WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Asante WoS, hawa ndio Watanzania tulivyo na sasa za nchi yetu, ni maneno mengi na vitendo vichache. ili kuingia bungeni na kuonekana ni mbunge machachari, lazima ujue kupiga sana domo hata kama wanachi wako wanakula majani.
Prof. Shivji aliwahi kusema, kuna wanasiasa hawapendi siasa bali wanataka madaraka kuneemesha matumbo yao. lakini pia kuna wananchi wanauchungu na nchi hii lakini hawako tayari kuisogelea siasa kwa sababu ni mchezo mchafu. Mmmoja wenye uchungu na nchi hii ni Mzee Mwanakijiji na wengine wengi wamo hata huku JF pia wamo. Uwezo wa kusema sana upo, tatizo ni uwezo wa kutenda!.
Kwa wenzetu mlio mbali, endeleeni kusema tuu, sisi tuliyoko huku jikoni, wengine wetu tilishatenda na tukatendwa unakia mahali unalazimika kuchagua ama ujinyamazie utunze familia yako siku ipite, ama utende, utendwe, usahaulike na hutasota tena maana utakuwa umekwisha habari yako, tatizo ni familia. Ukitanguliza mapenzi yako kwa nchi yako, huu ndio uzalendo wa kweli, utasema lolote na kufanya lolote kwa ajili ya nchi yako, ukitanguliza mbele familia yako, familia yako, kabla ya kusema na kutenda, unajiuliza mara mbili mbilimbili 'so what?'. na wengine wetu huamua kukaa kimya bila kusema lolote, bila kutenda lolote na kuiacha siku ijipitie, ikawa asubuhi, ikawa jioni, siku ikapita.
Pasco,huo ndiyo ukweli kwa walio wengi.Kama ni uchambuzi na upembuzi wa matatizo ya nchi yetu na viongozi wake hakuna kilichobakia.Hali halisi inajulikana, matatizo, mapengo, viunzi/vikwazo vyote vinaeleweka.Mapendekezo yameshatolewa katika kila eneo.Kilichobaki ni utekelezaji tu.Inanikumbusha tafiti chungu nzima ambazo zimefanyika na mapendekezo lukuki kutolewa na maripoti kibao kujaza mashelfu na sasa technolojia imerahisha uhifadhi wa haya matokeo.
The country is heavily pregnant with ideas - what is needed now is the midwife to deliver the baby.And we all know that it is painful to deliver.....nani yuko tayari kuumwa uchungu wa kuzaa??? Ingewezekana kukwepa nadhani hakuna mwanamke angeukubali uchungu wa kuzaa.... ila nature has its own way to ensure whether u like it or not utazaa!Bahati mbaya sana mimba iliyopo kwa sasa haina cha kuisukuma izaliwe....kuzaa ni hiari..tutasubiri sana.
Ukisema eti wananchi waandamane kupinga mambo fulani kama walivyofanya nchi nyingine, tulion akilichowapata wazanzibari kipindi kile cha uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi.Nani anataka kufa? nikifa, nani atakumbuka kuwa nilifia nchi waje wanilelee wanangu? Sana sana watu wanaweza kunicheka na kusema yule naye! Haya kimbelembele kimeiponza familia yake... ona sasa wanae wanavyotaabika!
Binafsi sioni mabadiliko makubwa saaaana katika kizazi hiki ambacho kimeshaharibika kuanza fikra, mitizamo na vipaumbele vya maisha.
Haya ni mawazo yangu ya moyoni yasio na unafiki wa kufurahisha baraza.