Kova achunguzwe, gorofa analojenga Ilala pesa alipata wapi?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
huyu kamanda wa Polisi wa kanda Maalum Dsm naye ni fisadi tu. Anaporomosha gorofa pale Ilala makutano ya Pangani na Morogoro Streets karibu na Mahakama ya Mwanzo.

Tetesi zilizowahi kuzagaa ni kwamba alipata pesa nyingi akiwa Mbeya alipokuwa akiruhusu mihadarati kupitishwa na hata kutuma askari kusindikiza au kupokea magari yaliyobeba sheheni hiyo.

Hilo gorofa inasemekana ni la shemeji yake, wengine wanasema ni swahiba tu aitwaye Issa, au maarufu Mister Kep. Wote hawa kwao Kondoa.

Hivyo ili aendelee kula matunda juu ya migongo ya Watanzania masikini, serikali inamuach tu, kwani analipa fadhila kwa kufunika madudu mengi tu ya wakubwa hapa jijini, zikiwemo kashfa zao za ngono, za traffic accidents na hata za mauaji.

Nyingine ni kama hii ya sasa ya Dr Ulimboka -- ni lazime aitetee serikali na timu ya uchunguzi aliosema ameunda kuchunguza itakuwa ni ya magumashi tu.
 
Kwikwi kwi hizi ndo habari auwiiiiii hebu tupia picha aiseee kapata wapi pesa tumfanyie calculation kutokana na anachokipata na ujenzi wa ghorofa hy,kapata wapi hela za kununua kiwanja hicho ambacho ni zaidi ya Ml 500?????
 
Hivi kwanini watu wenye tittle serikalini wakifanya kitu huwa tuna link na ufisadi? ni kweli kuna ambao kweli ni mafisadi lakini kuna ambao sio. Tatizo tumekuwa nchi ya kijamaa muda mrefu na tumesahau kwamba siku hizi mtu unaweza chukua mkopo pia na kufanya biashara huku unafanya kazi. Kama ni suala la ufisadi hata humu JF jamaa wakishuka na kufanyia uchunguzi utakuta mafisadi ni wengi, hata kama umejenga chumba na sebule kwa milioni 6 lakini wakilinganisha na kipato chako na muda uliokaa kazini unaweza kuwa ni fisadi. Ufisadi sio kwa viongozi tu hata huku uswahilini. Mtoa mada nadhani bado ana fikra kwamba unapokuwa mfanyakazi unatakiwa huishi maisha flani hivi.
 
huyu kamanda wa Polisi wa kanda Maalum Dsm naye ni fisadi tu. Anaporomosha gorofa pale Ilala makutano ya Pangani na Morogoro Streets karibu na Mahakama ya Mwanzo.

Tetesi zilizowahi kuzagaa ni kwamba alipata pesa nyingi akiwa Mbeya alipokuwa akiruhusu mihadarati kupitishwa na hata kutuma askari kusindikiza au kupokea magari yaliyobeba sheheni hiyo.

Hilo gorofa inasemekana ni la shemeji yake, wengine wanasema ni swahiba tu aitwaye Issa, au maarufu Mister Kep. Wote hawa kwao Kondoa.

Hivyo ili aendelee kula matunda juu ya migongo ya Watanzania masikini, serikali inamuach tu, kwani analipa fadhila kwa kufunika madudu mengi tu ya wakubwa hapa jijini, zikiwemo kashfa zao za ngono, za traffic accidents na hata za mauaji.

Nyingine ni kama hii ya sasa ya Dr Ulimboka -- ni lazime aitetee serikali na timu ya uchunguzi aliosema ameunda kuchunguza itakuwa ni ya magumashi tu.

Mkuu ebu jipange vizuri tukuelewe..
 
Hivi kwanini watu wenye tittle serikalini wakifanya kitu huwa tuna link na ufisadi? ni kweli kuna ambao kweli ni mafisadi lakini kuna ambao sio. Tatizo tumekuwa nchi ya kijamaa muda mrefu na tumesahau kwamba siku hizi mtu unaweza chukua mkopo pia na kufanya biashara huku unafanya kazi. Kama ni suala la ufisadi hata humu JF jamaa wakishuka na kufanyia uchunguzi utakuta mafisadi ni wengi, hata kama umejenga chumba na sebule kwa milioni 6 lakini wakilinganisha na kipato chako na muda uliokaa kazini unaweza kuwa ni fisadi. Ufisadi sio kwa viongozi tu hata huku uswahilini. Mtoa mada nadhani bado ana fikra kwamba unapokuwa mfanyakazi unatakiwa huishi maisha flani hivi.
Kwa hiyo unahalalisha ufisadi sio kwa kuwa hata humu wamo?? Hii nchi machizi mko wengi sana. Kwa mshahara wa polisi jinsi ulivyo Kova hajafikisha hata mshahara wa 2M, leo utudanganye anakopesheka kwa 500M unatuona wajinga eeeh. Tunaelewa ili ukopesheke lazima uwe na collaterals na uwezo wa kulipa sio tu kila mtu anakopesheka na kwa bongo cheo cha kova hakimfanyi apate mkopo zaidi ya hutu tumikopo tudogo twa up to 20M. Ingekuwa nchi hii inafuatA utawala wa sheria tungemchunguza Kova na kuangalia kodi anazolipa TRA kwa mwaka na kuhusisha na kipato chake na jengo. Kila kipato halali kinatakiwa kuendana na kodi halali. But CCM hawafanyi hivyo kulinda mfumo fisadi wanaonufaika nao
 
nadhani hoja isiwe kuwa anajenga ghorofa hoja iwe kama amepata fedha kwa njia chafu. Inamaana mtu akiba halafu akawa mwendo wa lager hatoshitakiwa kwa vile hakuna kinachoonekana?
 
Kwa hiyo unahalalisha ufisadi sio kwa kuwa hata humu wamo?? Hii nchi machizi mko wengi sana. Kwa mshahara wa polisi jinsi ulivyo Kova hajafikisha hata mshahara wa 2M, leo utudanganye anakopesheka kwa 500M unatuona wajinga eeeh. Tunaelewa ili ukopesheke lazima uwe na collaterals na uwezo wa kulipa sio tu kila mtu anakopesheka na kwa bongo cheo cha kova hakimfanyi apate mkopo zaidi ya hutu tumikopo tudogo twa up to 20M. Ingekuwa nchi hii inafuatA utawala wa sheria tungemchunguza Kova na kuangalia kodi anazolipa TRA kwa mwaka na kuhusisha na kipato chake na jengo. Kila kipato halali kinatakiwa kuendana na kodi halali. But CCM hawafanyi hivyo kulinda mfumo fisadi wanaonufaika nao

Asante kwa kuniita chizi ila lengo la hoja yangu ilikuwa kubadili mtazamo nguvu ya kupiga ufisadi isiishie kwa viongozi wa juu tu hata huku mtaani kuna watu wa kawaida wanakula bata kwa fedha chafu na jamii kubwa inaona kawaida tena akipita mtaani jamaa yupo safi kuna deal alipiga ila kuna group la watu wakifanya ndio tunawaona wao ndio mafisadi. Inaeleweka ili ukope unahitaji collateral lakini hoja yangu hapa ni kwamba mtu anaweza kuchukua mkopo akafanya biashara ili kukuza kipato then baadae anafanya mambo makubwa lakini sijasema mkopo achukue ajenge mjengo kama huo mdau na ndio maana nikataja na umri wa mtu katika utumishi wake. HOJA HAPA HATA HAO VIONGOZI AMBAO NI MAFISADI KABLA YA KUWA VIONGOZI WALITOKA HUKU TULIPO NA KAMA NDIO TULIWALEA HIVYO JUHUDI ZA KUKEMEA PANDE ZOTE ZIFANYIKE JAPO HUWEZI KUONDOA KABISA. Usiumie kwa kumwita mwenzako chizi wakati sifa ya binadamu ni kutofautiana hoja na ndio maana tunafanya mikutano pia tunakutana humu JF kwani hoja ya mtu hata kama ina mapungufu kuna mwingine anaweza akapata point ya kuboresha (ndio maana tupo humu JF)
 
Back
Top Bottom