Kongamano la Kupinga Death Penalt in Tanzania Ubungo plaza

...ndo mana tunaendelea kuwa maskini. Wenzentu china ukipatikana na kesi ya rushwa unanyongwa. Leo hii tanzania mnapinga adhabu ya kifo.
 
Haya makongamano wakati wananchi wa tanzania wako katika wkt mgumu kimaisha yanaandaliwa na system (UWT) ili kuondoa macho ya media na mawazo ya wananchi kwenye reality na kuwasahaulisha machungu wanayo yapata. Tazama machungu haya: nchi iko gizani(Ngeleja), elimu duni(sekondari za kata), mishahara duni, mafuta bei juu, mafuta yanachakachuliwa, hali ngumu ya usafiri na gharama kubwa ya maisha kwa wakazi wa mijini, madeni makubwa kwa serikali kutokana na wachache kujichotea fedha za umma(EPA, DOWANS, Alex stewart), watanzania wenye sifa kushindwa kusaidiwa ili wasome vyuo vikuu, serikali kushidwa kutoa huduma kwa jamii, bunge lisilokuwa na maamuzi lililojaa usharobaro, rushwa iliyokithiri. Sasa watanzania kunahaja ya kuwa na midahalo ya mambo ya kufikirika na kuacha nchi ikichuliwa na *****. Hizi taasis zenye sauti kwa hakika zinatumiwa na system kutusahaulisha haya machungu kwani ni Tanzania tu ambapo raia anatandikwa na bakora zote hizi na kuvumilia. Nashauri taasis hizi zipange ratiba ya open debate juu ya hizi burning issues na tusimamishe midahalo yoyote ambayo itachangia ku-divert community attention mpaka kieleweke
 
Tatizo sio adhabu ya Kifo!
Tatizo ni utawala mbovu, ndio cha kujadili kipindi hiki.
 
Back
Top Bottom