TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Thursday, 30 September 2010 20:09 0diggsdigg
Exuper Kachenje
KATIKA kusaidia sekta ya elimu nchini, kampuni ya vifaa vya elektroniki ya Dell ipo mbioni kusambaza kompyuta milioni moja kwa wanafunzi nchini ili kupunguza matumizi ya madaftari na vitabu.
Meneja wa fedha wa Dell, Kanda ya Afrika ya Kati na Magharibi, Alwin Thankachan, alibainisha hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa wakala wa bidhaa za kampuni yake nchini ambao umepewa kampuni ya Mitsumi.
Kampuni ya Mitsumi pia imepewa uwakala wa bidhaa za kampuni ya vifaa vya elektroniki ya Toshiba ya nchini Japan ambayo kwa pamoja na Dell watasambaza bidhaa zao kupitia Mistumi zikiwemo kompyuta, vifaa vya studio, betri na vifaa mashine ya kuhifadhia umeme (Power Sever) vya Dell na Toshiba.
Thankachan aliyezungumza kwa kupokezana na meneja mkuu wa Mitsumi, Hitesh Shah ,alisema Dell kupitia kampuni ya Mitsumi inajipanga kuzungumza na serikali, Benki ya Dunia (WB) na wadau wengine ili kuwezesha mradi huo kuanza. "Kenya upo mradi kama huo unaendelea, tunasambaza kompyuta milioni moja kwa wanafunzi kusaidia sekta ya elimu, ikiwa ni mradi wa Benki ya Dunia," alisema Thankachan. Naye meneja mkuu wa Mitsumi, Hitesh Shah alisema,
"Tunajipanga kuzungumza na serikali, serikali ikiruhusu, mradi huo utaanza katika kipindi kisichozidi miezi sita ijayo." Kuhusu biashara Hitesh alisema kampuni inafanya kazi katika nchi 12 tofauti baadhi zikiwa Kenya, Uganda, Rwanda, Hongkong na kuwa nia yake ni kuwawezesha
Watanzania kuondokana na bidhaa bandia katika sekta hiyo zinazoathiri wateja na uchumi wa taifa, na kwamba wateja watakaonunua bidhaa za kampuni hizo kupitia Mitsumi watafanyiwa matengenezo bure. Akizungumzia Jumuia ya Afrika Mashariki, Hitesh alisema hatua hiyo ni ishara njema kwa wapenda maendeleo na kuwa itakuza biashara na uchumi wa nchi husika. Mwisho
Source:Mwananchi