Sijui tuseme ndio urafiki umeshamili au limetokea kwa bahati mbaya. Kwa mara ya kwanza niliona nguo zenye chata ya Tanzania zikiuzwa madukani Uchina ni zile za Kappa. Baada ya muda, nikapita mtaani nikaona wajasiria mali wamefyotoa za kwao ila wamekosea jina, nikasema bora na mimi nijipatie yangu moja kuonesha uzalendo nikagundua jamaa wamekosea jina, badala ya TanzanIa wao wameandika TanzanLia, ndio hivyo walenga walisema kazi ya mikono....
Upande wa mbele wa kofia ya karume kama ilivyokutwa na mdau wa kidarubini
Katika sherehe ya muungano tukiwa katika kubadirishana mawazo na mdau wa Blog ya Kidarubini, aliniambia kuwa ameona kofia za karume mtaani, nikadhani ni uzushi kwakuwa mara nyingi tumezoea kupiga matani, akasisitiza na kusema atanitumia picha. Leo asubuhi bila hiyana nimepata picha zikionesha kofia ya Rais mstaafu wa visiwani ikiwa sokoni, tena ni kofia ya kampeni, lol. Sasa swali nnalojiuliza ni imekuwaje hapa, je ni zile zilizobaki wakati wa kampeni? Ila kampeni ilikuwa ni miaka saba iliyopita. Nimekosa jibu hivyo napenda kuwauliza wana Ughaibuni munalionaje hili?
Kofia ya karume ikiwa sokoni, bei ni yuan 10 ambayo ni sawa na shilingi 2600 ya bongo.
Source: Ughaibuni.com