Lisa
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 1,549
- 1,074
Ameolewa na ana watoto wawili , Mungu amempa watoto wakike 2.Lkn Kuanzia baba mkwe , mawifi , shemeji zake wanamlaumu kwa kuzaa watoto wakike, na kusema mwanamke gani anazaa watoto wakike tuu.wakamshauri mwanaume akaenda kuoa mke mwingine ambaye atamzalia mtoto wa kiume.Bahati mbaya huyo mwanamke alizaa mtoto wa kiume lkn tahahira.Na katika wale mawifi waliokuwa wanamlaumu mke wa kwanza wa kaka yao, naye ameolewa amezaa mtoto wa kiume lkn tahahira. sasa wanasema huyo mke wa kaka yao wa kwanza ndiye anayewaroga wanazaa watoto wa aina hiyo, jamani mshaurini maana ameshachoka , kipi bora aendelee kubaki kwenye ndoa hiyo ili alee watoto au Aondoke maana amelemewa na lawama.