Ingawa uchaguzi wa CCM ni wao, hakuna kitu kimenishangaza kama watu wenye udhu kama Fredrick Sumaye waziri mkuu wa zamani kuangushwa na Mary Nagu mtuhumiwa wa kughushi vyeti vya taaluma. Nimeshangaa kwa mafisadi kama Edward Lowassa na Andrew Chenge kupeta huku watu wenye udhu kama Sumaye kutupwa nje. Je CCM na wanachama wake wameanza kujitofautisha na biashara ya kula takrima bila kujali kama wanayemchagua ni fisi, fisadi au chatu? Nini mawazo yako?
Sijui una maana gani unapotumia neno "udhu" ila kama una maana ya "usafi" basi nadhani humfahamu vizuri huyu jamaa. Frederick Sumaye ninayemjua mimi ni mmoja wa waasisi wa ufisadi ndani ya CCM. Kwa kumbukumbu zangu huyu jamaa wakati akiwa waziri mkuu aliwaambia wafanyabiashara kuwa yeyote anayetaka mambo yake yamnyookee lazima ajiunge na CCM. Matokeo yake ni wimbi la wafanyabiashara kuingia ndani ya CCM na kuzigeuza siasa za ndani ya chama kuwa biashara ya kuuza na kununua kura. Kama sikosei hajawahi kujibu kashfa ya kutumia vibaya madaraka pale alipojibinasfishia mashamba ya ushirika ya kijiji akiwa waziri mkuu .