Kuanguka kwa Sumaye na kupeta kwa mafisadi nini tafsiri yako?

Sijui una maana gani unapotumia neno "udhu" ila kama una maana ya "usafi" basi nadhani humfahamu vizuri huyu jamaa. Frederick Sumaye ninayemjua mimi ni mmoja wa waasisi wa ufisadi ndani ya CCM. Kwa kumbukumbu zangu huyu jamaa wakati akiwa waziri mkuu aliwaambia wafanyabiashara kuwa yeyote anayetaka mambo yake yamnyookee lazima ajiunge na CCM. Matokeo yake ni wimbi la wafanyabiashara kuingia ndani ya CCM na kuzigeuza siasa za ndani ya chama kuwa biashara ya kuuza na kununua kura. Kama sikosei hajawahi kujibu kashfa ya kutumia vibaya madaraka pale alipojibinasfishia mashamba ya ushirika ya kijiji akiwa waziri mkuu .

Sijarlewa mashamba ya ushirika yepi,mbona km alishakanusha hiyo issue,inshort binafsi siwezi kumlinganisha sumae na genge la mtandao linalotaka kukamata nchi 2015 ni balaa tupu ni bora hata na la sasa,yatu watu wanaopita kwa rushwa ni hatari ni lazima fedha zao zirudi
 
Haya ni baadhi ya mambo ya kifisadi yaliyosimamiwa barabara na Sumaye kwa miaka kumi akiwa waziri mkuu chini ya utawala wa Mkapa:

1/Uuzwaji wa mashirika ya umma ovyoovyo.

2/Mikataba ya kitapeli kwenye madini.

3/Alihusika kuchukua 10% yake wakati wa uuzwaji wa NBC kwa bei ya kutupa.

4/Alitumia nafasi yake kama PM kuchukua mkopo usiohalali NSSF.

5/Alisisimamia kwa nguvu zote bungeni kufanikisha ununuzi wa rada na ndege ya rais katika mazingira tata.

6/Alisimamia kwa nguvu zote pamoja na Magufuli, uuzwaji wa nyumba za serikali kwa vigogo na yeye akichukua za kwake kadhaa.

7/Ndio mwasisi wa mpango wa vigogo kujimilikisha Lanchi za taifa, yeye ana za kwake kadhaa Arusha na Manyara achilia mbali shamba kubwa la mifugo kibaha.

8/Alijimilikisha soko kubwa la mazao hasa mahindi la Kibwaigwa.

9/Ilisemekana alikuwa amefisha zaidi ya bilioni 50 nje ya nchi, hasa benk za uswisi

10/Alikuwa anasimamia kwa karibu sana kutoa misamaha tata ya kodi kwa wafanyabiashara hasa wenye asili ya kiasia(Ni Sumaye aliyetoa kauli kuwa ukitaka mambo yako kibiashara yaende vizuri basi ahamia CCM)

11/Alisimamia serikali bungeni kupitisha sheria ya kuhalalisha Rushwa kwenye uchaguzi kwa jina la Takrima.

12/Ilisemekana alikuwa anaumiliki wa maghorofa kadhaa katikati ya majiji ya Arusha, Mwanza na Dar ambayo yalikuwa yanajengwa kwa kasi kama uyoga.

Kweli tanzania sikio la kufa,watu tunapoza rushwa,sumaye amelalamikia rushwa na sio nafasi ya urais
 
Huyu mzee FS aliaga kuwa anaenda HARVARD kusoma.Kumbe hata kanuni rahisi HAJUI.kanuni mbili zingemtoa
1.Hawezi kusukuma gari akiwa ndani ya gari hilo hilo maana atasukuma uzito wako!Kuendelea kuwa kwenye mfumo uliofisadika akitegemea usafi,eti mnaita udhu,ni ndoto ya alinacha.
2.Hawezi kudai usafi wowote iwapo wakati wa kupitisha ile sheria ya takrima alichekelea,maana alisahau kanuni ya Emanuel Kant:hebu jitahidi kufanya mambo yale ambayo yangefanywa kanuni/sheria dunia nzima na wewe ungeeependa kufanyiwa!Haitofautiani na ile ya kumpenda jirani kama nafsi yako:
3. Sijui, IWAPO msomi huyu wa Harvard,sijui yenyewe au hili ni tawi la wachovu huko HARVARD ,ANGESHINDA UCHAGUZI KWA MUUJIZA WOWOTE KAMA ANGELISEMA MANENO HAYA HAYA KWA MSISITIZO HUO HUO
4.NI WAKATI MZURI BAADA YA MANENO HAYA ANGETANGAZA KUSTAAFU KUTOKA KWENYE KILE ALICHOKIITA MHESHIMIWA ROSTAM AZZIZI(kama alivyokuwa wakati huo) siasa za majitaka za CCM,aje CDM,AKATAE CHEO CHOCHOTE,ASHIRIKI HISTORIA AZIZI YZ KUIKOMBOA NCHI,MAANA KUMBE KILA MTUME WA SASA HUENDA ALISHAPITA MAPITA FULANI NA KILA MWENYE DHAMBI ANA NAFASI AZIZI YZA KUONGOKA NA KUWA MTUME!
 
Sijarlewa mashamba ya ushirika yepi,mbona km alishakanusha hiyo issue,inshort binafsi siwezi kumlinganisha sumae na genge la mtandao linalotaka kukamata nchi 2015 ni balaa tupu ni bora hata na la sasa,yatu watu wanaopita kwa rushwa ni hatari ni lazima fedha zao zirudi

Frederick Sumaye ni mhanga wa mfumo wa siasa aliousimamia yeye mwenyewe ndani ya CCM - yaani mfumo wa kuuza na kununua kura. Ni unafiki tu unamsumbua kulalamika eti kuna mtandao wa rushwa kwenye kura.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom