Kova: Maandamano ya DOWANS kesho marufuku!

Serikali yetu ni mchoko kabisa. Yaani kila siku kodi zinakusanywa kulipa jeshi lakini yanakaa kaa kulea viambi badala ya kutimiza wajibu wao. Inakuwaje mharifu anaingia nchini, walinzi mnafanya nini?
 
kova hana uwezo wa kuwazuia kuandamana. waendelee na maandamano yao...labda intelijensia imewaambia huo ndo utakuwa mwanzo wa mwisho wa dola ya ccm...
kwenye nyeusi hapo...hii ndio sababu kubwa....we fikiria hayo mashere hayo ya miaka 50 kila wizara alshabaab wakiamua kuua hawawez? ni mpaka kwenye mkusanyiko wa maandamano?

Club ngapi Dar hapo huwa zinakesha na watu kibao? alshabaab hawawezi kuua huko? hayo mafoleni yasiyo na tija barabarani alshabaab wakiamua kurusha gurunet hawawezi kuua?
 
wazuie sasa hata pambano la simba na yanga maana mle uwanjani ikirushwa gurunet moja wengi watakuga kwa kukanyakagana...mwambien asitishe na mechi hiyo
 
Tunamtaka Kova pia apige maruku match ya Jumamosi kati ya Simba vs Yanga kwa sababu ya tishio la ugaidi wa Al-Shabaab. Vinginevyo hiyo intelegensia yake itakuwa ni kiini macho, ukichukulia most recent incidence ya huko Uganda Al-Shabaab huwa wanapenda kushambulia mikusanyiko ya mashabiki wa mpira.

Kova kazi kwako piga marufuku match ya watani wa jadi kama kweli una credible information ya tishio la Al-Shabaab!
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....

Ukiona hivyo jua polisi wanatumika kisiasa,kuficha maovu yao na ikiendelea hivi sisi wananchi tutaanza kudill na hawa polisi sababu tunaishi nao mitaani kwetu.
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....

hivi maandamano ni kesho?n0t jumam0si?
 
sasa ndiyo nimeelewa kumbe dowansi ni ya al shabaab, ndiyo maana walikuwa hawaonekani hazarani kudai pesa zao na wakaamua kumtumwa mwakilishi wao.
 
Tatizo hawa maitelijensia wetu wanafikiria kwa masaburi! Vitu vya muhimu kwa Taifa kwao havina umuhimu...

Muhimu kwa nchi hii ni MAANDAMANO?.Afadhali yazuiliwe maana hata serikali yetu tukufu imekata rufaa,sasa maandamano ya nini kama sio kihelehele.
 
.....intelejesia ya kabichwa kangu inaniambia 'yawezekana sirikali yenyewe ikaamua kuwauwa watu ''wake'' kwa kisingizio cha Al shabaab'
Nataka kuiamini itelejesia ya kabichwa kwangu sababu yeyote au kundi lolote linalopingana na sirikali adhabu yao ni risasi. Nadhani sasa itakuwa bomu au mabomu....
Viongozi kuweni na huruma, leo kwetu kesho kwenu.
 
Muhimu kwa nchi hii ni MAANDAMANO?.Afadhali yazuiliwe maana hata serikali yetu tukufu imekata rufaa,sasa maandamano ya nini kama sio kihelehele.

.....teh! teh! Kwenye mahakama ya 'kichina', wajifunge wao kwenye mkataba, waseme wamekataa rufaa. Dhamira yao tangu awali ni kuilipa 'dowance'.
Kukata rufaa!!
 
Muhimu kwa nchi hii ni MAANDAMANO?.Afadhali yazuiliwe maana hata serikali yetu tukufu imekata rufaa,sasa maandamano ya nini kama sio kihelehele.
Freedom of expression. Tanzania una uhuru wa kuwa kiherehere. Miaka 50 mnayoipigia debe ni ya nini?
 
Unapokataza watu kuandamana kisa Al-Shaabab ni ishara tosha kwanza hao jamaa wapo hapa nchini.

Pili huo uwepo wao ni kwamba polisi imeshindwa kuwazuia wasiingie nchini,

Tatu wameshaingia, pia umeshindwa kuwazuia wasilete madhara.

Mikusanyiko iko mingi tu, si lazima iwe Maandamano ya Dowans.

Mbona wakati wa Kampeni za Siasa hawazungumzii Al Shaabab? Kwenye masoko makuu ya Nafaka kama Tandale, Urafiki, Tandika, Kariakoo kote huko mbona hawazngumzii hao Al Shaabab?

Ubungo Bus Terminal, Mwenge, Mbagala kote huko kuna mikusanyiko mikubwa ya watu, hao Alshaabab hawawezi kufika?

Jumamosi inayokuja kuna Mechi kati ya Simba na Yanga ambapo takriban watu Alfu 50 au zaidi wanategemewa kuingia, hakuna uwezekano wa hao Alshaabab kuwepo?

Yani hao Alshaabab wapo kwenye maandamano ya Dowans tu??!!!!

Kwanza kama kweli wapo, hao Alshaabab wakitaka hata hiyo mikusanyiko yao ya miaka 50 ya uhuru wa bendera watailipua tu.

Napata mashaka na uwezo wa huyu Mzee, kwani amekua mtu wa majigambo mengi kuliko uhalisia wa kitu.
 
Tafadhali LCHR, nyie ndo waandalizi wa maandamano haya. Toeni taarifa hapa. Kama maandamano yapo au hayapo...nini msimamo wenu. Siye tupo tayari
 
Jeshi la Polisi liko mifukoni mwa mafisadi.Yamkini Kova ni wakala kamili wa mafisadi kama jeshi zima polisi lilivyo wakala wa mafisadi.
 
Aache ushamba. Al Shabaab wanahusikaje na maandamano ya amani?
 
Al shaababu ni kundi la kigaidi la kimataifa, kova ni mtu mdogo na wa chini sana kudili na ishu ya alshababu, nahodha au Jwtz ndio watueleze. Kova hapa anaonesha usaliti wa waziwazi kwa watanzania.
 
Foolish! Kwa nini hakutoa tahadhari ya watu kutokukusanyhka? Tunafahamu kuwa magaidi wanatageti sehemu zenye watu wengi ikiwemo sokoni, shuleni, stendi nk kwanni hajatutaarifu mapema ili tujihadhari sio kwenye maandamano tu? Huu ni usongombwingo.
 
Suala la Dowans liko mahakamani na ni suala la kisheria sio mihemko.Wanaharakati wameishakula hela ya ma-donors wao kwa ajiri ya hayo maandamano ya kuwapotezea watu muda wao wa kujenga taifa.tusitumike kuwa daraja la mafanikio ya wengine.serikal imekata rufaa tena sasa unamuandamania nani kama sio wehu.
 
Back
Top Bottom