Kuadimika kwa mafuta ya taa.

Mangandula

Senior Member
Nov 30, 2011
184
37
Kwa muda wa siku tano sasa mafuta ya taa yameadimika ukanda wa huku kwetu mikoa ya Iringa, Njombe, na Mbeya. Sijui na nyie wenzetu huko Dar mtindo ni huohuo? Wanasema mpaka jumanne! Jamani wanajamii tujadili hili suala kwa siye tulio vijijini bora ikosekane sukari lakini siyo mafuta ya taa! Je ni halali kukosa mafuta ya taa kwa wiki nzima? Tafakari.
 
Jamani wana jamvi tujadili kuadimika kwa mafuta ya taa huku kwetu! Mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya. Je na mikoa mingine yameadimika? Maana bora tukose sukari kuliko mafuta ya taa kwa sisi tulioko vijijini, tutafakari.
 
Hapa mkoa Singida ndo usiseme jana nimezunguka karbu sheri zote hamna kerosene,serekali vp?
 
Kuna njia mbadala ya mafuta ya taa kwa kutumia kwa mwangaza. Mojawapo ni kutumia taa kama hizi za solar za bei nafuu. Hizi zinakuwa badala ya kibatari. Kama kutahitajika mwanga zaidi kuna zingine za bei ya juu kidogo. Kwa maelezo zaidi tembelea hapa utaona taa za solar za Wakawaka.
 
Na jiko la mchina utatumia nini? Maana bila mafuta halifanyi kazi na mkaa bei juu. Twafwaa!
 
Back
Top Bottom