KOSA LA PILI LA Mtanzania ni kudhani lazima CHADEMA Itukomboe

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,452
3,065
Ni kweli kosa letu la kwanza ni kuiamini CCM hata baadhi yetu kutumika vibaya kuilinda pale ambapo ilipaswa kuanguka kifo cha mende. CCM ilipaswa iondoke enzi za NCCR, Ikapaswa iondoke kwa mara nyingine enzi za CUF, sasa inapaswa iondoke ktk enzi za CHADEMA. Tunaweza kushindwa tena kufanya hivyo, CHADEMA pia inaweza kushindwa kufanya hivyo kutokana na kuaminiwa sana na Wananchi kama ilivyowahi kuaminiwa NCCR na CUF.

Kosa la pili ni kudhani ni lazima CHADEMA waiondoe CCM, hapana. Sio kazi ya CHADEMA kuiondoa CCM, ndo maana kila nikisia CCM inapigana na CHADEMA, najua sasa kweli CCM inaondoka, yaani mfa maji hutapata kwa silokuwepo.

Suala la CCM kuondoka liko mikononi mwa wananchi, suala la CHADEMA kupewa nchi liko mikononi mwa wananchi wale wale watakao inyima kiti CCM waipe CHADEMA Ukumbi.

Ikifikia wakati CHADEMA wakawa na jukumu la kuondoa CCM , hakika hawataweza maana jukumu hilo ni la wananchi; Tusifanye makosa hayo kwa mara ya pili. CHADEMA watatuongoza pale tu ambapo tuwawapa ridhaa hiyo tuliyowanyanganya CCM, na wajue kuwa tunaweza kuwanyanganya vilevile na kuwapa NCCR au TLP iwapo hawatafanya yale tuliyokusudia.

UKOMBOZI NI WATU na WATU NDO WATANZANIA WENYEWE SIO CHAMA NA WANACHAMA WAKE

Kama chama chochote cha upinzani kinataka ridhaa hiyo kutoka kwa wananchi, kijishughulishe na matatizo ya wananchi orodha ni ndefu sana na inajulikana. CHADEMA kwa sasa wako mbele sana na mbali sana, lakini sio hoja CCK wakawatimulia vumbi? sio hoja CUF waka-regroup na kufanya vema.
 
Ndo tegemeo la watanzania chadema ndo mkombozi wetu
 
Ndo tegemeo la watanzania chadema ndo mkombozi wetu

"I am not a liberator. Liberators do not exist. People liberate themselves" by Ernest Che Guevara.
Hata hivyo Chadema anaweza kuwa wewe (ukijisemea mwenyewe), au anaweweza kuwa mimi (nikijisemea mwenyewe) Lakini kamwe mimi siwezi kusema wewe ni chadema (mkombozi) na kamwe nawe usijeamini mimi ni chadema (mkombozi). Hata raisi wenu aliaminiwa kwa zaidi 81% na wapiga kura (sio watz) leo mnalia.
Sema mimi ni mkombozi sio yule ni mkombozi, utaumia!
Kila mtu anaweza kujikomboa mwenyewe, na kama kila mtu atapata ukombozi wenye mantiki, basi mtajikuta pamoja kwenye furaha ya ukombozi.
Mungu wetu anaita sasa!
 
"I am not a liberator. Liberators do not exist. People liberate themselves" by Ernest Che Guevara.
Sema mimi ni mkombozi sio yule ni mkombozi, utaumia!
Kila mtu anaweza kujikomboa mwenyewe, na kama kila mtu atapata ukombozi wenye mantiki, basi mtajikuta pamoja kwenye furaha ya ukombozi.
Mungu wetu anaita sasa!
Hii falsafa ya kuwa kila mtu anaweza kujikomboa mwenyewe ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo. Tunaona tuliowapa dhamana "wanavyojikomboa wenyewe" na kutuacha Watanzania mafukara.

Vyenginevyo, ninakubaliana na maelezo yako mengine kuhusu kosa la Watanzania kuamini kuwa chama fulani kitawakomboa. Ukombozi wa nchi [na ujenzi wa nchi kwa jumla] ni kazi ya wananchi wenyewe. Nilishasema mara kadhaa na sichoki kurudia kuwa "kinachohitajika Tanzania ni ukombozi wa mawazo" na wala sio kubadilisha Chama tu.

Nitawasikitia CHADEMA au chama chochote kuchukua madaraka wakati bado wananchi hawajabadilika sio kwa kujua haki zao, bali kujua na kutimiza wajibu wao kama wananchi wazalendo. Watanzania kwa miaka mingi tumekosa uzalendo.

Ningekishauri chama kinadhamiria kuiongoza Tanzania kipigane na hilo kwanza kuwakomboa Watanzania kifikra, badala ya mfumo wa "Chama kwanza nchi baaye", na "mimi kwanza (wengine) taifa baadaye", mkazo uwe "Nchi na taifa Kwanza kabla ya chochote."

Mungu Iokoe Tanzania - Kwa sasa Tanzania inahitajika zaidi kuokolewa kwani baraka inazo.
 
Back
Top Bottom