Kuacha na kuachwa! Ipi ni shughuli pevu

lijamaa limoja liliachwa na demu wake live live demu alikuwa anafagilia mapene jamaa ndio katoka univ demu anataka mashoping ya woolworths msela apeche aroro.....
.....basi jamaa kamkuta kiwanja shori wake na mshefa kamind akataka kubwia vidonge afe.....nikamwambia kunywa.....wala sikumkataza na wala sikuita ndugu zake....tangu siku ile kawa kama mie akiachwa anashukuru..ndio mwanzo wa kupata mashori wapaya wakali....

Belinda wewe umeshaacha wangapi?

Huyo rafiki yako lakini aliipata pata na haiwezi kumtoka hii japo maisha yanaendelea.

Bolded words: Sitaweza kukujibu sasa hivi na hapa jamvini,subiri nifikirie listi yote ya walioniacha/niliowaacha halafu nitakuPM na historia zao. Kuelezea najua sana,ushindwe wewe kusoma!
 
Zote ni shughuli, kwa kuwa mnaachana. Unapodhani unaacha kumbe unaachwa. Umefanyiwa vitimbi kusudi uache. Ukweli hakuna anayeacha wala anayeachwa. Mnaachana baada ya kuoana/kuwa pamoja.
 
HAPA NIMEPAPENDA!
ningependa kukupeni uzoefu wangu kwenye hii 'sustainable-impact'.lakini kabla ya kufikia huko ningependa MNIAMINI JAMANI.kuna impact moja inakuwa kama JINAMIZI!UNAKUTA HUNA AMANI.unasononeka,roho inakuuma

.........hatima ya yote utamtafuta na kumwomba msamaha,ili UPATE PEACE-OF MIND.

anaeachwa huwa anaumia mwanzoni(kama alipendalakini finally,ni kama maumivu huwa yanaisha.

ila anaeacha!........anafanya kwa kukomoa na anajiona kawini mwanzoni mwa picha(hasa kama alifanya ivo kwa ubabe wake tu).kama alipenda LAZIMA ATAUMIA SANA,kuna vitu vingi atavimiss sana.anaweza hata kujiingiza kwenye ulevi,au kuwa kicheche ILI APATE RELIEF

TRUST ME!hii kitu jamani muiangalie kwa three dimension mtajua tu

ni heri kuhifadhi
machozi yako kwa sababu aliyekuacha hathamini penzi lako ila kuna kuachwa kwingine
kunatokea kwa sababu sio nyie mmeamua ila
circumstaces ndio zimewafanya muachane hapo
lazima chozi likutoke yaani mmeachana ilhali
bado mnapendana,,,
 
Point taken, kote ni sawa tu but kuachana huku mnapendana kuna uma sana tu!
 
Anaeacha anakuwa tayari amejiandaa kwa hilo ila mshtuko ni kwa yule aliyeachwa anakua hajajiandaa kwa hilo.
 
Maumivu hutegemea sababu iliyopelekea kuachwa au kuacha ingawa kuna ile hali isiyo kuwa na sababu,hapo sidhani kama kuna maumivu.
 
kuachwa haipo chini yako ni maamuzi ya anayekuacha ila kuacha ndo kupo chini yako,ila kumwacha mtu anayekupenda ni kazi sana,analalamika sana hadi unakosa raha ya kuishi
 
kuachwa haipo chini yako ni maamuzi ya anayekuacha ila kuacha ndo kupo chini yako,ila kumwacha mtu anayekupenda ni kazi sana,analalamika sana hadi unakosa raha ya kuishi
You just need to take it easy. Kama mtu hanitaki kwa nini niumie wakati mapenzi hayalazimishwi?
 
Back
Top Bottom