Kova usijali, polisi ni wateja wetu!

eRRy

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
1,125
204
Wikiendi iliyopita, gazeti hili lilituma waandishi wake katika kona mbalimbali jijini Dar es Salaam ili kuona hali halisi ya biashara ya ukahaba, sambamba na kupokea nukuu za wanawake wanaofanya biashara hiyo.

Katika mzunguko huo, waandishi wetu walitembelea maeneo ya Oysterbay, Masaki, Upanga, Magomeni, Kariakoo, Buguruni, Temeke, Tandika, Kinondoni, Afrika Sana, Sinza na kuona taswira halisi. Picha halisi iliyoonekana ni kuwa biashara inazidi kukomaa na kwamba kadiri siku zinavyojongea ndivyo kasi ya wanawake wanaojisajili kwenye ‘ujasiriangono’ inavyoongezeka.

Uchunguzi wa Uwazi umebaini kuwa kulega kwa hatua za kisheria dhidi ya wanaojihusisha na biashara hiyo ndiyo zao la kuendelea kushamiri, hivyo kutia shaka jitihada za serikali kuukabili Ukimwi. Nukuu za machangudoa kuwa baadhi ya askari polisi ni wateja wao, ni kipimo kingine cha kuonesha kushindwa kwa jitihada za kuitokomeza biashara ya uchangudoa.

Machangu walioongea na gazeti hili wikiendi iliyopita, walisema kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova asijali wao kuendelea na biashara hiyo kwa sababu askari wake ni kati ya wateja wao wakuu. “Polisi wanatuchukua sana, wakati mwingine wanatuomba ofa nasi tunawahudumia ndiyo maana bado tupo. Jeshi haliwezi kutuondoa kwa sababu askari wake wanapata raha kutoka kwetu,” alisema mmoja wa machangu, aliyekutwa ameweka mitego, Oysterbay.

Kuhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, machangu hao walisema kuwa wao hawamuelewi na wanamshangaa kwa sababu hata afanye nini hawezi kufanikiwa.

“Wakuu wengi wa mkoa wakija hapa wanakuwa wakali, lakini mwisho huwa wanatulia. Mimi nina mwaka wa 12 nipo kwenye biashara hii, utaona kwamba nilikuwepo tangu enzi za Mkapa akiwa madarakani,” alisema dada mmoja aliyekutwa ametega Kinondoni, jirani na Makaburini, Dar.

Changu huyo aliendelea kusema: “Utaona ni kiasi gani nilivyo na uzoefu, polisi wanaondoka wanakuja wengine wapya, tunawapokea wakija kwetu tunawahudumia, wanakuwa washikaji wetu, wakati wa misako wanatutonya nasi tunachukua tahadhari. “Sasa hivi Rais ni JK mimi nipo, leo hii Mkuu wa Mkoa ni Lukuvi, lakini tulikuwepo tangu Makamba na hata Abbas Kandoro alikuja na kutuacha.”

Mrembo mwingine alisema kuwa si rahisi kwa polisi kuamua kwa dhati kuwatokomeza kwa sababu kama baadhi yao ni wateja wakuu, wanaelewa thamani na faida yao. “Hivi wewe ukitumwa umkamate mkeo utakubali? Kwa vile polisi wanafahamu faida zetu hawawezi kutuondoa moja kwa moja.

“Wanatufaidi sana, wakati mwingine kwa hela ila mara nyingi ni bure kwa sababu huwa wanatuambia wao ndiyo wanaotulinda ili tuendelee kufanya biashara,” alisema mrembo mmoja, aliyekutwa ametega Kariakoo, Barabara ya Uhuru.

Wakati ikizungumzwa hivyo, imebainika kuwa jitihada za polisi zinaweza kuwaondosha machangudoa na wasionekane Dar na hata mikoa mingine.

Uchunguzi wa gazeti hili eneo la Buguruni, umebaini kuwa kwa kiasi kikubwa biashara hiyo imedhibitiwa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na sasa, makahaba wanaonekana mmoja mmoja tena kwa kuiba.

Hapo kabla, Buguruni ilibatizwa jina la Kijiji cha Ngono, ikielezwa kuwa ufuska unafanyika waziwazi, machangudoa wakiwa wametanda, tena wakiwa huru, wakati mitego yao huiweka jirani kabisa na Kituo cha Polisi.

Inaelezwa kuwa mafanikio ya kuwaondosha machangudoa hao, yamekuja baada ya hivi karibuni polisi mmoja kushambuliwa na watu wanaotajwa kuwa ni wahuni, hivyo askari kudumisha doria.

Hatua hiyo ya polisi kudumisha doria, huku kukiwa na mkazo wa viongozi wenye nyota zao, imeleta mafanikio makubwa kwamba si tu kutokomeza wahuni na vibaka, bali pia kuwapa kashkashi machangu ambao kwa sasa wameingia mitini.

Kutokana na picha ilivyo Buguruni kwa sasa, Uwazi limegundua kuwa kumbe ni kazi rahisi kwa polisi kuutokomeza ukahaba Dar, ila mkazo ndiyo bado ni tatizo. Kamanda Kova, alishatoa tamko kuwa atatumia nguvu zake za kijeshi kumaliza uchangudoa Dar.

1256017862_uwazifront.jpg


Source: http://www.globalpublisherstz.com/2009/10/20/kova_usijali_polisi_ni_wateja_wetu.html
 
Tatizo ni sisi tunaonunua hii commodity, tususie basi halafu tuone, au ndo tutagongewa milango majumbani kama machinga wauzavyo bidhaa zao?
 
Tujitahidi kuwahifadhi hawa dada zetu wasiadhilike mabarabarani.

Jamani tuwaoe wawili, watatu au wanne na kama tutachelea kufanya insafu basi tuoe mmoja.

Tuhamasishane kuwaoa.
 
Tujitahidi kuwahifadhi hawa dada zetu wasiadhilike mabarabarani.

Jamani tuwaoe wawili, watatu au wanne na kama tutachelea kufanya insafu basi tuoe mmoja.

Tuhamasishane kuwaoa.

hahaaa mkuu Barubaru wazo zuri sana hili.ningekuwa mbunge ningepeleka muswada binafsi kunako bunge
 
Back
Top Bottom