Kongamano la CHADEMA Vyuo Vikuu Dodoma

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
863
Wakuu.Habari za Jumapili.

Leo tena tunaendelea na harakati zetu za kujipenyeza na kuwekeza kwa Vijana wa Vyuo Vikuu.Vijana wa CHADEMA Dodoma wameandaa Kongamano kubwa la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma mabalo linaendelea hivi sasa katika Ukumbi wa African Dream Area D. Mada Kuu katika Kongamano hili ni Vijana Wasomi na Mustakabali wa Taifa.

Watoa mada ni Wabunge wa CHADEMA wakiongozwa na Kamanda Freeman Mbowe-Kiongozi wa Upinzani Bungeni(KUB).

Ukumbi umeshajaa na hivi sasa tupo tunasikiliza the Best Speech ya Martin Luther King tukiwa tunamsubiri Mgeni rasmi afungue mkutano.

Picha za Matukio mtazipata tukiwa tunaendelea.

P100411_1203.jpg

P100411_1147_01.jpg

Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira.
 
Mwalikeni pia mkuu wa mkoa wa Dodoma (hata sijui anaitwa nani) aliyepiga marufuku harakati za kisiasa za vyama vya upinzani UDOM
 
Hapo sawa , lazima kieleweke. Wakizomea wabunge wao, wanaona sawa, wakizomea wanafunzi ni utovu wa nidhamu!!!!! Safari hii walete darasa lingine, lakini hatudanganyiki.
 
Akhsante dada Regia na safu nzima kwa harakati zenu tuko pamoja.Kama hutojali tujuze safu nzima ya wabunge wa CHADEMA waliopo kwenye mkutano huo.Thanks
 
Msizime moto mpaka kuelekea uchaguzi maana bwana mkubwa anasema vyama vingine ni vya wanaharakati wakati ndo vimewafanya hawalali huko Dodoma.
 
Akhsante dada Regia na safu nzima kwa harakati zenu tuko pamoja.Kama hutojali tujuze safu nzima ya wabunge wa CHADEMA waliopo kwenye mkutano huo.Thanks

Wewe sasa unataka kuleta majungu,na wale ambao hawapo na wana udhuru unataka kusema wamekimbia au wana2miwa na CCM?
 
habari nzuri dada Regia, wasiwasi wangu wasije kusema mkutano hata huo wa ndani hauna kibali wakaja kupiga mabomu - Naunga mkono 100% wazo hili la kuwekeza kwa vijana ili waweze kujua hatma ya taifa lao na wawe tayari kulitetea, hakuna kuchelewa wakati ni huu.

Hebu tujuze safu ya wabunge (wapiganaji) waliomo ndani ya nyumba?
 
Akhsante dada Regia na safu nzima kwa harakati zenu tuko pamoja.Kama hutojali tujuze safu nzima ya wabunge wa CHADEMA waliopo kwenye mkutano huo.Thanks

Hivi sasa Kamanda Mbowe ndio anafungua mkutano.

Wabunge walioko ni
1.Mbowe
2.Mnyika
3.Lema
4.Wenje
5.Msigwa
6.Silinde
7.Prof Kahigi
8.Joseph Selasini
9.Esta
10.Naomi
11.Chiku
12.Raya
13.Sabreena
14.Kiwanga
15.Kiwelu
16.Christowaja
17.Christina
18.Pauline
19Mrusha sredi
 
Msisitizo uwekwe kwa vijana waliohudhuria wajitahidi kuwazindua na kuwaelimisha wenzao ambao hawakuhudhuria juu ya umuhimu na nafasi yao ktk ukombozi wa mtanzania...bravo UDOM...kura za hapo tu zinatosha kuwatia kiwewe mafisadi
 
Mbowe anasema kinachoendelea Dodoama sasa ni mipango ya MUNGU.Anasema wakati Kamati Kuu ya CCM inavunjika CHADEMA inafanya Kongamano na Wasomi.Amesema kuwa pamoja na CCM kujivua gamba lakini ni kazi bure kwani CCM wana Kansa na tayari iko ndani ya damu na akasema hii ni fursa kwa CHADEMA.
 
Asante dada Regia endelea kutujuvya, huna haja ya kututajia wabunge wote wa CDM zaidi ya mgeni rasmi na wale utakaotaka wewe.
 
Mbowe anasema kinachoendelea Dodoama sasa ni mipango ya MUNGU.Anasema wakati Kamati Kuu ya CCM inavunjika CHADEMA inafanya Kongamano na Wasomi.Amesema kuwa pamoja na CCM kujivua gamba lakini ni kazi bure kwani CCM wana Kansa na tayari iko ndani ya damu na akasema hii ni fursa kwa CHADEMA.

thanks Regia.. keep updating us please!
 
Wera wera weraaaaaa.....lete mambo dada RM! Hakika mwaka huu ccm watajinyonga kwa presure....yaani hawana pakutokea kabisaaa.
Zanzinbar kuna moto wa muungano na katiba,Tanganyika kuna moto wa katiba na mswaada wake. Dodoma kuna timbwili la CC ya ccm na huku CDM wakifungua matawi vyuoni!....ama kweli ccm sasa bye bye....acha niitemee mate ccm twuuuuh....
 
Back
Top Bottom