Kortini kwa kumtapeli Mama Kikwete

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani (jina tunalihifadhi), mkazi wa Mbagala Kuu jijini Dar es Salaam, amefikishwa mahakamani kujibu shtaka la kughushi cheti cha elimu.
Anadaiwa kukiwasilisha cheti hicho katika ofisi za mfuko wa Wanawake na Maendeleo (WAMA), unaoongozwa na mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete, kisha kujipatia Sh. 689,500.
Kesi hiyo imefunguliwa katika mahakama ya wilaya ya Ilala ambapo hati ya mashtaka ilisomwa na Wakili Credo Lugaju, mbele ya Hakimu Mkazi Pamella Kalala.
Mwanafunzi huyo anakabiliwa na mashtaka matatu ya kughushi, kuwasilisha hati za kughushi na la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu
Katika shtaka la kwanza ilidaiwa kuwa katika siku, muda na tarehe isiyofahamika huko shuleni Jangwani, mshtakiwa alighushi cheti cha matokeo ya mtihani wa kidato cha nne chenye namba 0890208.
Cheti hicho chenye namba S. 0204/0561 kilidaiwa kuonyesha matokeo ya kughushi yaliyodaiwa na mshtakiwa kuwa ni halali.
Pia ilidaiwa kuwa Juni 12, mwaka jana, muda wa mchana katika ofisi za WAMA zilizoko mtaa wa Luthuli, huku akijua kuwa ni kosa na kinyume cha sheria, mshtakiwa huyo aliwasilisha cheti cha kughushi.
Cheti kinachodaiwa kuhusika katika shtaka hilo kilikuwa na jina la Halima Mahamoud na kiliwakilishwa kwa mtu aliyetajwa kwa jina la Subira Mgalu.
Katika shtaka la tatu, ilidaiwa kuwa kati ya Juni 6 na Desemba 29 mwaka jana, muda wa mchana huko ofisi za WAMA, mshtakiwa alijipatia Sh. 689,500 kutoka kwenye ofisi hizo kwa udanganyifu.
Ilidaiwa kuwa alijifanya anakwenda kuzitumia kwa ajili ya kulipia ada ya shule, matumizi ya shule na tiba kitendo ambacho ni uongo.
Mshtakiwa alikana makosa yote na kurudishwa rumande kwa kukosa wadhamini wawili wa kuajiriwa katika taasisi zinazotambulika serikalini.
Kesi hiyo ilipangwa kutajwa tena mahakamani hapo Machi 4 mwaka huu na upelelezi bado haujakamilika.
 
Kwa hiyo anaitwa Halima Mahmoud..,sasa wamehifadhi jina gani hapo..
 
Riziwani katapeliwa na fundi seremala kesi iko mahakamani,
leo mama kikwete katapeliwa.
Je ni kwamba hawa ni matajiri sana au hawana kabisa mbinu za kuwagundua matapeli?
 
Back
Top Bottom