Kuandikwa au kufutwa kazi na sintofahamu hiyo

L'AMOUR

Senior Member
Mar 8, 2011
110
24
Imenishangaza kutumika kwa Tanzania maneno kama kuandikwa na kufutwa kazi pia hali ya sintofahamu. Sasa najiuliza yale maneno yetu ya kuajiriwa au kupata kazi na kufukuzwa kazi ni yepi hasa ndio tuyatumie? Haya maneno nimezoea kuwasikia wakenya kupitia TV zao na sasa yameingia Tanzania na tunakutana nayo magazetini. Je magazeti au vyombo vya habari vinaruhusiwa kutumia lugha yoyote hata kama inaweza kupotosha umma?
Natangulisha shukurani za dhati kwa kunijengea kiswahili kizuri
 
nimemsikia mkuu wa nchi akitumia neno 'sintofahamu', nalo hili sijui limetokea wapi na nini hasa maana yake.
 
Imenishangaza kutumika kwa Tanzania maneno kama kuandikwa na kufutwa kazi pia hali ya sintofahamu. Sasa najiuliza yale maneno yetu ya kuajiriwa au kupata kazi na kufukuzwa kazi ni yepi hasa ndio tuyatumie? Haya maneno nimezoea kuwasikia wakenya kupitia TV zao na sasa yameingia Tanzania na tunakutana nayo magazetini. Je magazeti au vyombo vya habari vinaruhusiwa kutumia lugha yoyote hata kama inaweza kupotosha umma?
Natangulisha shukurani za dhati kwa kunijengea kiswahili kizuri

Si wewe tu unayeshangaa. Unajua tatizo ni kupenda kuiga bila kufikiri sawa sawa. "Kuandikwa na kufutwa" sio maneno sahihi kwa maoni yangu. Inashangaza sana kuona kuwa watu wanaotakiwa wajifunze kiswahili kwetu (Wakenya) ndio tunaowaiga.
Hilo la sintofahamu kwanza limeanzia redio za kimataifa (sana sana Sauti ya Ujerumani, na BBC). Halina maana pia. Wanaolitumia nadhani wanataka kumaanisha dhana inayobebwa na neno "CONTROVERSY" katika lugha ya kiingereza. Waseme tu "Utata".
Mimi huwa nakasirika sana japo kitaluma sio mweledi wa lugha. Ni sawa na wanaotumia neno"nimeboreka" wakimaanisha "am bored". Sasa jamani kuboreka ni mnyambuliko wa mzizi wa neno "bora" ambao unamanisha kuwa bora zaidi. Kwa nini hao wasiseme "nimeudhika"? au "sijafurahia"?
 
Kwa hiyo ni suutafahamu??? Nashukuru kama ni kiswahili sahihi na vipi hawa waandishi wa habari huwa wanasisitizwa kusomea lugha kama ilivyokuwa zamani kwenye kozi zao za HGL, HKL au KLF ili waweze kutufundisha sisi wasomaji,wasikilizaji au watazamaji wa TV? Kama ni hivyo basi kiswahili kinakuwa na kama si hivyo basi ni kwa nini wanaachia watu wachache wachafue fani yao bila sababu. Pia mkuu kama neno sahihi ni suutafahamu je si sahihi kulitumia kama kuna utata kama mdau alivyoeleza hapo juu?? Tafadhali tujulishe jinsi ya kutumia maana hii lugha inachezewa mpaka wageni wanatudharau kwa kuiga kiswahili chao kibovu kisicho na ladha ya matamshi. Naomba niwasilishe tena hoja hii kwa waliobobea. Ahsante
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom