Kova: Maandamano ya DOWANS kesho marufuku!

Alishindwa vipi kutumia intelleligencia yake kujua kwamba DOWANS ni wezi hapo mwanzo?
 
Duh kamanda katoa kali ya mwaka! Hivi ndivyo jinsi viongozi wetu wana loose credibility.Jesus! 'Facts' stranger than fiction. Sasa hapa la msingi ni kususa game uwanja wa taifa hadi hapo kamanda atahakisha usalama wetu maadam mkusanyiko pale utakuwa mkubwa pia.
 
Kova ajiandae al shabaaab wakifanya kweli. Siombei, lakini ikitokea atafute pa kujificha.
Huyu mpuuzi anafkiria al shabaab wanahitaji watu laki tano kupiga bomu, yapo matukio ambayo watu chini ya 10 wamepigwa bomu na al shabaab. So kama lengo lake ni kutuokoa atukodie na tax ili tuachane na dala dala mana ndani ya dala dala tunakuaga zaid ya 50.

Haya mazee yenye akili finyu sijui tumetoka nayo wapi. Kwa mawazo yake anadhani kwa kusema hivyo watanzania watamuelewa na bosi wake anamwona huyu ni intelligent kwa upuuzi kama huu. Ama kweli ni shida kutawaliwa na vilaza.
 
Unapokataza watu kuandamana kisa Al-Shaabab ni ishara tosha kwanza hao jamaa wapo hapa nchini.

Pili huo uwepo wao ni kwamba polisi imeshindwa kuwazuia wasiingie nchini,

Tatu wameshaingia, pia umeshindwa kuwazuia wasilete madhara.

Mikusanyiko iko mingi tu, si lazima iwe Maandamano ya Dowans.

Mbona wakati wa Kampeni za Siasa hawazungumzii Al Shaabab? Kwenye masoko makuu ya Nafaka kama Tandale, Urafiki, Tandika, Kariakoo kote huko mbona hawazngumzii hao Al Shaabab?

Ubungo Bus Terminal, Mwenge, Mbagala kote huko kuna mikusanyiko mikubwa ya watu, hao Alshaabab hawawezi kufika?

Jumamosi inayokuja kuna Mechi kati ya Simba na Yanga ambapo takriban watu Alfu 50 au zaidi wanategemewa kuingia, hakuna uwezekano wa hao Alshaabab kuwepo?

Yani hao Alshaabab wapo kwenye maandamano ya Dowans tu??!!!!

Kwanza kama kweli wapo, hao Alshaabab wakitaka hata hiyo mikusanyiko yao ya miaka 50 ya uhuru wa bendera watailipua tu.

Napata mashaka na uwezo wa huyu Mzee, kwani amekua mtu wa majigambo mengi kuliko uhalisia wa kitu.
Me Love Your comment. KAMA KWELI KUNA TISHIO LA AL SHABABU WAZUIE MIKUSANYIKO YOOTE HAPA DAR, KARIAKOO IFUNGWE KESHO, MECHI ZA SOKA ZIFUTWE, VYUONI NA MASHULENI PIA WASIENDE KWA KUWA TISHIO LA L SHABABU LIMEKUWA KUBWA. yaani hii nchi sijui usanii utaisha lini?? Ikibidi tutaandama hivyo hivyo mtupige mabomu na risasi muwasingizie alshababu.
 
Hili tishio la dowans hajawahi kuliona hata kidogo?
Mkuu, atalionaje na yeye hatumii akili yake! Hiyo amri ya kukataza maandamano sio yake, niya Rostam Azizi kupitia makuadi wake walioko serikalini. Kova yeye ni kipaza sauti tu.
 
Nilitaka kutukana lakini nadhani Kova anatumika tu na kwa bahati mbaya hataweza kuliona tusi hili, lakini namwombea yeye na aliyemtuma miaka 50 ya mateso kwa kuzuia haki ya kiraia kupinga mambo ya hovyo yanayofanywa na majangili yanayojiita serikali,,,, hawa ni wabaya zaidi kuliko Al Shaabab anaowaogopa Kova, maamuzi ya kishe-nzi wanayofanya ndiyo yanayotengeneza Al Shaabab tofauti itakuwa ni majina
 
Kama kutuua watuue tu, Hawajaanza leo. Kesho mi niko barabarani kama kawa!!
 
NAITISHA MAANDAMANO YA KUGOMEA MECHI YA SIMBA NA YANGA KUPINGA KUZUIWA KWA MAANDAMANO YA KUPINGA DOWANS.....

Hizi double standards hatuzitaki...

Tusiende kwenye mechi ya Simba na Yanga kama protest ya kunyimwa haki yetu ya kuandamana!
 
Hakuna umuhimu wa maandamano, mahakama imeshatoa hukumu ya mwisho. Bora ameyazuia.
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....

watazuia kila kitu,watamzuia kila mtu lakini hawata zuia upanga wa Mungu.na hasira yake.Kova jiandaeni
 
Suala la Dowans liko mahakamani na ni suala la kisheria sio mihemko.Wanaharakati wameishakula hela ya ma-donors wao kwa ajiri ya hayo maandamano ya kuwapotezea watu muda wao wa kujenga taifa.tusitumike kuwa daraja la mafanikio ya wengine.serikal imekata rufaa tena sasa unamuandamania nani kama sio wehu.
wehu ni wale wanaokiuka katiba ya nchi
 
Sasa kama wana wasiwasi na Al Shabab, kazi ya polizi na JWTZ ni nini? Wenyewe wanatakiwa kuweka ulinzi na kuhakikisha wananchi wako salama na si hizi habari za Mwanasesere.

Inafika wakati ufike kwa watu wazima tena wenye dhamana serikalini waache kuongopea watu wazima wenzao.

Hizi stori hata ukipeleka shule ya chekechea ya Mwl J. K. Nyerere Kinondoni wanafunzi watabaki wanakucheka tu.
 
Namfananisha kova na wanasiasa wanaohubhri udimi..yeye anahubiri al shabaab,kwan hao al shabaab hawafai hata kutajwa midomon mwetu
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....

Acha kuzunguka. Sema MAGAMBA (CCM) Wamemwagiza Kova kuwa toilet paper. Lakini waubiri siku ipo, yaja. Hao wanaojulikana tutawachinja siku nchi ikikombolewa toka mikononi mwa mafisadi.
 
Nadhani sasa kila member humu atume message at least kwa watu kumi wasiende uwanjani mechi ya Simba na Yanga jumamosi maana Al-Shabab watashambulia. Pia wanafunzi wasiende mavyuoni na mashuleni, kusiwe na mikusanyiko yeyote maana hao jamaa watatushambulia!!!
 
Back
Top Bottom