ktk hili tigo wamefulia

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
Sijui ni kujiamini sana kwa kuwa na wateja wengi, sijui ni dharau, mtanisaidia,

Angalia, wanafungua saa 4 asb hasa mbagala, wakati wenzao saa moja,
vibanda viko vichache, barabara ya kilwa wako rangi tatu tu, barabara ya morogoro kuanzia ubungo viko vibanda vitatu tu, na cha mwisho kiko magomeni usarama kingine kiko mnazi mmoja.

yaani ni kero tupu na ukienda wale vijana hawana speed kabisa,

nashauri waongeze zaidi vibanda, km Muhimbili hakuna tigo, na sehemu nyingine kwenye mlundikano wa watu hakuna tigo ila zain wako kila sehemu.
 
Unalalamimika nini haswa?
Nini kinacho kukelekekata mkuu? Hivyo ni vibanda vya vocha au nn?
 
sehemu za kusajili line ndugu yangu, yaani tigo we acha tu ni kero kweli kweli, sasa imekuwa issue, yaani inatakiwa ufunge safari ya siku nzima kwa ajili kusajili tigo tu, kama ni kazini omba ruhusa ya siku mbili nzima maana siku ya kwanza ni ya kusajili na siku ya pili ni ya kupumzika ile kashi kashi unayoipata, ya kugombania foleni, na kusimama kwenye jua kali siku nzima.
 
Vyabure vinamambo sana kaka, we acha tu...! Ngoja tusake mahela tuingie mitandao ya ukweli you pay much and get much. Sio kunyanyasika kisa wako cheap.
 
Kama kuna mtumishi yeyote wa tigo humu JF ni vyema awe makini na sentensi hiyo hapo juu yenye bold na underline, vinginevyo watafulia kweli kweli maana watakaosajiliwa ni wachache,
 
Sijui ni kujiamini sana kwa kuwa na wateja wengi, sijui ni dharau, mtanisaidia,

Angalia, wanafungua saa 4 asb hasa mbagala, wakati wenzao saa moja,
vibanda viko vichache, barabara ya kilwa wako rangi tatu tu, barabara ya morogoro kuanzia ubungo viko vibanda vitatu tu, na cha mwisho kiko magomeni usarama kingine kiko mnazi mmoja.

yaani ni kero tupu na ukienda wale vijana hawana speed kabisa,

nashauri waongeze zaidi vibanda, km Muhimbili hakuna tigo, na sehemu nyingine kwenye mlundikano wa watu hakuna tigo ila zain wako kila sehemu.
???????????!!!!
 
sehemu za kusajili line ndugu yangu, yaani tigo we acha tu ni kero kweli kweli, sasa imekuwa issue, yaani inatakiwa ufunge safari ya siku nzima kwa ajili kusajili tigo tu, kama ni kazini omba ruhusa ya siku mbili nzima maana siku ya kwanza ni ya kusajili na siku ya pili ni ya kupumzika ile kashi kashi unayoipata, ya kugombania foleni, na kusimama kwenye jua kali siku nzima.

Unajua nashindwa kuelewa kwa nini muanze walalamikia tiGO muda huu wakati mlikuwa na muda wote wa kufanya usajili wa simu zenu kutoka July 2009 mpaka Desemba 2009 sasa inapokaribia mwisho ndio mnakaa na kulalamika. Nadhani mlitakiwa kujilaumu kwa kuchelewa kujisajili!
 
Suala sio hilo ila ni kwa nini voda, zain na zantel wameweka mawakala wengi kila kona ila wao hakuna, unafanya kuulizia tu wanakopatikana, na wakati mwingine unatoa pesa ili uelekezwe waliko,

wakati huu wa ushindani wa kibiashara hilo lina nafasi kweli?
 
Wewe siku zote hizo hujasajili ulikua wapi! Biashara asubuhi,,wakeUP
Any way kwa kukusaidia,,nenda Buguruni,,saa mbili kamili wanakua tayari,,usitake kutoroka kazini,,,
 
hii ni kero au education,science and tech ndugu yangu!!? Lakini kiukweli hata mimi wananikera kwa hilo,mpaka leo line yangu sijaisajili, sijawahi kukuta kibanda hakina foleni na muda wa kusubili unakuwa hamna!!
 
Leo nimeanza safari ya kusajiri line yangu, nimeanzia mnazi mmoja, foleni kali sana, nikaenda magomeni usarama hapo ndo usiseme, kiguu na njia hadi mwembe chai, nyomi kibao, sikukata tamaa hadi ubungo ukipita kwenye mataa unapinda kama unaenda chuo kikuu, na hapo watu wengi sana,

hata hivyo nikaamua kusubili hapo, nimekaa tangu saa 4.30 asubuhi, ilipofika saa 8.15 nikaamua kuhondoka bila kusajili line,

Tatizo, wanaweka vitoto havina kasi ya kuhandika, anaandika herufi moja moja kila baada ya dakika 5, mtu mmoja kummaliza ni saa nzima na kuna watu wengine wana line zaidi ya tano.

Ushauri, ni vyema wahusika waongeze sehemu za kusajilia, na pia wawaombe watu wenye uwezo wa kumudu hizi kazi vinginevyo muda utaisha na line zetu bado kusajili.
 
sehemu za kusajili line ndugu yangu, yaani tigo we acha tu ni kero kweli kweli, sasa imekuwa issue, yaani inatakiwa ufunge safari ya siku nzima kwa ajili kusajili tigo tu, kama ni kazini omba ruhusa ya siku mbili nzima maana siku ya kwanza ni ya kusajili na siku ya pili ni ya kupumzika ile kashi kashi unayoipata, ya kugombania foleni, na kusimama kwenye jua kali siku nzima.
ninyi waswahili mnapenda sana ku-front load mambo.hizi line walianza kusajili kabla ya mwezi wa sita.hadi leo mmekaa tu.mnajisababishia foleni bure finally mnalaumu!
 
Kwa hiyo wanatoa adhabu au??!!
 
Leo nimeanza safari ya kusajiri line yangu, nimeanzia mnazi mmoja, foleni kali sana, nikaenda magomeni usarama hapo ndo usiseme, kiguu na njia hadi mwembe chai, nyomi kibao, sikukata tamaa hadi ubungo ukipita kwenye mataa unapinda kama unaenda chuo kikuu, na hapo watu wengi sana,

Kaitaba usipoangalia utafika Morogoro
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom