Hivi kuna ubaya gani katika kulalamika? Kuna ubaya gani kwa mtu kama Mzee Butiku na Warioba kumwambia Rais JK kwamba awe jasiri na kufanya maamuzi magumu hasa katika kusafisha CCM na Serikali yake. Kwamba Rais wetu amezungukwa na wafanyabiashara ambao wamemfanya mateka wao. Hivi kuna mtu mwenye akili timamu ambaye halioni hili? Kwamba anachotakiwa kufanya Rais JK ni kuwatema (to purge) hao ili CCM na Serikali virudi katika msitari. Nani asiyejua kwamba Serikali inashindwa kutekeleza kikamilifu maamuzi ya Bunge kuhusu Richmond kwa sababu ya hao wafanyabiashara waliomzunguka Rais wetu?
Kuna ubaya gani katika Mzee Butiku kutwambia kwamba watu wale wale waliogawa pesa kwa vijana wa CCM katika mchakato wa urais 1995(sio 2005) zilizotoka nje ya nchi bado wapo na walianzisha mtandao ambao ulimwingiza Jk Urais 2005 na kumtaka hauvunje? La sivyo kuna hatari huko mbele tuendako. Haya sio malalamiko bali ni WOSIA. Kama watanzania tuna utashi wa kusikiliza wosia huu na kukubali au kuukataa.
Binafisi mimi namliganisha mzee Butiku kama nabii. Kazi ya nabii ni kuhubiri na kutahadhalisha na manabii wengi walitahadhalisha lakini hawakusikilizwa matokeo yake majanga yakawapata hasa waisrael. Na sisi kama tusipomsikiliza huyu mzee na kumbeza eti alikuwa anamtaka Salim awe rais na hivyo apumzike akale pensheni ole wetu! Wenye masikio na wasikie.