Kuacha na kuachwa

Unapowachwa au kuwacha ukiwa Ughaibuni ndio balaa kubwa, lakini kuwachwa au kuacha Bongo ni sawa na kupewa fursa nzuri ya kutafuta alie juu zaidi ya huyo aliyekuwacha au uliyemucha
 
Mwanaume ndiyo mwathirika kweli kwa kuachwa, ndiyo maana ili ajione yupo safe anakuwa na makoloni zaidi ya moja. Nayo anajikuta anaingia kwenye shida zaidi. Kuoa na kuwa na kimada kwa mwanaume anahisi ana-security kumbe ndo anazidisha balaaa.

Chukia kuachana. Labda iwe ni issue ambayo umeishindwa kabisa. Wapo wanaowaacha wenzao just coz eti kaona kitu kingine.

Wapo wanaume ambao wameecha wapenzi wao kwa madaha na kujigamba. Mbaya zaidi hajatofautiana kiasi cha kuamua kukumwaga.

SIKU NILIPOACHWA:
Niliamka siku ya Jumamosi kama kawaida yangu, ni siku ya kumtembelea boy friend ambaye kwa uelewa wangu tulikuwa wachumba, Kijana ambaye ndoto zangu ni kuja kuishi naye km mke na mme. Nilimtambulisha kwa ndugu, alitembelea nyumbani hata kama sipo, mama atamkaribisha kwa heshima zote.

Siku hiyo nilifika kwake, akanipokea vizuri tu, lakini nilihisi km ni mtu ana mambo mengi kichwani, sikujua nini kilimsumbua.
Mara akaniambia kuna kitu anataka anieleze. Nikaa kitako. Sikuamini alichonieleza, nilimsikiliza nikafikiri amechanganyikiwa, nilihisi kama nipo ulimwengu mwingine, nilihisi ninaota, kumbe ni kweli, aliyekuwa mbele yangu ni mpenzi wangi akinieleza kwamba hajisikii kunipenda tena.

Sababu mimi niongezeka uzito kidogo, nina mtindi mkubwa. Emempata potable, mzuri na presentable. Ananadika mbele za watu. Akatoa picha akanionyesha. Niliendelea kumsikiliza kwa makini huku nimeshikwa na butwaa. Akanyamaza, nikamuuliza umemaliza? akasema ndiyo, nikamwambia asante kwa kunieleza. Kwa masikitiko nikamuuliza kama anamaanisha na hayo anayoyesema, akajibu; ndiyo hivyo.

Nikanyanyuka na kuondoka kuelekea nyumba, kwa kweli nilijisikia miguu mizito sana, sikuwa na balance, kama niliyetaka kuanguka. Niliona nyota mbele yangu, Mungu alinisaidia nikafika nyumbani, nikaingia chumbani kutafakari sikupata majibu. Nikajiuliza nitawaambiaje ndugu zangu? sikuwa na jibu. Niliugua ndani ya moyo, mama aliniuliza kisa kinachonifanya nikae chumbani muda mwingi, sikuweza mwambia, nilidhani labda nikivuta subira my boy friend will come back. La hashaaah! siku zilianza kuyoyoma bila kisikia toka kwake. Nikajua kumbe nilichoambiwa ni kweli.

Nikamshukuru Mungu kwa kila jambo. Nikafunga ukurasa. Na kijana akaoa.

Kijana ndoa yake ilikuwa ngumu sana hata kufikia uamuzi wa kuachana na mkewe. Kijana akaanza kunitafuta ili turudiane, akisema kuwa huenda mimi ndiye ilikuwa chaguo la kweli. Kwa kweli sijarudi nyuma.
Hata sitaki kumwona huyu jamaa. Madonda aliyoyaweka moyoni mwangu Mungu ndiye anajua.

Namshukuru Mungu ninamaisha yangu mazuri sana, na nimeolewa.
 
Pole sana CMM kwa yaliyokukuta.

 
Last edited by a moderator:
Jaman kuna watu wanaakili kuliko kuwa clever. sijapost entry siku nyingi sana. nakuja hv:
kuachwa au kuacha, hiv vitu tujitahid kuvifanya kwa mazungumzo ya pamoja, kwan mwenzenu niliachwa halafu kwa mbwe mbwe kibao,, lakin baada ya muda wa miaka miwil familia ya aliyeniacha walipata shida na mkombozi ni mimi kutokana kaz ninayofanya. je nisaidien kabla sijawambia what i did. je ningefanyeje, nimsaidie kutatua shida ama niponde za kichwa?????????????????:angry::painkiller::yuck:

Ukimsaidia ndiyo itamfanya atambue zaidi umuhimu wako na itamfanya ajutie kitendo alichokufanyia, we mpe msaada kama unaweza halafu songesha mbele maisha yako. Ila zingatia kutoutumia huo msaaada kama njia ya kumrudisha kwako pia usioneshe dalili zozote za kumtaka tena. Hakika atajilaumu sana kukuacha, trust me.
 
Mi nadhani inategemea uliyemwacha alikuwa anakutreat vipi kama uliyemwacha alikuwa ni selfish wa mali zake kumuacha si unamdump kama matakataka tuu! loo kwangu itategemea mtu alikuwa ananitreat vipi unless otherwise nitamdump...by the way atatokea mwingine tuu atanitreat vizuri bana...
 
Back
Top Bottom