala yahusuyo Upinzani!!!
 
Kila siku tunasema CDM tuanzishe TV yatu hata kwa kuchangishana au hata redio lakini viongozi wako kimya
 
Back
Top Bottom