Kova kung'olewa kutoka wadhifa wake baada ya kuiabisha serikali ya CCM

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Kufuatana na kuidhalilisha serikali nzima ya CCM kuhusu tamko lake kwa umma kuhusu 'kutubu' kwa yule Mkenya kuna uwezekano mkubwa Kova akaondolewa katika wadhifa alionao sasa hivi.

Tetesi zinasema kuwa serikali haimuamini tena kamanda huyo kwani anaweza tena akaitia aibu serikali hasa katika siasa hizi za kutafutana baina ya wanasiasa na vita kubwa iliyopo baina ya CCM na upinzani.
 
Pale awekwe Godfrey Nzowa ndo anapaweza.nadhani mnamkumbuka alivokuwa RCO ARUSHA NA SASA MADAWA KILWA ROAD
 
Mida hii hang'olewi mtu ! Kwani hakuna umuhimu ni utawala wa mwenye nguvu mpishe.
 
Hii story umeipika Kama ccm wanavyopika habari zao nafikiri utakuwa umegraduate juzi kutoka kile chuo cha propaganda cha ccm
 
Pale awekwe Godfrey Nzowa ndo anapaweza.nadhani mnamkumbuka alivokuwa RCO ARUSHA NA SASA MADAWA KILWA ROAD

Mkuu huyo hana uzoefu na msitu wa pande! kuliko kumweka huyo wako tayari kumweka Abdallah Zombe!
 
cOMMENT NA THREADS ZA Mwiba zimeshuka thamani sana!
Enzi nikiwa ndio najiunga JF alikuwa mtu mwenye busara za ajabu, na ni mmoja wa watu walionivutia!
U never know with age!(refer thread ya leo inayohusu Hirizi)
 
Last edited by a moderator:
Kumuua nyoka sebuleni ni shida sana, akitolewa tu ntafaidi uozo wa CCM wote tangu madawa ya kulevya na matukio kama la Mwakyembe na wengine....
 
Pale awekwe Godfrey Nzowa ndo anapaweza.nadhani mnamkumbuka alivokuwa RCO ARUSHA NA SASA MADAWA KILWA ROAD

umesahau Kova alivyowachuna ngozi wale wachunaji ngozi kule Mbeya? mwache ang'ang'anie tu hapohapo
time will tell
 
Wooote hamjui kusoma alama za nyakati......Hemedi Msangi ndio anaandaliwa kushika mikoba ya Kamanda wa polisi kanda maalum...kwa uadilifu wake ulitukuka..
 
Nzoka ndio anastali kupewa hiyo nafasi ya kova kwani anakubalika kwenye ule mtandao wa wale vijana wanaopatiwa mafunzo ya kareti na kurushia mawe mikutano ya wapinzani
 
Hata wakimuweka nani utakuwa ni uwendawazimu tu mpaka pale watakapoacha vyombo hivi kufanya kazi zake kwa uhuru na si kuvitumia kisiasa na vingine kuvigeuza kama vichaka vyao kujificha ili makosa yao yasifahamike
 
Back
Top Bottom