Korea Kaskazini yatoa ujumbe usioelewaka! Korea Kusini yashikwa kiwewe

Yaani hawa jamaa huwa wananichekesha sana, N. Korea yeye ni mkwara mara ahamishe makombora mara hivi hawaeleweki,wanakuwa kama kitoto wakitaka kupigana mtu anaanza kukunja mikono ya t-shirt wakati haihusiani
:-!:-!:-!
 
Haya mabingwa wa cryptography mtudadavulie maana ya hizo secret messages.
Unahitaji key ku "decode"...Hivyo vitabu vya ku "decode" wanavyo hao wanaotuma na wanaopukua. Lakini inaweza kuwa ni bosheni tu kuwapanikisha Korea kusini maana unaona tayari wamepaniki. Ingekuwa ni misheni ya kweli wasingetuma wazi hivyo ukizingatia wamarekani nao watakuwa bize kuifungua
 
Hawa jamaa ipo siku wataitia dunia kwenye vita kuu ya 3.. Maana mi hata siwaelewi alaf mijitu yenyewe ni ndugu kabisaaaa, yan ni wapuuz mpaka basi
Si wanatenganishwa na USA ili wasije wakaungana kwa sababu zile Korea ziko kwenye eneo la kimkakati, wakiungana USA anaona atakuwa kwenye hatari. Kwa hiyo anasingizia kwa kusema Korea Kaskazini wakorofi na kutumia sababu mbalimbali ili hao ndugu wawilo wasije wakaungana wakawa tishio kwa USA. Ndio hivyo...
 
Hata bila ya msaada wa marekani korea kusini anauwezo wa kutoa kichapo kikali kwa korea kaskazini. Korea kusini wapo juu kijeshi kuliko korea kaskazini tena kwa umbali mrefu tu. Wana silaha za kisasa zaidi, bajeti wao ya jeshi ni kubwa zaidi. Ni kati ya nchi 10 zenye uchumi imara duniani. Hata bila marekani Ikitokea vita kati ya hizi nchi mbili sidhani kama korea kaskazini anaweza ku survive labda asaidiwe na china
Naam unaongea kwa taarifa zile zile za kimagharibi....maana ndio haohao wanaotoa taarifa za kuweka nafasi na uwezo Wa mataifa mbalimbali duniani...!!! Walakini hazina ukweli 100%,
 
Hizi nchi mbili hazitakuja kupigana, sanasana ni miaka ya mbele zitakuja kuungana na kurudi kua nchi moja.
Hizi mbwembwe za North Korea kila mwaka ni maneno tu, wanajua vizuri uwezo wa kupigana hawana, wakifanya chochote nchi zote za UN zitaamsha majeshi yao kuishambulia kwa nguvu moja ya ajabu sana, they won't stand a chance, nchi kama marekani sio ya kuichukulia poa kabisa, vifaa walivyo navyo wanaweza kuiangusha N.Korea ndani ya muda mfupi mno.
 
Hata bila ya msaada wa marekani korea kusini anauwezo wa kutoa kichapo kikali kwa korea kaskazini. Korea kusini wapo juu kijeshi kuliko korea kaskazini tena kwa umbali mrefu tu. Wana silaha za kisasa zaidi, bajeti wao ya jeshi ni kubwa zaidi. Ni kati ya nchi 10 zenye uchumi imara duniani. Hata bila marekani Ikitokea vita kati ya hizi nchi mbili sidhani kama korea kaskazini anaweza ku survive labda asaidiwe na china
Kuna mamburulas humu yatakubishia tu, South Korea ni taifa la first World wakati kaskazini ni Second World au third kabisa.
Na wanalo jeshi la kisasa kabisa duniani lenye uwezo na mbinu nzito za kupigana vita.
 
Marekan siyo jitu la kuliamini asilimia 100%! Korea kusini kinaweza kikanuka Marekani akasema atatuma ndege za kuogeza mafuta tu hapo korea kusini akala kichapo cha mbwa!
au aanze kuwauzia silaha
 
Jamani mimi sielewi kabisa hivi ugomvi wa north na south korea ni nini si ni kila mtu ana kwake
1:Maslahi(Russia vs USA).
2:Ujamaa wenye msimamo mkali(Communism) vs Ubepali mkali(Imperialism).
3:Maeneo ya kimkakati(Strategic area of influence) (a) Russia:- China, North Korea na kwenye maeneo mengine kama Indochina(Vietnam, Laos na Cambodia na bahari ya China Kusini(Paracel Islands na Spratly islands).
(b) USA(Marekani):- Japan, Korea Kusini,Taiwan na visiwa vingi kama Guam, Federated state of Micronesia, Northern Mariana Islands etc. Maeneo yote na mengine ambayo sijayataja ambayo yamekaa kimkakati zaidi ndiyo tatizo kubwa sana hasa kwa kuzingatia namna ya kueneza ushawishi hapa Duniani kwenye Mataifa mengine.

HITIMISHO:

Urusi hata kubali kushindwa/kuzidiwa kete na Marekani katika dhoruba inayoendelea kwenye eneo la Peninsula ya Korea, na upande wa Marekani ni hivyo hivyo. Mmoja kati yao kushindwa itakuwa ni aibu/fedheha kwa washirika wake kwamba yeye ni m'babaishaji tu na sio wa kutegemewa katika harakati thabiti za kujikomboa kwenye makucha ya Kibepari kwa wale ambao hawataki kabisa kujihusisha na sera za Kibepari na upande wa pili ni hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom