Ktk suala la muungano watanganyika tumeachwa nyuma na wazenj.

Noti mpya tz

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
974
244
Pamoja na kwamba kuna vitu tunawaamulia wazanzibari lakini ktk kudai muungano uliosawa mametuacha, wana nchi yao na katba yao sisi Tanganyika haipo na hatujali. Tunalipa ushuru bidhaa za zenj wao halipi.
 
Pamoja na kwamba kuna vitu tunawaamulia wazanzibari lakini ktk kudai muungano uliosawa mametuacha, wana nchi yao na katba yao sisi Tanganyika haipo na hatujali. Tunalipa ushuru bidhaa za zenj wao halipi.

Hiýo ni ktka harakati za kula.Usipokubali kuliwa kidogo huli! Sasa we unakataka kula tu bila kuliwa? Haiwezekan
 
Segwanga, mbona umekimbilia suala la kula ambalo halihusiani na maada?
Penda kula sana veve segwanga.
 
pamoja na kwamba kuna vitu tunawaamulia wazanzibari lakini ktk kudai muungano uliosawa mametuacha, wana nchi yao na katba yao sisi tanganyika haipo na hatujali. Tunalipa ushuru bidhaa za zenj wao halipi.

sisi unajua ni bora liende tuuu!
Tunajua matatizo yapo ila tunamezea tuu!
 
Kelvito, inabidi tufike mahali tuamke tusiliache bora liende maana haliendi tunakotaka, na sasa kwa vile tumerudishiwa usukani basi tubadilishe mwelekeo.
 
Naunga mkono hoja'inabidi tujadili muungano na ss tanganyika tujue faida zake coz mpk sasa naona wazanziba wanapendelewa sana. Kwanza mbona hatuna wawakilishi wetu zanzibar?wabunge na mawaziri kama wao walivyo huku bara?
 
Pamoja na kwamba kuna vitu tunawaamulia wazanzibari lakini ktk kudai muungano uliosawa mametuacha, wana nchi yao na katba yao sisi Tanganyika haipo na hatujali. Tunalipa ushuru bidhaa za zenj wao halipi.
Tunalipa mara tatu,kwanza tunalipa kwa ZRA na TRA pale zanzibar,ukivusha tena KUJA Tanganyika/tanzania bara Tunalipishwa tena.
 
Ghibuu,
hicho ndicho ninachokisema mimi. zanzibar mtu wa bara huwezi hata kugombea ubalozi nyumba 10 ukashinda lakin wao wamejaa kwenye maofisi bard hadi uwaziri
 
Ghibuu,
hicho ndicho ninachokisema mimi. zanzibar mtu wa bara huwezi hata kugombea ubalozi nyumba 10 ukashinda lakin wao wamejaa kwenye maofisi bard hadi uwaziri

Hivyo nyinyi watanganyika hamujui kua Serekali ya Zanzibar si ya muungano? serekali ya muungano ni ya Tanzania!

Na ndio maana mukaona wazanzibari wanafanya kazi huko kwenu. Wazanzibari wameamua wawatafutie serekali yenu ya Tanganyika kwasababu mumeipoteza. Ikipatikana tanganyika Huko hatagusa Mzanzibari ajira zenu, Wazanzibari watabakia kwenye muungano tu na sio serekali ya Tanganyika.

Hivi sasa munaidhulumu Zanzibar kwakua bajeti Ya muungano munaitumia katika mambo yote ya Tanganyika Wakati Zanzibar Mambo yasiokua ya muungano inajitegemea wenyewe.

Hebu ndugu zangu niambieni wizara ipi isio ya muungano Tanganyika ambayo inajiendesha wenyewe bila ya mfuko wa muungano?.

Jibu kwa hoja usitoe fedhuli ili tuimarishe jukwaa letu.
 
Albimany, mi ni muumini wa uwepo wa taifa la tanganyika. shida yangu ni kwanini muungano uwe wa sehem moja? yaani mzanzibar kuajiriwa bara bila ubaguzi lakin mbara abaguliwe zenj.
 
Tatizo sio wazenji kama tunavozipablish,tatizo ni serikali yetu ambayo haitaki muungano ujadiliwe.Wazenji wanatuacha nyuma kwasababu wanaelimishana juu ya huu muungano na katiba yao.Ikiwa viongozi wana confuse watanganyika na kutuambia zanzibar sio nchi ni mkoa wakati ukifika siku za muungano tunasherehekea?Sasa hapa wananchi wanakuwa hawaelewi Zanzibar ni nchi au mkoa na hata wengine hawajui tofauti ya Unguja na Pemba.

Nadhani suala la kulipa kodi vilevile ni tatizo moja sugu lakini ni tatizo linatokea huku kwetu Tanganyika.Kwasababu hizo kodi zinazolipwa iwe ni mzanzibari au sisi watanganyika basi hizo hela zote zinaletwa Tanganyika.Kwahiyo hata kama ni mzanzibari analeta gari na kulishusha ZNZ na akalileta Tanganyika inambidi na yeye alipe mara mbili japo kuwa makusanyo ya kodi zote zinakuja Tanganyika.Na hili hata wazanzibari walilalamikia lakini hakuna anaelifuatilia.

Ni sisi wenyewe watanganyika tunatakiwa tutafute elimu ya kuhusu huu muungano pamoja na katiba yetu inasema nini kwasababu hatuijui na wala hatujui nini kinachotakiwa kubadilishwa na kwa misingi gani.Wazenji wameanza sikunyingi kulalamika na huu muungano lakini kumekuwa na hali ya kupublish habari za ukweli na uongo,lakini la muhimu ni kujifunza vizuri huu muungano na hizo kero zake kwa pande zote mbili ili kupata picha ya ukweli kuliko kujiuliza maswali ambayo hapa kila mtu atasema yake vile anavojisikia.
 
TANGANYIKA ITARUDI MUDA SI MREFU kwa utaratibu huu unaoendelea na watu kuzidi kujua kero za huu muungano ni dhahiri kuwa VIONGOZI WETU wataamka kutoka kwenye huu usingizi mzito wa kulewa sifa na kusahau kero za wale wanaowaongoza
 
Back
Top Bottom