Kodi za gari barabarani lisipoingiliwa vizuri linaweza kuwa janga kwa watu wengi

Nishauza gari ndogo 6 za Biashara, na zote zina Jina langu kamili.
Sina uhakika kama hao ambao niliwauzia wamebadilisha majina, na hata sijui ntawapata wapi kikitokea kimeo chochote kinachohusu kodi kwa Gari nilizouza, (ikiwa hawajabadili umiliki).
Kwa hakika tumbo linasokota niliposoma habari hii.
Uvuvi wa kufanya kazi unawafanya wabuni njia za uonevu ili kurahisisha kazi zao.
 
Hii sheria ya TRA kwamba kama uliuza gari lakini aliyenunua akubadilisha umiliki kodi utadaiwa wewe kwa nini gari yenyewe isijisimamie yenyewe, kama hailipiwi kodi ikamatwe gari husika maana kila gari inajitegemea kwa usajiri wake.

gari kama iko geraji kutokana na mtu kukosa pesa ya kutengeneza au kutokuwepo vipuri vyake, kwa nini wasisubiri siku ikiingia barabarani ikamatwe.

Mwisho kuna gari zimepata ajali ambazo gari hazitengenezeki kabisa, watu wakauza kama chuma chakavu na ripoti za polisi wakatupa maana walijua mwisho wa gari umefika, mfano kuna mabasi na malori, malori mengine yamepata ajali nje ya nchi kama Congo au Zambia wakakata kama chuma chakavu watalipaje hizo faini kubwa hivyo, maana wengine wameshapoteza malori na mabasi mengi aliyopata ajali.

TRA yenyewe ilikuwa haitoi elimu vizuri kuhusu kodi za gari,
Ili kunusuru watu kwenye hili janga ni bora kuwaambia watu wote wenye gari gereji ambazo hazitengeneki na waliyokata kama chuma chakavu waripoti TRA ili zifutwe baada ya hapo ndio sheria ianza kutumika ipasavyo, la sivyo wananchi wengi wataingia kwenye matatizo makubwa maana wengine hiyo pesa hawana tena na hawakufanya kwa maksudi.

Nawasilisha.
Mnapanic nini? Kwani jukumu la kubadili jina ni la muuzaji? We uliyeuza si una sale agreement? Unless hamkuandikiana. Sale agreement tosha kumlinda muuzaji. Sio jukumu langu kuhakikisha kuwa aliyenunua amebadili jina maana tumeandikishiana kihalali kabisa.
 
Nishauza gari ndogo 6 za Biashara, na zote zina Jina langu kamili.
Sina uhakika kama hao ambao niliwauzia wamebadilisha majina, na hata sijui ntawapata wapi kikitokea kimeo chochote kinachohusu kodi kwa Gari nilizouza, (ikiwa hawajabadili umiliki).
Kwa hakika tumbo linasokota niliposoma habari hii.
Uvuvi wa kufanya kazi unawafanya wabuni njia za uonevu ili kurahisisha kazi zao.
Usijali we utaonyesha proof kama ulishauza hayo magari. Kutobadili ni kosa la jinai kwa yule aliyenunua kwani anakuimpersonate wewe wakati ulishamuuzia. Anatakiwa abadili jina na alipe kodi kwa jina lake sio la mtu mwingine.
 
Umenikumbusha machungu! Ilikamatwa gari yangu na nikaambiwa nadaiwa, nilipokwenda Tra na kuwaambia sidaiwi kwa kuonyesha nakala zangu ila wakasema unadaiwa gari ya zamani na hujailipia tangu elfu mbili na kumi.
Hiyo ni gari niliyomuuzia mtu tangu mwaka huo na hata alipo sijui, ilibidi tu nilipe hizo milioni tatu ili niikomboe gari hii.
Eh!!! Hata baada ya kuonyesha sale agreement? Huu sasa ni wizi.
 
Yaani pesa inatafutwa kibabe sana siku hizi, elimu hatujapewa na kudaiwa tutalazimishwa. Itafika mahali tutashindwa kulipia hayo magari yatakayokamatwa watahamia kwenye mali zingine kama nyumba na mashamba..
 
Hii sheria ya TRA kwamba kama uliuza gari lakini aliyenunua akubadilisha umiliki kodi utadaiwa wewe kwa nini gari yenyewe isijisimamie yenyewe, kama hailipiwi kodi ikamatwe gari husika maana kila gari inajitegemea kwa usajiri wake.

gari kama iko geraji kutokana na mtu kukosa pesa ya kutengeneza au kutokuwepo vipuri vyake, kwa nini wasisubiri siku ikiingia barabarani ikamatwe.

Mwisho kuna gari zimepata ajali ambazo gari hazitengenezeki kabisa, watu wakauza kama chuma chakavu na ripoti za polisi wakatupa maana walijua mwisho wa gari umefika, mfano kuna mabasi na malori, malori mengine yamepata ajali nje ya nchi kama Congo au Zambia wakakata kama chuma chakavu watalipaje hizo faini kubwa hivyo, maana wengine wameshapoteza malori na mabasi mengi aliyopata ajali.

TRA yenyewe ilikuwa haitoi elimu vizuri kuhusu kodi za gari,
Ili kunusuru watu kwenye hili janga ni bora kuwaambia watu wote wenye gari gereji ambazo hazitengeneki na waliyokata kama chuma chakavu waripoti TRA ili zifutwe baada ya hapo ndio sheria ianza kutumika ipasavyo, la sivyo wananchi wengi wataingia kwenye matatizo makubwa maana wengine hiyo pesa hawana tena na hawakufanya kwa maksudi.

Nawasilisha.
Upo sahihi kbs tatizo kubwa nchi yetu hao TRA wanafanya mambo kwa kukomoana Elimu hawakutoa lkn watakueleza sheria msumeno bila kuzingatia huyo mlipa kodi akupata Elimu hiyo kabla ila ndio hivyo tna wacha tuisome namba
 
Tatizo ninalioliona ni kuwa TRA hawatoi elimu kwa wahusika. Yan mambo yamekuwa ni kuviziana. Kwani wanashindwa nini kutoa elimu elekezi kuhusu hilo. Watuambie ni sehemu gani imeandikwa gari ukiuza au ikiharibika tukatoe taarifa kwao.mbona hayakusemwa kipindi chote hicho mpaka leo umeingia uongozi mpya ndio tuishi kwa kuchimbua hizo wanazosema sheria ingawa sijui zipo kwenye kitabu gani.
Sheria kama zipo,mwenye jukumu la kuzitolea elimu ilikuwa ni TRA wenyewe,watu wa kitengo cha elimu jwa mlipa kodi wanalipwa mshahara wa kazi gani,wanavimba matumbo tu,basi hapo wakihojiwa siasa nyingiii,hawa ni wakufukuza tu,teua kitengo kipya.
 
Tatizo TRA, huwa hawatoi elimu kwa mlipa kodi, huwa wanafanya vitu kama kutukomesha raia
 
Tanxania watu wapo kwa ajili ya kukomoana tuu na ndio chanzo cha umasikini wametolea macho magari mafita yanapita bila import duty, dhahabu Accasia mining wanatudai VAT wao wanapata faida kwenye uchimbaji dhahabu lakini still hawalipi kitu..magari ndio yamegeuka kuwa ndio madini kwa TRA..
 
Jambo la muhimu ni serikali kubadili mfumo huu uchwara wa kukimbizana na Road License kwa kuwalipisha watu ambao magari yao yamepaki nyumbani au gereji.
Mtu hatumii barabara halafu analipa ushuru wa barabara.

Kuna wazo zuri sana la kuiweka Road license kwenye mafuta.
Ili mtu alipie kwa kadiri anavyotumia barabara.

Lakini pia kila mtu anapouza gari anakua na formu ya mauziano.
Huwezi kuuza au kununua gari kama karanga bila mkataba wa mauziano.
Hivyo serikali haina nia ya kumuumiza mtu yeyote kwa hili la Road License. Hapa kila mtu aliyenunua gari kihalali atalipa R. L kwa kipindi alichotumia gari.
Tatizo linakuwa kwa wale waliopark magari yao bila kutoa taarifa.Hapa serikali itoe ufafanuzi kamili.
Unajua mfumo wao unavyofanya kazi au umeandika kitu usichokijua?
Ni hivi÷
Gari yenye jina la mtu mwingine,na mtu huyo anayoa au alikuwa na magari mengine,pengine ameyauza au yapo ila hayatembei wao wanahesabu tu roadlicence,kwahiyo wakiikamata gari yoyote yenye jina la mmiliki huyo,liwe linadaiwa au la,basi wewe kutumia gari hilo utalipa madeni mengine ya mmiliki huyo kwakuwa wao wanachukulia kuwa gari hiyo ni yake.
Sasa wewe huna deni kwenye gari yako,inakaaje kwao au unalipaje deni usilolijua.
Hii ni sawa na gari yako aendeshe mtu mwingine ikiwa ilifanya kosa la barabarani trafiki wanakamata gari badala ya aliyefanya kosa na hawaliachii mpaka ulipe,sasa si ni uonevu huo,wakati aliyefanyakosa wamechukua details za leseni yake kwanini wasimsubiri wakati wa renewal.
 
Yani kodi zimekuwa kama adhabu maana zinatengenezewa mazingira ambayo mlipaji anaonekana kama mtu mwenye hatia tu. Hili linapaswa kutolewa elimu ya kutosha na kuhamasisha watu kulipa kodi. TRA badilikeni bana. Anzisheni kampeni maalumu ya kuelimisa watu katika maswala ya kodi. Tengenezeni vi clip vya video na audio visungunge watsapp fb , Instagram nk. Wadau ni wateja wenu hawa na sio maadui.
 
Hewalaa!, kodi zimekuwa ni adhabu sasa, na usipolipa (hata kwa sababu zilizo nje ya uwezo) utatozwa na faini juu.
 
Nishauza gari ndogo 6 za Biashara, na zote zina Jina langu kamili.
Sina uhakika kama hao ambao niliwauzia wamebadilisha majina, na hata sijui ntawapata wapi kikitokea kimeo chochote kinachohusu kodi kwa Gari nilizouza, (ikiwa hawajabadili umiliki).
Kwa hakika tumbo linasokota niliposoma habari hii.
Uvuvi wa kufanya kazi unawafanya wabuni njia za uonevu ili kurahisisha kazi zao.
Mkuu naamini katika mauziano yenu kutakuwa na mawasiliano ya hao watu Anza kuwasaka hii issue ni kimeo na pia hata gari Hizo zikifanya tukio either ajali au ujambazi serikali ita hangaika na wewe mpaka kuja kujiridhisha uliuza Hizo gari umeshateseka sana kama sio kuozea kabisa Segerea
 
Unajua mfumo wao unavyofanya kazi au umeandika kitu usichokijua?
Ni hivi÷
Gari yenye jina la mtu mwingine,na mtu huyo anayoa au alikuwa na magari mengine,pengine ameyauza au yapo ila hayatembei wao wanahesabu tu roadlicence,kwahiyo wakiikamata gari yoyote yenye jina la mmiliki huyo,liwe linadaiwa au la,basi wewe kutumia gari hilo utalipa madeni mengine ya mmiliki huyo kwakuwa wao wanachukulia kuwa gari hiyo ni yake.
Sasa wewe huna deni kwenye gari yako,inakaaje kwao au unalipaje deni usilolijua.
Hii ni sawa na gari yako aendeshe mtu mwingine ikiwa ilifanya kosa la barabarani trafiki wanakamata gari badala ya aliyefanya kosa na hawaliachii mpaka ulipe,sasa si ni uonevu huo,wakati aliyefanyakosa wamechukua deyails za leseni yake kwanini wasimsubiri wakati wa renewal.

Ndio maana nikasema kuwa tatizo litakua kwa wale waliokuwa wamepaki magari yao tu bila kutembea barabarani.
Hawa watajikuta wanalipia ushuru wa barabara wakati hawakuitumia na hawakujua umuhimu wa kwenda kutoa taarifa TRA.

Kwa upanda wa kuuzuana nimesema kuwa kuna mkataba wa mauziano.
Umeandikwa tarehe na mwaka uliouza gari na kuna madhahidi.
Tena siku hizi kuna form za mauziano zinatolewa hata TRA mara nyingine wamekua wakizitoa.
Hizi form zinapelekwa mahakamani na kugongwa muhuri na sahihi ya hakimu.
Kwa hiyo sio rahisi kwa muuzaji mwenye mkataba wa mauziano kuingia kwenye deni la mteja aliyenunua.
Hapa atakayekamatwa na kushitakiwa ni mnunuzi.
Na kwa mifumo ya sasa hata akijificha kuna siku atakamatwa tu .
 
Hii sheria ya TRA kwamba kama uliuza gari lakini aliyenunua akubadilisha umiliki kodi utadaiwa wewe kwa nini gari yenyewe isijisimamie yenyewe, kama hailipiwi kodi ikamatwe gari husika maana kila gari inajitegemea kwa usajiri wake.

gari kama iko geraji kutokana na mtu kukosa pesa ya kutengeneza au kutokuwepo vipuri vyake, kwa nini wasisubiri siku ikiingia barabarani ikamatwe.

Mwisho kuna gari zimepata ajali ambazo gari hazitengenezeki kabisa, watu wakauza kama chuma chakavu na ripoti za polisi wakatupa maana walijua mwisho wa gari umefika, mfano kuna mabasi na malori, malori mengine yamepata ajali nje ya nchi kama Congo au Zambia wakakata kama chuma chakavu watalipaje hizo faini kubwa hivyo, maana wengine wameshapoteza malori na mabasi mengi aliyopata ajali.

TRA yenyewe ilikuwa haitoi elimu vizuri kuhusu kodi za gari,
Ili kunusuru watu kwenye hili janga ni bora kuwaambia watu wote wenye gari gereji ambazo hazitengeneki na waliyokata kama chuma chakavu waripoti TRA ili zifutwe baada ya hapo ndio sheria ianza kutumika ipasavyo, la sivyo wananchi wengi wataingia kwenye matatizo makubwa maana wengine hiyo pesa hawana tena na hawakufanya kwa maksudi.

Nawasilisha.
NARUDI SEHEMU MOJA UKINISAIDIA HII UTANIELEWA

UNAPOANZISHA BIASHARA YA DAWA ..UKAWA UNALIPA KODI KUNASEHEMU WANAKWAMBIA KAMA UTAACHA KUUZA UWANDIKIE BARUA..ULISHAWAH JUA SABABU ZA ILE BARUA MPWA....N KWAMBA KAMA HUKUANDIKA UKAJA MWAKAN NA BIASHARA YA PEMBEZANDOVU TIN ILEILE UNALIPAKWANZA PESA YOTE YANYUMA NDIO UNAENDELEA NA PEMBEZAKO
 
Mkuu naamini katika mauziano yenu kutakuwa na mawasiliano ya hao watu Anza kuwasaka hii issue ni kimeo na pia hata gari Hizo zikifanya tukio either ajali au ujambazi serikali ita hangaika na wewe mpaka kuja kujiridhisha uliuza Hizo gari umeshateseka sana kama sio kuozea kabisa Segerea
Umeuza gari miaka 8 iliyopita bado unaishi na namba ya aliyekuwa mnunuzi tu,?maisha ya wasiwasi sana hayo,ndiyo maana magonjwa ya shinikizo la damu yamekuwa mengi sana sasa hapa Tanganyika.
 
Vitu kama hivi ndo tulitegemea wabunge wetu watuwakilishe huko bungeni,lakini badala yake baadhi yao wanaona muhimu ni kuonekanana "live" kwenye luninga.kwa hili TRA wanatuburuza.
Huo ndio ukweli. Wabunge wangekua serious kwa mambo kama haya. Kuna watu masikini kabisa gari zao zilikua chini kwa pengine hata miaka tano kwa kukosa hela ya kutengeneza. Leo hii akitaka kulifufua anatakiwa alipie road license kwa muda wote lilipokua chini. Magari mengi ya aina hiyo sasa yanafanya shughuli za usiku tu. Akikamatwa anatoa kitu kdg serikali inaendelea kukosa mapato.
 
Back
Top Bottom