Korea ya Kaskazini na Tanzania:Picha haiko sahihi!

Inaonekana tatizo linalotukabili tumeshalijua-atleast wengi wetu. Kwamba ni uongozi mbovu, ukosefu wa uadilifu na kutowajibika kikamilifu.

Sasa naomba niulize: Huo uongozi unapatikana vipi??? Do we get our leaders from Mars?

Kwa hiyo fundamental issue hapa ni namna ya kubadili mfumo wetu wa kupata viongozi kusudi tuweze kupata viongozi waadilifu na wachapakazi. Hapa hakuna swala la teknolojia wala misaada. Tatizo liko kwetu tunaochagua hao viongozi. Either sisi ndo hatujui tatizo ni nini au tunaamini kwamba uongozi siyo tatizo. Na kama tatizo siyo uongozi basi adui yetu yuko kwingine..tuendelee kumsaka!

Hatuwezi kulia lia kila siku eti wanaotukwamisha ni viongozi wasio waadilifu wakati tukipewa nafasi ya kuweka viongozi tunaoona wanatufaa.. tunachagua wale wale. Sasa hapo mwenye tatizo ni nani haswa? ni kiongozi aliyechaguliwa au ni wewe uliyemchagua..halafu baadaye unaanza kumlaumu? na hata ukimlaumu..akirudi tena unamchagua..si na yeye anakuona punguani?

Kuna jamaa alisema: "stupidity is doing the same thing over and over again expecting different results"

Kwa hiyo kama tunafanya yale yale kila baada ya miaka mitano, we can as well forget this debate ya maendeleo! Unless adui wa maendeleo yetu yuko kwingine na si uongozi. Sad but true.

Masanja,
 
Well said............Mkuu Masanja,

Inabidi kuongeza nguvu kuelimisha wananchi kuwa wanao uwezo wa kuleta mabadiliko...............JF tunaweza kuanza na wabunge wa sehemu fulani as pilot campaign kuwaelimisha wananchi juu ya power waliyonayo......just thinking......
 
but Mkuu unajua kuwa udikteta ni kama falsafa ya uongozi ambayo ikitumiwa vizuri inaleta maendeleo ya haraka? mfano mzuri Japani walianza kuendelea katika falsafa hiyo katika zama zile za Meiji na kupiga hatua kubwa ya maendeleo licha ya kuwa asilimia kubwa ya mali ghafi za viwanda vyao wanaagiza nje. Kwa korea kujitenga kunawaleta faida moja kubwa inayochangia maendeleo yao kiasi kuwa wana uhuru wa kufanya maamuzi makubwa bila ya kubugudhiwa sana na mataifa beberu ndo maana masoko yao ya kuuza silaha hayachagui mradi pesa tu kwao...
 
Inaonekana tatizo linalotukabili tumeshalijua-atleast wengi wetu. Kwamba ni uongozi mbovu, ukosefu wa uadilifu na kutowajibika kikamilifu.

Sasa naomba niulize: Huo uongozi unapatikana vipi??? Do we get our leaders from Mars?

Kwa hiyo fundamental issue hapa ni namna ya kubadili mfumo wetu wa kupata viongozi kusudi tuweze kupata viongozi waadilifu na wachapakazi. Hapa hakuna swala la teknolojia wala misaada. Tatizo liko kwetu tunaochagua hao viongozi. Either sisi ndo hatujui tatizo ni nini au tunaamini kwamba uongozi siyo tatizo. Na kama tatizo siyo uongozi basi adui yetu yuko kwingine..tuendelee kumsaka!

Hatuwezi kulia lia kila siku eti wanaotukwamisha ni viongozi wasio waadilifu wakati tukipewa nafasi ya kuweka viongozi tunaoona wanatufaa.. tunachagua wale wale. Sasa hapo mwenye tatizo ni nani haswa? ni kiongozi aliyechaguliwa au ni wewe uliyemchagua..halafu baadaye unaanza kumlaumu? na hata ukimlaumu..akirudi tena unamchagua..si na yeye anakuona punguani?

Kuna jamaa alisema: "stupidity is doing the same thing over and over again expecting different results"

Kwa hiyo kama tunafanya yale yale kila baada ya miaka mitano, we can as well forget this debate ya maendeleo! Unless adui wa maendeleo yetu yuko kwingine na si uongozi. Sad but true.

Masanja,

Wewe ndiyo anafikiri hivyo. Wenzako CCM ameshatuwekea development plan kibao na wanategemea katika miaka 15 - 20 ijayo TZ itakuwa kama South Korea, Singapore au Malaysia.

Sasa wewe usitukatishe tamaa kwa vile maendeleo yako njiani. Mkapa alishaweka msingi na sasa JK anajengaukuta kwa nini unafikiri haitawezekana??

Au mwenzetu Msingi wa Mkapa na Ukuta wa JK hauuoni??
 
In 46 years you have no "Technology and Capital" do you expect that you will have it in the current situation where people think like you? Mwanakijiji never said we shall stop our relationship with the West, he just asked: Why we have a very good relationship with the west "who have Technology and Capital" and we are still backward and Korean have such bad relations and are better than us? Answer that question first.

That's not even a question.

As I said no country has been developed simply because of good or bad relationship with the west. This is to say, good relationship alone is not a [causal] factor. It depends on how you capitalize on that good relationship.

North Korea is not doing fine [if they are doing fine] because of their bad relationship with the West. My problem with your [& Mwanakijiji] argument is that, you think of relationship with the west as a determining factor [ a deal breaker].

That is if you have a good relationship with the west then you should not be poor. North Korea wana uhusiano mbaya na nchi za magharibi lakini wanafanya vizuri. Sisi tuna uhusiano mzuri na nchi za magharibi lakini tunafanya vibaya.

Don't you see that good relationship alone is not a factor. Now, bad relationship with the west will do more bad than good. North Korea ingekuwa wapi kama isingekuwa na vikwazo? So, maendeleo ya nchi yataletwa na wananchi wenyewe, kwa kufanya kazi.

You cannot sit back and relax, ukisubiri mahusiano yetu na nchi za magharibi yawe mazuri au mabaya ndipo tuendelee. Is this what you are telling us? And why do you think you are right by suggesting that our good relationship with the west might be a reason for our mess?
 
Tatizo kubwa siku zote kwa nchi hizi za afrika ikiwemo tanzania linachangiwa na mambo yafuatayo:

(1) ushabiki kupita kiasi wa vyama bila kuangalia nini chama kitafanya kurekebisha mustakabali wa nchi na vile vile uwajibikaji wa mwanachama mmoja mmoja katika kuchangia maendeleo ya nchi

(2) viongozi ambao wamejikita kwenye propaganda na wala sio kutekeleza majukumu muhimu ya nchi. Si jambo la kushangaza kuambiwa kuwa viongozi wanatekeleza sera za chama tawala lakini ukiuliza tafsiri ya sera hizo kwa vitendo, muda (long term and short term) hutapata bla bla bla tu.

(3) information gap ambao wengi wameichukulia kama ni faida kwao. vitu vingi vyenye kugusa maslahi ya taifa vimekuwa siri tu hata bunge halina nguvu ya kuhoji

(4) mfumo mbovu wa kiutawala ambao umekosa ufanisi, mwelekeo etc ambao mwisho wa siku unaletea hasara taifa! je kuna umuhimu wa kuwa na DED, RAS, RC, DAS? kweli haiwezekani kupunguza mivyeo hii?

(5) utawala ulolemazwa na misaada, sera nyingi zimekuwa zimetokana na external influences (donor community) na mwisho wa siku tunatengeneza sera ambazo wao wanataka na sio zinatokana na mahitaji ya watanzania

(6) kupoteza imani kuwa vitu vyetu haviwezi kuendelea bila misaada au ushauri kutoka kwa nchi nyingine. siku zote huwa naamini mtu anapojikwaa hujifunza kutembea vizuri. na kama philosophers wanavyosema failure ni mwalimu mzuri! kwanini hatuwezi kutengeneza economic models zetu? solutions ambazo zinalenga matatizo yetu wenyewe (tanzanian perspective)? k

wa mfano students wa makerere wametengeneza gari in very crude forms but if well funded do you think they can develop something better (ref: prototype this in the discovery channel) ni kitu kidogo but will motivate, encourage change of mindset, attitude and ultimately pipo will start to invent. Challenge: let us believe in ourselves and go out and implement! All the G20 we bow at them today they were once worse than us. And who says that aliyekutangulia basi hutamkuta au kumpita?
 
That's not even a question. As I said no country has been developed simply because of good or bad relationship with the west. This is to say, good relationship alone is not a [causal] factor. It depends on how you capitalize on that good relationship. North Korea is not doing fine [if they are doing fine] because of their bad relationship with the West. My problem with your [& Mwanakijiji] argument is that, you think of relationship with the west as a determining factor [ a deal breaker]. That is if you have a good relationship with the west then you should not be poor. North Korea wana uhusiano mbaya na nchi za magharibi lakini wanafanya vizuri. Sisi tuna uhusiano mzuri na nchi za magharibi lakini tunafanya vibaya. Don't you see that good relationship alone is not a factor. Now, bad relationship with the west will do more bad than good. North Korea ingekuwa wapi kama isingekuwa na vikwazo? So, maendeleo ya nchi yataletwa na wananchi wenyewe, kwa kufanya kazi. You cannot sit back and relax, ukisubiri mahusiano yetu na nchi za magharibi yawe mazuri au mabaya ndipo tuendelee. Is this what you are telling us? And why do you think you are right by suggesting that our good relationship with the west might be a reason for our mess?

Zungu, I think you misunderstand the whole sentiment behind the question; what you are saying is actually what I am implying.

Lakini pia zaidi ni kuwa Tanzania katika hali ya kawaida ingetakiwa kuwa imepiga hatua kubwa ya maendeleo kulinganisha na nchi nyingi za kiafrika au hata za mabara mengine. Hatujawahi kuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, tuna mazingira mazuri ya kijiografia, kisiasa tumekuwa na utulivu wa kutosha, tuna raslimali lukuki, tuna watu wa kutosha tu kama sehemu ya nguvu kazi n.k Kwanini tupo hapa tulipo?

Kinachonogesha zaidi ni kuwa sisi ni wapokeaji wa misaada mikubwa ya kigeni wa kwanza katika Afrika (kama nchi) na kwa muda mrefu tumepokea mabilioni ya fedha za misaada na mikopo ya kila aina; zaidi ya yote tumekuwa miongoni mwa nchi zilizofutiwa karibu madeno yote yasiyolipika na nchi mbalimbali na taasisi mbalimbali za fedha. Huwezi kuelezea umaskini wetu rationally na ukaeleweka.

Katika muda wote huo ni kitu gani tumefanya ambacho kinaonesha umahiri wetu kwenye jambo lolote? Tumeunda kitu gani cha kujivunia na kusema kuwa hiki ni mazao na matunda ya ubunifu wetu? Tumeboresha kitu gani kilichoundwa na wengine na kukifanya kuwa ni cha kwetu kweli? Leo hii hata samani tunaagiza toka ng'ambo, nyanya toka ng'ambo na vitunguu toka ng'ambo. Vyote hivyo ni kwa sababu, hatuna ulazima wa kuangalia nguvu zetu wenyewe kwani kama tunaweza kuvipata kwa wenzetu why bother?

Wakati Biafra imejaribu kujitenga na Nigeria na wakawa wako under siege kwa karibu mwaka na zaidi walijikuta wanalazimika kutegemea ubunifu wao wenyewe kuendeleza viwanda, mashinde mbalimbali n.k Ni hilo hilo linalotokea Cuba na Korea ya Kaskazini. Unapojikuta umebanwa kwenye kona unalazimika kurudi kwa watu wako na uwezo wako wa ndani kuhakikisha kuwa una survive. Tanzania haijawahi kufikia mahali hapo. Kwani kwetu sisi there is no necessity!

Whatever we want our uncles can provide and whatever we short off our cousins can finance easily!

Sasa ninachojengea hoja ni kuwa kama North Korea katika kutengwa kwake na jamii ya kimataifa imefikia literacy level ya 99% wakati Tanzania ikiwa na video, na matv na ma internet bwelele level yake ni 70% then something is wrong! Kama nchi iliyotengwa na kupigwa vita na kuitwa axis of evil inaweza kutengeneza magari yake, meli zake, zana zake za kijeshi, miundo mbinu yake n.k tunaweza vipi kuelezea upungufu wetu?

Sasa sizuungumzii North Korea kama mfano wa nchi za kidemokrasia au kusema kuwa maisha ni mazuri sana na kwamba kuwa chini ya utawala wa kidikteta ni bora; ninachojengea hoja ni kuwa kuna faida gani kuishi katika uhuru na demokrasia ya vyama vingi kama muda mrefu tunatumia katika siasa, udaku, na kupiga domo!

Umesema suala ni kufanya kazi; ndiyo nakubaliana na wewe! Huko nyuma tuliwahi kuwa na "Kazii ni kipimo cha utu"; tuliukataa unyonyaji na ukabaila, tulitaka kujenga jamii ya watu wanaoheshimu na kupenda kazi. Tulianza kutengeneza vitu vyetu sisi wenyewe kwa kutumia wataalamu wetu wenyewe kuanzia radio, matairi, mashine mbalimbali, betri, zana za kilimo, n.k n.k Vyote tulivifanya kwa sababu tuliamini kuwa tunaweza kufanya mambo hayo. Wakati huo bidhaa za kigeni zilikuwa adimu na hivyo ilitulazimu kufanya mambo kivyetu vyetu.

Ndipo ikaja rukhsa!

Tukafurahia kupata mitumba sokoni, kuagiza maradio ya PANASONIG (mwenyewe nilinunua nilidhania PANASONIC!), tukafurahia kununua ma TV (nakumbuka miaka ile hadi uende Zanzibar kununua) au kwa sisi wa kanda ya ziwa kwenda Kampala! Sasa ikawa ni ruksa kubweteka kwani hatimaye vyote tunavyovitaka tunaweza kuvipata kutoka kwa "wafadhili". Matokeo yake viwanda vyetu vikaanza kufa taratibu huku tukibeza bidhaa zetu!

Na katika akili zetu wenyewe tukaamua "hey, we don't need them why don't we privatize them". tukaanza kuvigawa kama njugu na kama miogo ya kukaanga iliyowekwa masala tukaviweka juani. Aliyetaka alikuja na kutwaa kwa bei ya chee! Wenyewe tukaona sifa kuwa hatimaye tuko kwenye ubepari kweli kweli! Tukabinafsisha hadi uzalendo wetu! Katika uduni wa maoni yetu wenyewe tukaona Watanzania hawawezi kuendesha kitu chochote tukaanza kuleta wageni kutuendeshea vitu vyetu, NBC, Tanesco, ATCL, Posta n.k

Leo hii Watanzania wapo wapo tu, hata kile kidogo wanachoweza kukifanya wenyewe inabadi wapate ushauri toka kwa kina mjomba (si unakumbuka suala la Dowans na kampuni ya ushauri toka Ujerumani)?

Sasa hapa ndipo sisitunaona fahari, wakubwa wakija na kutupa pongezi tunaona sifa, matokeo yake tunalalamika kuona Wachina wanazidi kujazana na Wakenya nawatu wengine ambao wanaonekana kuchukua nafasi zetu. Really?

Sasa Korea ya Kaskazini wamelazimika kujitegemea kweli kwa karibu vitu vingi. Katika unyonge wao na katika kutengwa kwao wamelazimika kujiangalia wao wenyewe. Na katika kufanya hivyo wameweza kufanya mambo ambayo sisi wengine tunayawazia na kuombea kina Brown na Obama kutusaidia kuyafanya.

Swali linabakia, ni jinsi gani basi tunaweza kuchochea wananchi wetu kujitegemea na taifa letu kutegemea nguvu zake zenyewe, vipaji vyake na wataalamu wake? Tunaweza vipi kuamsha fikra za utafiti na ubunifu na kuzawadia vipaji mbalimbali vilivyolala ndani ya wananchi wetu? Je tuchague njia ya DPRK (piss off the West and do our own thing) au tufikiri namna mpya ya kuhusiana na nchi nyingine hasa hizi kubwa bila ya kuonekana tegemezi hadi wa fikra?
 
north korea mbona mbali mnaionea tanzania.....linganisheni tz na somalia hatuwafikii wametuacha mbali......
 
Mkuu, umeniacha hoi..kweli JK wananchi wake wamemchoka jamani...duh..
Lakini unajua nini? Kwa yeyote ambaye kesha tembelea Somaliland..atakubaliana na wewe! I for one I do!
 
Mwanakijiji,

Asante kwa post nzuri.
Tufanye kuwa baada ya kujadili post hii;

1. Tumeweza kufanya uchunguzi wa kutosha na kuweza kuyatambua matatizo tuliyonayo na makosa tunayoyafanya sisi waTanzania yanayo tuzuia kuendelea.

2. Tumeweza kupiga hatua kubwa zaidi, nakuweza kupata suluhisho la matatizo na marekibisho ya makosa hayo.

Kitu ambacho TUNGEKIKOSA kingekuwa ni Kiongozi ambaye atatutoa mahali tulipo na kutupeka kwenye utekelezaji wa suluhisho lililopatikana (2).

Kwa maoni yangu, hapa ndipo tatizo lililopo, kwani hata bila ya kuwa na 1. na 2., kiongozi anayefaa angeweza kuwa chachu wa/ chanzo cha kuwepo kwa 1. na 2. kwa nia ya kutupeleka kwenye maendeleo.
 
Mkuu, umeniacha hoi..kweli JK wananchi wake wamemchoka jamani...duh..
Lakini unajua nini? Kwa yeyote ambaye kesha tembelea Somaliland..atakubaliana na wewe! I for one I do!
Wait a minute.....nani aliwahi kufika Rwanda baada ya genocide? nilifika laiti kama ingekuwa ni tanzania leo hii labda tungekuwa tumeshakufa kwa dhiki....lakini iangalieni the new Rwanda after 14 years huwezi kuamini kama ndio ile ya mwaka 1995......

Unazungumzia Somalia Mogadishu au ile ya Puntland... ?
mogadishu.....
 
Kulinganisha utawa wa kiimla wa Korea ya Kaskazini na Tanzania ni sawa na kufananisha mbingu na ardhi.

Mosi, Korea kaskazini imefika hapo ilipo kutokana na vita baridi kati ya kundi la 'warsaw' na lile la NATO.

Pili, Urusi na Uchina waliwekeza sana katika utawala huu hasa katika nyanja ya teknolojia ya ulinzi na usalama na kupuuza masuala muhimu ya usalama.

Tatu, kuendeleza sehemu hiyo ya pili hapo juu, korean peninsular ni eneo lililokuwa maalum kwa usalama wa USSR na PRC kwa hiyo walimwaga kila aina ya msaada kulinda eneo hilo lisitwaliwe na USA.

Nne, wananchi wake wanakufanya njaa kwani serikali yenyewe imekalia kulimbikiza silaha na kufanya mauzo ya silaha kwenye 'lack makert'

Takwimu zinaonyesha ya kwamba pamoja na kuwa na teknolojia ya kisasa na kutambia mataifa makubwa lakini ukiondoa pazia utaona ya kwamba ni mrusi na mchina ndiyo wako nyuma ya move zote za Korea Kaskani. PRC wanauwezo wa kuruhusu mapinduzi na mabadiliko ya China.

Mwisho, Kim Jong Il anawatesa wananchi wake kwa njaa na wananchi wake wanaishi katika karne ya 18 kimaisha.

Hitimisho: Dikteta ni dikteta hata ukimpaka rangi za namna gani bado atabaki kuwa dikteta na hawana nafasi katika ulimwengu huru wa kidemokrasia. Unategemea Tanzania itaendelea ukiacha siasa mbovu , sera zisizo na manufaa kwa mwananchi wa kawaida na sasa UTAWALA ULIOPO MADARAKANI NI SAWA NA TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA CHEKECHEA AMBAYO UFANYA KAZI YA KUKIMBIZA MPIRA KILA KONA YA UWANJA BADALA YA KUWA PROFESSIONAL KWENYE HIYO KANDANDA YA KISIASA.

mwisho kabisa unategemea nini kama uchumi wa Tanzania asilimia 98 huko mikononi mwa sekta isiyo rasmi[DE SOTO 2005]? kisa: mifumo mibovu na uongozi usio na 'road map' au ukiwa na road mapo haujui kuweka vipaumbele.

Mungu Ibariki Tanzania

Sidhani kama kweli ni democracy ya kweli western educated person kupiga kura na locally educated person kwa kutumia analysis ya western driven policies yet tukawa kwenye same level ya decision making kuamua this is my choice i.e good for my well being. Sikubaliani nayo kabisa democracy ambayo haiko guided ni kama free market iliyoleta global economic crisis. We realy need to redefine democracy in our own (local) context otherwise tutaendelea kufuata mkumbo wa dunia yenye selfish individuals to safe guard their group interests.

Inasikitisha kwamba wakati wananchi bado wako trustworth ndiyo maana wakipewa wali na kanga wanabakia waaminifu kupigia kura huyo mtu but the one who gave the wali anakuwa tapeli baada ya kupata alicho kihitaji. Hii inapeleka ujumbe mbaya sana kwani after a while hii trust tukiipoteza hata ungekuwa unatokea mass hawatoamini tena na ndo kinachojitokeza kwenye working class moyo wakujituma kufanya kazi unakufa sijui tutaweza kugawana huu umaskini? Yet tunakumbatia democracy za western definition wakati hata wao kuna limitations on sensitive issues.
 
Back
Top Bottom