Kuandamana na mpenzi au mke wako popote,kila inapobidi.

Tall

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
1,425
165
Kuna watu huandamana na wake zao au wapenzi wao popote waendapo,hao huitwa kumbikumbi,na wapo wanaosema,kuandamana na mpenzi wako kila uendako si tabia nzuri,
ina hasara nyingi sana kuliko faida Mwana JF unasemaje?
 
hakuna hasara, ni faida sana tena hakuna raha kama ya kuandamana na mpenzi/mke/mume wako!
 
Ni jambo zuri lakini inategemea na maeneo mnayoambatana.Maeneo ya Uswahilini ni karaha tupu na umbea kila kona kiasi kwamba mnakuwa hamuoni hata hiyo raha ya kuwa pamoja.
 
hakuna hasara, ni faida sana tena hakuna raha kama ya kuandamana na mpenzi/mke/mume wako!

kweli kabisa kuandamana na mkeo au mpenzi wako ni safi sana.wanaopinga watakuwa mienendo yao katika mahusiano si mazuri yaani matendo yao si mema mbele ya wapenzi wao
 
ni jambo zuri lakini inategemea na maeneo mnayoambatana.maeneo ya uswahilini ni karaha tupu na umbea kila kona kiasi kwamba mnakuwa hamuoni hata hiyo raha ya kuwa pamoja.
tena uswahilini mvuta bangi mmoja anaweza akaamua kuanza kukutukana matusi ya nguoni mbele ya wife.hapo itabidi ufe(upigane) kulinda heshima inapobidi
 
Kwangu mimi si kuongozana na mke tu, naona fahari sana kuongozana na wife na watoto
 
Kama safari inawahitaji wote kwa pamoja powa lakini sio kuandamana kila kona bila sababu ili mradi tu mmeonekana pamoja kila saa mtachokana.ni vizuri saa nyingine mkatengana kidogo hili mtamaniane zaidi.
 
Kuandamana na mke/mme ni vizuri kutegemea na sehemu mnayoenda, mfano kama wewe mme unashughuli zako zinazohitaji uharaka, mtagombana bure na mke wako kwa vile tembea yao ni ya konokono. Pia nilishawahi kushuhudia jamaa yangu akiwa na mke wake yaani jumla tulikuwa watatu, mimi, jamaa yangu na mke wake tukafika sehemu vijana wakaanza kumuita mke wa jamaa nae akauchuna wakaanza kumtukana kiasi kwamba mie sikufurahishwa na tabia hiyo.
Ila kwa ujumla inabidi angalau mara mojamoja tuandamane na familia zetu/mke/mme.
 
Kuna watu huandamana na wake zao au wapenzi wao popote waendapo,hao huitwa kumbikumbi,na wapo wanaosema,kuandamana na mpenzi wako kila uendako si tabia nzuri,
ina hasara nyingi sana kuliko faida Mwana JF unasemaje?
kuandamana kila sehemu ni ishara kwamba you are both comfortable and proud of each other, in many cases hii kitu huboresha penzi na kuongeza maelewa na kuaminiana

asikwambie mtu, kuandamana kila sehemu ni kitu kizuri... tatizo la watu wengi ni zile skeletons tunazoficha
 
Kuna watu huandamana na wake zao au wapenzi wao popote waendapo,hao huitwa kumbikumbi,na wapo wanaosema,kuandamana na mpenzi wako kila uendako si tabia nzuri,
ina hasara nyingi sana kuliko faida Mwana JF unasemaje?

Mi naona shwari kwa sababu kama unaweza kutembea na driving license au wallet kila sehemu WHY NOT WIFE naye pia ni Identity yako!!
 
sioni hasara yake hata kidogo ................ila sidhani kama in reality unaweza kuongozana na mpenzi wako kila pahala.

nadhani majukumu ya maisha hayaruhusu hali kama hiyo kwa sasa
 
Kuandamana popote mnapoenda?....yaani kazini, na kwenye kila ishu unayofuatilia!!! mwe
kuandamana kwenda sehemu ni vizuri kama mmepanga, siyo kufuatana (mguu wako mguu wangu)
 
tuandamane kwenye visehemu maalum bwana, siwezi kuacha shughuli zangu za kinyumba/watoto nikaenda nae bar cjui wapi kisa kuandamana, na muda nao wa kuambatana kila mahali unatokea wapi, labda mie cjui....
 
Ni vyema sana kuandamana pamoja

au mie cjawaelewa maandamano mnayoyazungumzia hapa? yaani leo tunatoka job tnaandamana bar huko wanakodaigi wanaenda kupoteza mawazo ya kikazi tunatoka huko cjui saa 4-5? au ni maandamo ya kivipi? mana hayo mie ctayaweza kabisa, hivi mtaandamanaje kila mahali?
 
kuandamana, bar,hotelini,vikao vya arusi.sherehe,mpirani,kuona ndugu,kanisani,msikitini,kwenye muziki/burudani,shambani,safarini............
 
Hamna shuguli nyingine za kufanya?kama hakuna ni vema lakini kama kuna majukumu mengine si vema kuambatana kila kona..Mapenzi hayako katika kuambatana.
 
kuandamana, bar,hotelini,vikao vya arusi.sherehe,mpirani,kuona ndugu,kanisani,msikitini,kwenye muziki/burudani,shambani,safarini............

vingine hapo ni sawa, hiyo ya bar mara moja moja mana majukumu nayo ya kifamilia inabidi tuyaweke sawa.
 
Ni vema kuandamana lakini siyo ndo kila siku kila mahali. Nahisi kama inaweza fika wakati mtabore hivi! Mmelala wote usiku kucha mnazunguka wote mchana kutwa....siku mbili tu mmeshachokana. Stori zitaisha maaana matukio yote mpo pamoja! Au kuna kitu sijaelewa hapa! to me kuandamana occassionally kuna 'ladha' zaidi kuliko kila siku! Hata kisaikolojia kuna nyakati mtu anahitaji muda wa kuwa peke yake.
 
exactly ma bro, mie kama mama nahitajika kuwa nyumbani baada ya mihangaiko ya kutafuta ugali inabidi niwe home kuweka hiki na kile sawa, ni jukumu langu, sasa tukiambatana kila mahali muda wa kuangalia mengineyo nitaupata kweli?
 
Back
Top Bottom