Kuanguka kwa Sumaye na kupeta kwa mafisadi nini tafsiri yako?

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,719
Ingawa uchaguzi wa CCM ni wao, hakuna kitu kimenishangaza kama watu wenye udhu kama Fredrick Sumaye waziri mkuu wa zamani kuangushwa na Mary Nagu mtuhumiwa wa kughushi vyeti vya taaluma. Nimeshangaa kwa mafisadi kama Edward Lowassa na Andrew Chenge kupeta huku watu wenye udhu kama Sumaye kutupwa nje. Je CCM na wanachama wake wameanza kujitofautisha na biashara ya kula takrima bila kujali kama wanayemchagua ni fisi, fisadi au chatu? Nini mawazo yako?
 
mimi sio muislamu ila hebu uliza mislamu udhu ni nini halafu jibu ufananishe ni Sumaye! ndani ya CCM hakuna mwenye udhu hata mmoja!1
 
Ukidhani umesimama angalia usianguke....maisha yanaenda hayasimami kumsubiri mtu.
 
Principle ya sehemu yoyote ni kuwa ukiondoka kwenye position, unapoteza network (mtandao) na influence. Hiki ndo kilichomgharimu Sumaye. Ila kumuita mwenye udhu sidhani kama ni msafi kiasi hicho, maana naye alipokuwa madarakani tuliona alichofanya!
 
Simple,JK bado anamhofia Sumaye,kumbuka ile kauli yake kwamba "ukiingia madarakani kwa kalamu utabaki kwa risasi",nadhani anaogopa visasi kwasababu inasemekana na yeye ni mtu wa hivyo.
 
Mimi nakushangaa wewe mleta mada. Kama hao unawaita mafisadi bado ni Wabunge na wengine wenyeviti wa bunge unahitaji shahada ngapi kujua kwamba Chama ndio tatizo? "tumefika hapa kwa sababu ya uzembe wa Bunge, udhaifu wa JK na uozo wa CCM"- JJ Mnyika (Mb).
 
Ukweli ni kwamba Nagu alibebwa na wakubwa. Full stop. Rushwa kwa kwenda mbele.
 
Wakuu nguvu kubwa sana imetumiwa na SSM kuhakikisha Sumaye hashindi!!! Pesa kibao ilimwaga kupita kiasi. Na mkono wa mamvi pia upo kwa sana kwa sababu fulani fulani hivi. Katika hali ya kawaida yule mama asingepata kura, hatakiwi kule japo anatumia nguvu nyingi sana kutaka kutetea kiti cha ubunge. Rushwa zilikuwa zinapitishwa usiku wa manane!! Fisadis at work!!
 
Huyu sumaye hata akigombea kitu chochote hawezi kabisaa kushinda. niko tayari kumpigia maiti kura kuliko kumpatia sumaye. Yaani alikuwa waziri mkuu tanganyika miaka kumi na akshindwa kabisaa kutatua kero ya magari msongamano ktk barabara ya ali hussein Mwinyi.
 
EL na FS wote ni mafisadi wakuu ila EL ufisadi wake unafahamika zaidi. Ukijua na ya FS basi hutakaa umwamini yeyote ndani ya CCM. Kwa taarifa yako ufisadi ni sera ya CCM ndio maana wananchi tunapiga kelele wafukuzwe lakini ndio kwanza wanapongezwa na kupewa madaraka zaidi!
 
Back
Top Bottom