Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

kamanda cha kujua watu hapa siyo watoto fukuza majambazi la z sivyo lazima ukubali CCM haiwezi kudumu kwa kuwakumbatia majambazi. Tuko makini na hili mkuu
Tatizo watu wakijua kubonyenza keyboard huona kuwa wanajua kila kitu... huyo anayesema ccm lazima ife hana lolote jipya... hili bandiko ni nzito sana lakini limekosana nyama, sasa bora tupige soga tu.. ndio maana nasema ni ndoto
 
Mkuu unajua usipokuwa na mawazo kuwa CCM itakufa basi utakuwa umepitwa na wakati. nani achukue CCM mafisadi au? kuna mtu yuko tayari kupoteza au unafikiri migogoro iliyopo sasa inatoka wapi? kanu imekufa lakzima CCm kwa sababu ilianzishwa na watu lazima ife tu. CCM sasa hivi ni kampuni ya kuwalinda majambazi na kama haitawafukuza majambazi lazima ife tu.
KANU ilikufa kirahisi hivyo kama unavyofikiria?kusingekuwa na MUUNGANO WA VYAMA KANU ISINGENG'OKA kamwe?
Ndugu yangu ni rahisi kuanzisha vita lakini ni ngumu kuimaliza!sasa kuzaliwa kwa CCM ni tofauti kabisa na kifo chake!CCM haitakufa kwa kuiponda kwenye internet!kwani babu zangu kule Ng'wamalasa hawana hata neti hata magazeti hawasomi?ni kazi sana kusasababisha kifo cha CCM!
ila hakuna kitu kisichoshindikana kumbuka maneno matupu hayamtoi nyoka pangoni!
 
KANU ilikufa kirahisi hivyo kama unavyofikiria?kusingekuwa na MUUNGANO WA VYAMA KANU ISINGENG'OKA kamwe?
Ndugu yangu ni rahisi kuanzisha vita lakini ni ngumu kuimaliza!sasa kuzaliwa kwa CCM ni tofauti kabisa na kifo chake!CCM haitakufa kwa kuiponda kwenye internet!kwani babu zangu kule Ng'wamalasa hawana hata neti hata magazeti hawasomi?ni kazi sana kusasababisha kifo cha CCM!
ila hakuna kitu kisichoshindikana kumbuka maneno matupu hayamtoi nyoka pangoni!

Vyama vya siasa tanzania vimeshaungana lakini juzi juzi tu CUF iliwatolea nje CHADEMA wasiwe kwenye meza moja kuongelea masuala ya muafaka na ccm, mwaka mmoja before that mbowe alinukuliwa akisema kwamba wapinzani wapo kwa sababu wamepandikizwa na ccm ili wawatetee ccm, na kuongeza kwamba mreama ni mroho wa madaraka ! leo je huyo aliyeongea haya maneno yupo wapi ? KAUNGANA NAO HAO HAO ALIOKUWA ANAWAPONDA WENZAKE ! sasa tumchukulie kama mropokaji ? nae yupo kama hao aliowakandia ? yaani hata nashindwa kumuelewa yeye mbowe na wenzake !
 
CCM ikifa lazima tujue hao waliomo humo watahamia kwenye chama chenye nguvu wakati huo sasa hapo kama watawakaribisha hao walio toka kwenye CCM iliyo kufa basi na ufisadi nao utahamia kwenye chama walicho kimbilia au walicho jipenyeza kwa hiyo tutapata akina rostam,chenge,mkono,balali na wengine kibao wataenda tu huko.
 
Its true ! CCM haiwezi kufa ila kuna watu ndani ya CCM watakufa na infact wamekwisha anza kufa natural Death, watapukutika taratibu hadi ibaki ccm safi, alama za nyakati zinaonyesha hivyo!
 


1.CCM haiwezi kufa,

2. isipokuwa viongozi wabovu tu ndio wanaotakiwa kutoka au kutolewa mara moja,

3. CCM kama chama haina kosa lolote

4. viongozi wachache wabovu na mafisadi!

1. Hii sawa

2. Watatoka lini na nani yuko responsible kuwatoa wakati kila kukicha wanajikita katika kuhakikisha hawashikiki?

3. Kosa ni kukaa na MAFISADI(Mapepo) wabaya bila kuwakemea, ni sawa sawa na yule mwenye mifugo inayokwenda kuvamia mashamba ya majirani halafu mwenye shamba akilalamika, mwenye mifugo aseme hana kosa.

4. Lakini ndio wameshika mipini na ndio decission maker katika chama.
 
Its true ! CCM haiwezi kufa ila kuna watu ndani ya CCM watakufa na infact wamekwisha anza kufa natural Death, watapukutika taratibu hadi ibaki ccm safi, alama za nyakati zinaonyesha hivyo!

Tayari wameandaa watoto wao wa kuzaa kukamata nafasi hizi!
 
ccm kufa halina shaka, kila kilichozaliwa kitakufa. hata wewe mimi na wengine tutakufa. the matter of time
 
Sasa hiyo CCM ikifa waliokuwa mafisadi ndani yake wataenda wapi?

Kwangu mimi nasema kwamba linalotakiwa kufa si jina CCM bali wale ambao kwa pamoja wanafanya CCM iwe CCM. Wale wote waliofanya CCM ipotezwe mwelekeo. Wale wote waliokumbatia mafisadi na Mafisadi wenyewe!

Hao ndo wa Kutokomezwa!
 
Tayari wameandaa watoto wao wa kuzaa kukamata nafasi hizi!

Kweli kabisa kila mtoto wa kigogo anajianda kushika hatamu ndani ya CCM kwa hiyo humo wanalithishana tu vyeo.Yaani hapo ni transfar ya ufisadi toka kwa baba kwenda kwa mtoto.
Mtoto wa nyoka ni nyoka tu hawezi kuwa mjusi wakuu.
 
My take

Tuliambiwa tukasema wanazusha, tukasikia wenyewe bado hatukuami, sasa tunayaona kwa macho yetu lakini kama ndege aliye mwagiwa maji, wala hutushtuki tena. Forget about CCM na kufa au kufufuka. Swali! Wako wapi Watanzania safi wakuipigania nchi hii? Kama wapo are they patriotic enough to take their responsibility kama watoto wa Tanzania? Kufa kwa CCM hakutasaidia lolote kama Watanzania tutabaki kushabikia, kukosoa tukiwa nje, (bila kuwa wanachama wa chama chochote) na kushangilia wachache wanaotambua na kujua wajibu wao kama watanzania na kuufanyia kazi. Tunachohitaji ni watanzania kuwa patriotic na kutimiza wajibu wao kama raia popote walipo. Baada ya hapo naamini CCM ITAKUWEPO, mafisadi HAWATAKUWEPO (kama wapo hatutaogopa kuwashughulikia) na VYAMA VINGINE MBADALA VYENYE NGUVU KULIKO CCM VITAKUWEPO. Hapo panafikika, lakini sio kwa dua za CCM kufa, bali kwa sisi watanzania kutimiza wajibu wetu kweli kweli. It is time we wake up and play our part in turning this country around, (sio kelele tuuu kila siku)
 
watu wengine wakisikia neno kifo wanatishika sana,lakini kimantiki lazima kinachozaliwa lazima kife,na hata Yesu Kristo alishasema mbegu lazima ife ili iote na sayansi ya mimea imethibitisha hilo.

Tatizo ninaloliona ni kwamba watu wanaiona CCM kama ni mungu wa Tanzania sasa wanajiuliza "hivi CCM ikifa hatima ya Tanzania itakuwaje: hawa kwa mujibu wa Mwalimu Nyerere ni wajinga tuu yaani hawajui na kwa bahati mbaya hawajui kama hawajui

Achilia mbali vyama vya siasa, historia inatuonyesha kwamba hata tawala kubwa kabisa za dunia hii hufa. Uajemi kabla ya kuja kwa tawala ya kirumi ndiyo ilikuwa tawala kubwa sana duniani lakini ilianguka na hiyo urumi yenyewe ikaporomoka na ndiyo asili ya kuwa na kanisa la Roma lenye nguvu duniani

kwa hiyo siyo CCM tuu hata Marekani siku moja itakoma kuwa tawala kuu ya dunia, kinachogomba hapa ni suala la muda. ukitaka kujua kama CCM itakufa au la ni lazima ujiulize kwa vigezo vipi CCM iko hai.

uhai wa chama chochote cha siasa ni uchangamano wake kwenye jamii inayoiongoza na kujitegemea yenyewe bila ya kuegemea dola. CCM inatumia sana nguvu ya dola na rasilimali za nchi kuendelea kuwepo madarakani na hivyo kuonekana kuwa hai

siku CCM ikiwa haina vyeo vya kimadaraka ya serikali hakuna atakayetumia "vijisenti"vyake kuomba uongozi ndani ya chama hicho, wala ile hofu ya wafanyabishara kukichangia chama hicho itakufa.

Kama ilivyoitokea KANU kwa kunyang'anywa majengo na rasirimali za umma walizojigawia walipokuwa madarakani ndivyo itakavyokuwa kwa CCM pia. watanyang'nywa Kirumba,kambarage,SUKITA,Samora,sokoine,Jamhuri ya Dodoma na Morogoro na mali nyingine nyingi

lakini kwa sasa njia ya mkato ni kuhakikisha kwamba CCM inakufa kwanza ili tuweze kurudisha mali zetu mikononi mwetu. na njia rahisi ya kuiua CCM ni kuwahamasisha wananchi waikatae na hata wanapotishwa kwa mtutu wa bunduki!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom