Kuandaa movie ya muendelezo (Series)

pamoja sana kaka...ushauri wangu kwako...member ambao utaungana nao kwa ajili ya hiyo project. mngeteneza group zuri la telegram...then mipango ianzie hapo
 
Ahsante sana mkuu wadau siwaoni ila ahsante sana kwako
 
Mkuu nahisi Burget inategemea na aina ya story utunzi ukifika mahali fulani ndio unaweza kunipa taswira ya budget ya kuanzia
Sawa Sawa.. Ila Series Means Inakuwa na Cast Wengi.. so Kama Utataka Kutoa Movie Ya Uhakika Unatakiwa Kuangalia Mfuko wako Upoje.. soko lq Bongo na Nje linataka nn... Usije Ukaumia Halafu soko likakutupa..

Inabidi Ukae Na Watu muumize kichwa Mtoe Series ya Ukweli
 
jamaa umesema vizuri sana mwanzo wa maandalizi ukiwa mzuri utanipa mwangaza wa mbeleni naamini kitu kua kizuri ni vile unavyojitoa japo kiukweli changamoto ni nyingi.

Nipo nawasiliana na wadau kadhaa Pm sasa na nipo tayari kupokea kila wazo na sitawaacha watakaofanikisha
 
Kwa ushaur tu anza kubuni story ila utangaze na maeneo ya national parks na vivutio vyote tulivo navo Tanzania itasaidia na hasa location iwe maeneo kama tanga au arusha aisee itakuwa poa.. Big up brother una wazo zuri
 
Shukrani sana Babu JP mawazo yako ni mazuri sana tutazingatia hili pia
 
Ok, mkuu mtoa mada kwanza naheshimu Mawazo yako, Ni Mawazo mazuri coz ile kuwaza tu ni hatua moja mbele, sijui uzoefu wako katika hili ila ntajaribu kutoa darasa kidogo ili na watu wengine ambao wapo interesting hata wakichangia wajue wanachangia nini!

Movie na Film ni the same, utofauti ni kuwa neno Film lilitumika miaka hiyo wakati wakitumia film kwa maana ya tape ku record, kuanzia zile film (tape) kubwa, mpaka kuanza kutumia Div miaka ya hivi karibu ambapo sasa Camera zimekua na uwezo mkubwa na nyingi zinatumia Memory Card tu kuhifadhi kile unacho record..
Kuna utofauti kidogo Kati ya Short Film na Series! Short film kwa kuokoa nguvu na muda ni aina ya film ama Movie yenye mwanzo Kati na Mwisho, lakini inapokuja kwenye Series huwa haina mwisho otherwise ni uwamuzi wa Producer mwenyewe kuamua Series yangu itaishia hapa! Ila inaweza kuendelea hata miaka 50 kama Producer atapenda.

Kwenye Series huwa kuna Scene, Episode, Season.....kila Scene kadhaa ni sawa na Episode kadhaa, na kila Episode kadhaa zinakamilisha Season moja! Kwenye Series huwa kuna Episode ambayo huisha kila baada ya 45 mins, kwa wenzetu baadhi ya Series kama Merlin kila Episode inaanza na kisa chake mpaka kinaisha, ikianza Episode nyingine inaanza na kisa kingine n.k.....

Mkuu mtoa mada nije kwako, kabla ya kuandaa Series Movie cha kwanza fikilia soko lako, ni la watu wa aina gani? La ndani ama nje? Kama ume target soko la nje basi lazima utizame story yako, (story ni kwanza kabla ya Quality ya Video) Je! Hiyo story inaweza kuleta ushindani huko International markets? Kama jibu ni ndiyo basi tafuta Wataalam waandae Script, (kumbuka Script ndo Movie) mtu wa kwanza kabisa anayeiona Movie ni Script writer.

Kwa series wanaweza kuwa hata writers 5, 24 hrs imeandikwa na Script writers zaidi ya 7, na wote wamepita mule mule, Script writers lazima wawe na uwezo mkubwa, wenye muono wa mbali, elimu pia, Script ikikamilika mnakaa wadau kupendekeza Director, mtakua na vigezo vyenu all in all lazima awe na uzoefu na uwezo mkubwa, wapo Directors wachache wana uwezo ila Producers ndo wanaharibu!

Mkimpata Director atapitia Script atakuja na Mawazo au Mapungufu, mtayafanyia kazi mtaenda na hatua ya kuunda Crew, kumbuka Kila mtu Ana mipaka yake, Director ni kama vile Coach kwenye team ya mpira, yeye ataunda team yake kuona nani ataweza kumsaidia vizuri, assistance director, location manager, Continuity, n.k, atawaleta kwa Producers kwa makubaliano mengine hasa mkwanja! Ikipita mnaenda hatua inayofuta............

Ngoja niishie hapa ntarudi!
 
Nimerudi..........

Hatua inayofuata ni kutafuta Production house ambayo nayo inatakiwa kukamilika, Cameraman na assistance wake, Video of photography, lights, Vocals, Make up artist na wengine, mmkiweka sawa huko mnatafuta Wasanii sasa! Na hapa ndo tunakosea......!

Wataalam wa story and script writing wanasema, Characters wakubwa kwenye Movie kwa maana ya Main Characters, Supporting Characters na Maadui, lazima watengenezewe tabia kwenye Story/Script, hasa main Character..

Mfano, Anapenda nini, kipi hapendi, anapenda pombe gani, labda anapenda mwanamke mwenye matako makubwa, Ana roho mbaya lakini Ana huruma na watoto n.k, hizi tabia zote huyo Character anatakiwa aziishi kwenye hiyo movie!

Mara nyingi Script writers huwa wanaweka sifa za Characters wake, mfano anamzungumzia Main Character wake lets say. Joe!

Atasema...
Joe kijana mwenye umri wa miaka 30, anaurefu wa futi 6, Ana mwili uliojengeka kimazoezi kiasi, anapenda pombe lakini Ana hasira, anapenda kufanya mazoezi n.k

Pia ataandika sifa za Supporting Character ambaye atakuja kuwa mke/mpenzi wa Joe...

Ataandika....
Anita ni msichana wa miaka 25, Ana urefu wa futi 5.5, mwenye mwili kiasi ila mwenye matako makubwa, anapenda urembo, mazoezi n.k....

Kama Director akianza kuchagua Cast, wajihi wa wahusika ndo kigezo cha kwanza baada ya uwezo wa kuigiza, ataanngalia umri, urefu kama script inavyotaka, na sio kwa sababu wewe Ni mweupe au umeweka wave nywele!.....
 
Ok, mkuu mtoa mada kwanza naheshimu Mawazo yako, Ni Mawazo mazuri coz ile kuwaza tu ni hatua moja mbele, sijui uzoefu wako katika hili ila ntajaribu kutoa darasa kidogo ili na watu wengine ambao wapo interesting hata wakichangia wajue wanachangia nini!

Movie na Film ni the same, utofauti ni kuwa neno Film lilitumika miaka hiyo wakati wakitumia film kwa maana ya tape ku record, kuanzia zile film (tape) kubwa, mpaka kuanza kutumia Div miaka ya hivi karibu ambapo sasa Camera zimekua na uwezo mkubwa na nyingi zinatumia Memory Card tu kuhifadhi kile unacho record..
Kuna utofauti kidogo Kati ya Short Film na Series! Short film kwa kuokoa nguvu na muda ni aina ya film ama Movie yenye mwanzo Kati na Mwisho, lakini inapokuja kwenye Series huwa haina mwisho otherwise ni uwamuzi wa Producer mwenyewe kuamua Series yangu itaishia hapa! Ila inaweza kuendelea hata miaka 50 kama Producer atapenda.

Kwenye Series huwa kuna Scene, Episode, Season.....kila Scene kadhaa ni sawa na Episode kadhaa, na kila Episode kadhaa zinakamilisha Season moja! Kwenye Series huwa kuna Episode ambayo huisha kila baada ya 45 mins, kwa wenzetu baadhi ya Series kama Merlin kila Episode inaanza na kisa chake mpaka kinaisha, ikianza Episode nyingine inaanza na kisa kingine n.k.....

Mkuu mtoa mada nije kwako, kabla ya kuandaa Series Movie cha kwanza fikilia soko lako, ni la watu wa aina gani? La ndani ama nje? Kama ume target soko la nje basi lazima utizame story yako, (story ni kwanza kabla ya Quality ya Video) Je! Hiyo story inaweza kuleta ushindani huko International markets? Kama jibu ni ndiyo basi tafuta Wataalam waandae Script, (kumbuka Script ndo Movie) mtu wa kwanza kabisa anayeiona Movie ni Script writer.

Kwa series wanaweza kuwa hata writers 5, 24 hrs imeandikwa na Script writers zaidi ya 7, na wote wamepita mule mule, Script writers lazima wawe na uwezo mkubwa, wenye muono wa mbali, elimu pia, Script ikikamilika mnakaa wadau kupendekeza Director, mtakua na vigezo vyenu all in all lazima awe na uzoefu na uwezo mkubwa, wapo Directors wachache wana uwezo ila Producers ndo wanaharibu!

Mkimpata Director atapitia Script atakuja na Mawazo au Mapungufu, mtayafanyia kazi mtaenda na hatua ya kuunda Crew, kumbuka Kila mtu Ana mipaka yake, Director ni kama vile Coach kwenye team ya mpira, yeye ataunda team yake kuona nani ataweza kumsaidia vizuri, assistance director, location manager, Continuity, n.k, atawaleta kwa Producers kwa makubaliano mengine hasa mkwanja! Ikipita mnaenda hatua inayofuta............

Ngoja niishie hapa ntarudi!
Ahsante sana mkuu nimevutiwa sana na maelezo yako upo vizuri sana hili ni darasa zuri sikutamani kumaliza kusoma

BTW lengo langu kubwa ni kufanya mabadiliko ya kuingiza utaalamu wa taaluma ya filamu katika movie zetu ambao kwa kweli haupo kabisa

Naomba endelea kutoa darasa hapa mimi nakupm muda huu!
 
Tukija upande wa kuandika story ambapo hapo ndo kutakua na mtihani upande Wako,
Waandishi tunasema Movie au Story ni Kisa, huitaji kukaa na Script writer kila siku kumwadithia Story ili aandike Movie, yeye atataka umpe Kisa Tu! Then yeye ataandika Script, sasa hapa mkuu, sijui umepanga kuandika story ya aina gani, manake kibongo bongo kama utawapa watu ambao sio Professional kuandika script kama ulivyosema 3, believe me kila mtu story yake itaenda lwake!

Kingine kuwalipa vizuri Wasanii, wakiamua kukukwamisha kama utawapunja pesa wanaweza na watakutia hasara, walipe muingie mikataba na muwe na mahusiaono mazuri, kumbuka series mtakua mna shoot hata baada ya miaka 3, msipokua na uhusiano mzuri wasanii watajitoa kuwakomoa, at the end mtaanza kuwaua watu kwenye story!

Naona niishie hapo, wengine wataendelea...
Je wewe mtoa mada Una uzoefu wowote na Movie???
 
Kwa ushaur tu anza kubuni story ila utangaze na maeneo ya national parks na vivutio vyote tulivo navo Tanzania itasaidia na hasa location iwe maeneo kama tanga au arusha aisee itakuwa poa.. Big up brother una wazo zuri
Umeshauri vizuri sana aisee.

TANAPA wameruhusu watanzania wowote wanaoweza ku shoot waende watawapa location hifadhini.

Akilishughulikia hili atakuwa ametusua sana aiseee
 
Kiukweli unaweza andaa story nzuri sana na ukawa na bajeti nzuri ila watakao kuangusha ni waigizaji.....bongo muvi 90 percent hakuna waigizaji makini,wapo wachache sana.
Wengi wao wanaigiza kuigiza thats why hawavutii kbs.
Najua utapata wakati mgumu sana kwenye kipande hiki.
Maoni yangu ni haya....kulingana na mazingira tunayoishi ningependekeza stori yako iwe na uhalisia means nature...unaweza tengeneza series inayomuhusu Chief Mkawa from the begin up to death.
Ukiangalia wenzetu wanazitumia series zao kujitangaza hasa tamaduni zao km wapi wametokea mpk walipo sasa ndo mana zinapendwa na kuvuka mipaka kwasababu zna upekee ukilinganisha na hizi za kuigiza tamaduni za watu.
Ngoja niishie hapa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom