Kosa letu ni kuwapa kura za kula kiasi cha kuvimbiwa na kutusahau wanyonge.

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Imekuwa ni jambo la kawaida kabisa kila serikali inapopitisha bajeti zake huwakandamiza wananchi.Hakuna siku bajeti ya serikali iliwalenga walalahoi katika kuwakomboa kutokana na uduni wa maisha. Mbaya zaidi hata kauli mbiu zao wanapo zitowa wakati wa kampeni hushindwa kutekelezeka na kukithiri kwa uchotaji wa pesa za umma unao fanywa na watendaji wa serikali ambao tuliwaamini lakini wametugeuka.

Huduma muhimu za kijamii hupandishwa kodi zake kiasi cha kupelekea hali ngumu inayowakumba wanyonge. Kwanini basi wananchi tunashindwa kujitambua na kuamua kuwaadabisha watawala wazembe na dhaifu waliotufikisha hapa,bila kujali wakati.Nasema bila wakati kwa sababu kila tunapo wapa wakati wanazidi kuipora nchi yetu bila huruma.Hakuna cha mtoto wa mkulima wala wa mvuvi kila nayekaa kwenye kiti cha enzi ana athiriwa na mfumo dume usio na tija katika kuliendeleza taifa.

Leo bajeti ya ofisi ya waziri mkuu itapitishwa na wawakilishi wetu wale wale walioapa hawatatutupa lakini wakiwa ndani ya mjengo hujisahau na kuchumia matumbo yao kwa kura zao za ndiyo bila kujali ndiyo hiyo ina maslahi na umma uliowaweka pale mjengoni. Tumeona bajeti ya afya ya Watanzania isivyokidhi mahitaji halisia lakini utasikia ndiyoooooooo.

Ifike mahali kura yetu isiwe kura ya kula,bali ilete maendeleo ikiwa ni sambamba na kuwahoji wabunge wetu kama tuliwatuma kuwa mabwana na mabibi ndiyo.Tunataka bunge lenye uwezo wa kuhoji serikali kutokana na mwenendo wake mbovu wa matumizi ya pesa za umma na kukithiri kwa uwizi usio kubalika mbele ya umma kwa sapoti ya wabunge wetu.

Mwisho,nasiktika bajeti hii ya waziri mkuu itapitishwa na wabunge wetu vihiyo bila kujali kama inamgusa mlalahoi wakati hii ni nchi yetu sote.Mungu tubariki Watanzania tuweze kujikomboa na kujitambua kila tunapopata fursa ya maamuzi tuitumie ipasavyo kwa kutafakari hatima ya maisha yetu yajayo.Ameen
 
Back
Top Bottom