Kombe la kumbukumbu la hayati philip mbogo(mb)

munduwakaya

Member
Oct 13, 2010
15
0
KAMPUNI ya Active Finance imedhamini ligi ya kumbukumbu ya aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Mpanda Kati, Mzee Philip Mbogo, kwa kutoa seti za jezi na mipira zenye thamani ya Sh milioni 4,500,000.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akikabidhi jezi na mipira hiyo kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi (UVCCM) wa Mkoa wa Rukwa, Paul Mzindakaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Kevin Mbogo, alisema ligi hiyo ni maalumu kwa kuenzi mchango alioutoa Mzee Philip wakati wa uhai wake.

“Ligi hii ni maalumu kwa kumuenzi Mzee Philip ambaye alifariki Machi mwaka 2007. Mzee Philip amefanya mambo makubwa kwa watu wa Mpanda Kati na ndio maana wenyewe wakataka kumkumbuka kwa kuandaa ligi ya mpira wa miguu ambayo kwa sasa iko katika hatua ya robo fainali,” alisema Mbogo.

Alisema ligi hiyo inashirikisha timu 13 na imeanza tangu Februari 26 mwaka huu na inatarajiwa kumalizika Machi 22 mwaka huu.

“Kila timu inayoshiriki ligi hiyo itapewa seti moja ya jezi na mpira mmoja,” alisema Mbogo.

Alizitaja timu zinazoshiriki ligi hiyo kuwa ni Mpanda United, Magereza FC, Makanyagio FC, Katavi Rangers, Reli Katumba, Kagera FC, Mwangaza Sekondari, Nselemwa Sekondari, Bufalo FC, Small Kids FC, Kazima FC, Kiboko FC na Mpanda Stars.

Katika hatua nyingine, alisema ligi hiyo itasimamiwa na Chama cha Mpira Wilaya ya Mpanda (MDFA).
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom